Papa Francisko amemtea Monsinyo Gianfranco gallone kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Zambia Papa Francisko amemtea Monsinyo Gianfranco gallone kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Zambia 

Mons. Gianfranco Gallone, ateuliwa kuwa Balozi nchini Zambia

Askofu mkuu mteule Gianfranco Gallone, alizaliwa tarehe 20 Aprili 1963 huko Ceglie Messapica, Brindis, Kusini mwa Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 3 Septemba 1988.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, hivi karibuni amemteuwa Monsinyo Gianfranco Gallone, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Zambia na wakati huo huo kumpandisha hadhi na kuwa Askofu mkuu. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Gianfranco Gallone, alizaliwa tarehe 20 Aprili 1963 huko Ceglie Messapica, Brindis, Kusini mwa Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi akapewa Daraja Takatifu ya Upadre hapo tarehe 3 Septemba 1988.

Baadaye akajiendeleza zaidi na kujipatia Shahada ya Uzamivu katika Sheria za Kanisa na Taalimungu ya Liturujia. Askofu mkuu mteule alianza kufanya utume wake hapa mjini Vatican tarehe 19 Juni 2000 na kubahatika kutekeleza dhamana na utume wake huko Msumbiji, Israeli, Slovacchia, India pamoja na Sweden. Mwishoni, alihamishiwa kwenye Sekretarieti kuu ya Vatican, Idara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Balozi Zambia 2019

 

12 February 2019, 10:23