Tafuta

Papa Francisko amemteua Monsinyo Ante Jozic kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Pwani ya Pembe. Papa Francisko amemteua Monsinyo Ante Jozic kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Pwani ya Pembe. 

Monsinyo Ante Jozic ateuliwa kuwa Balozi, Nchini Pwani ya Pembe!

Monsinyo Ante Jozic, ameteuliwa na Papa Framncisko kuwa Balozi mpya wa Vatican huko Pwani ya Pembe na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu. Askofu mkuu mteule Ante Jozic alizaliwa tarehe 16 Januari 1967 huko Trilj, nchini Croatia. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, tarehe 28 Juni 1992 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, hivi karibuni amemteua Monsinyo Ante Jozic, kuwa Balozi mpya wa Vatican huko Pwani ya Pembe na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu. Askofu mkuu mteule Ante Jozic alizaliwa tarehe 16 Januari 1967 huko Trilj, nchini Croatia. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, tarehe 28 Juni 1992 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Monsinyo Ante Jozic, akajiendeleza zaidi katika masomo ya Sheria, Kanuni na Taratibu za Kanisa na kujipatia Shahada ya uzamivu katika Sheria za Kanisa. Tarehe 1 Julai 1999 akaanza utume wa kidplomasia mjini Vatican. Katika kipindi chote hiki, amewahi kufanya utume wake kwenye Ofisi za Ubalozi wa Vatican huko: India, Urussi na Ufilippini.

Balozi Pwani ya Pembe

 

12 February 2019, 10:13