Tafuta

Vatican News
Askofu Mkuu Paul Gallagher Katibu Mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican Askofu Mkuu Paul Gallagher Katibu Mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican   (ANSA)

Askofu Mkuu Gallgher:Haki za binadamu na mazungumzo kati ya dini

Katibu Mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher ametoa hotuba yake mjini Geneva katika kikao cha 40 kwa ajili ya haki za binadamu za Umoja wa Mataifa.Kiini cha hotuba yake ni uhamasishaji wa haki za binadamu na mazungumzo ya kidini kuwa uwe ufunguo wa amani na maendeleo

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mazungumzo kuhusu mtazamo wa sheria ya kimataifa wa haki za binadamu zenye msingi wa hadhi ya kila binadamu ni hali inayohitajika kuhamasisha amani ya kudumu, hata kama chombo mwafaka kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo y binadamu fungamani na ambayo haiwezi kutoanzia katika huru wa dini, dhamiri na mazungumzo ya kidini. Ndiyo dhana msingi wa hotuba ya Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican aliyotoa  tarehe 25 Februari 2019 katika kikao cha 40 mjini Geneva cha Baraza la haki za binadamu za Umoja wa Mataifa.

Haki msingi za binadamu zinatishiwa na haki mpya

Katika hotubayake, Askofu Mkuu amekumbasha ni kwa jinsi gani ulinzi na uhamasishaji wa haki za binadamu kuwa moja ya nguvu za Umoja wa Mataifa na msingi wa maadili wa mahusiano ya kimataifa leo hii. Kufanya kazi kwake pamoja na ni moja ya lengo msingi wa shughuli za Vatican  kwa makubaliano kimataifa. Kwa bahati mbaya anaonesha Askofu Mkuu Gallagher kuwa, haki hizo ziko hatarini  kwa sababu ya mfumo na maendeleo ambayo yamegawanya asili ya binadamu ambaye anafungua njia iitwayo nyingine iitwayo“ haki mpya”. Na si mara chache inatokea migogoro kati yake, kama alivyokuwa amekweisha sema Baba Mtakatifu Francisko. Yeye alithibitisha kuwa, ukosefu wa uwezo wa kutambua asili yetu ya pamoja, msingi ambao unasimika haki zote, ni kugeuka ukiukwaji wa haki msingi za kibinadamu na kudhoofika kwa kina ubinadamu wote.

Wasiwasi juu ya ongezeko la ukiukwaji wa uhuru wa dini

Hata hivyo akiendelea na hotuba yake, Askofu Mkuu ameonesha wasiwasi mkubwa walio nao Vatican juu ya kuongezeka ukiukwaji wa haki za uhuru wa dini katika ibada za dini na imani. Haki hiyo msingi amekumbusha kuwa, haiwezi kamwe kuendelea kuwekewa vizingiti katika mzuzunguko binafsi, badala yake  kama inavyothibitisha Hati ya Mtaguso kuhusu hadhi ya binadamu “Dignitatis Humanae”, lazima itambuliwe hata kwa waamini katika matendo yao kijumuiya na kuwa na nafasi yao ya dharura katika mpangilio wa umma. Hiyo ina maana kwamba haki yenyewe ya dini inayoadhimishiwa kwa pamoja ibada, kuchagua viongoz wao wa kidini, kueneza ujumbe wao kwa njia ya vyombo vyote vya kisasa na kiutamaduni. Lakini pia inajikita kuwa na uwezekano wa waamini wake kuchangia kwa mijibu wa maoni yao ya kidini, mijadala ya kijamii, kisiasa, kiutamaduni na mpangilio wa kimataifa.

Uhuru na mazungumzo ya kidini ni ufunguo wa  maendeleo kufikia ajenda ya 2030

Askofu Mkuu Gallagher pia amesistiza ni kwa jinsi gani uhuru wa dini na dhamiri pamoja na kuhamasisha mazungumzo kati ya dini  ni hali msingi kwa ajili kutumiza ajenda ya maendeleo endelevu ifikapo 2030.  Anasema: iwapo tunataka kujikita kwa dhati juu ya hatua zilizochukuliwa miaka minne iliyopita na kupitia kutoka  maamuzi hadi  kufikia matendo, tunapaswa kwenda  zaidi ya lugha ya uchumi na takwimu na kufikia ukuu kimaadili, kitasaufi na kidini, mambo ambayo hayawezi kudharauliwa kwa maana ya kuleta  madhara ya binadamu na maendeleo yake kamili. Hii ina maana hata katika  hati ya pamoja iliyotiwa sahini hivi karibuni huko Abu Dhabi na Baba Mtakatifu Francisko na Imam Mkuu wa  Al-Azhar, Ahmad Al-Tayyib, ambapo inasisitiza juu ya mazungumzo, uelewa, kuendelea kwa utamaduni wa kuvumiliana, kumkubali mwingine na kuishi kwa pamoja kati ya binadamu katika kuchangia kwa kiasi kikubwa ili kupunguza matatizo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na mazingira ambayo yamezungukwa na sehemu kubwa ya binadamu.

Jitihada za Vatican katika ulinzi wa wadogo

Mada nyingine ambayo Askofu Mkuu Gallagher amegusia katika kuhitimisha ilikuwa ni ile ya ulinzi wa watoto. Katika pendekezo hili amependa kusisitizia juu ya jitihada za Vatican, si kwa ajili ya kuhakikisha tu usalama na ulinzi wa ushirikishwaji swa watoto na watu wazima waathirika, lakini pia hata kuunda mazingira salama kwa ajili yao kwenye taasisi ili kuendelea na shughuli dhidi ya janga hili la nguvu dhidi ya watoto.

27 February 2019, 16:28