Askofu Mkuu Auza wakati wa hotuba yake tarehe 5 Februari 2019 mjini New York.Ni mkutano ulioongozwa na mada ya mazungumzo ya kidini ya New York Askofu Mkuu Auza wakati wa hotuba yake tarehe 5 Februari 2019 mjini New York.Ni mkutano ulioongozwa na mada ya mazungumzo ya kidini ya New York  

Ask.Auza mafundisho ya dini yanachangia amani na uhuru wa kweli!

Askofu Mkuu Auza wakati wa hotuba yake katika Toleo la nane la wiki ya maelewano ya Umoja wa Mataifa mjini New York amesema mazungumzo ya kweli yanatakiwa kila mmoja awe na shauku ya kujijua,ya kukua na kuwa na ufahamu wa kina wa pamoja.Kila mmoja anatakiwa awe mfereji wa kidugu

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 5 Februari 2019, Askofu Mkuu Bernadito Auza, mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, ametoa hotuba yake katika Mkutano ulioongozwa na mada ya Mazungumzo ya Kidini ya New York:kujenga mshikamano kijamii na jumuiya ya pamoja,ambapo amejikita kukazia juu ya mazungumzo ya kidini na amani. Katika hotuba yake inaonesha mada msingi ya Waraka wa udugu kibinadamu kwa ajili ya amani duniani na kuishi kwa pamoja hasa ikiwa ni mada ambayo imefungwa katika mchakato wa ziara ya Baba Mtakatifu Francisko katika Falme za nchi za Kiarabu na kwamba, mafundisho ya dhati ya dini yanachangia amani na uhuru wa kweli kupambana na ugaidi, kuhakikisha hupatikanaji wa mafunzo na kazi hasa kwa wanawake na kulinda watoto, wazee na wadhaifu. Ikiwa ni katika kuadhimisha toleo la nane la Wiki ya Maelewano ya Kidini katika Umoja wa Mataifa, Askofu Mkuu Auza katika hotuba yake amesisitiza kwa dhati juu ya mazungumzo ya kidini, ambapo amepata hata fursa ya kuwakabidhi nakala ya waraka wa Baba Mtakatifu Francisko. Katika hotuba yake Askofu Mkuu Auzia amejikita kwa dhati kurudia na kukazia maneno ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa fursa ya kutia sahini Waraka huo mjini Abu Dhabi!

Mfereji wa kidugu na kushirikishana furaha na uchungu

Mazungumzo ya kidini ni suala la lazima la amani katika dunia, ni msingi wa kuhakikisha maendeleo ya binadamu. Na kwa kusisitiza ametaja jinsi gani ilivyo kashifa kwa Mungu kila mara wanapotumia jina lake katenda vurugu dhidi ya ndugu. Ukweli wa huruma ya kidini daima unatakiwa kumpenda Mungu na jirani. Ili kujenga jumuiya ya pamoja ni lazima dini zote na watu wa imani wawe mfereji wa kidugu. Askofu Mkuu Auza anabainisha tena kwamba, Baba Mtakatifu Francisko anapenda kuzungumzia juu ya mazungumzo ya kidini kama suala la kutembea pamoja (caminar juntos) mahalia ambapo watu wa dini tofauti na utamaduni wanaanza kijadiliana na maisha,wanashirikishana furaha na uchungu.

Kuwatambua watu wengine ni moja ya mtindo wa kukuza maelewano

Mantiki nyingine ambayo imeoneshwa na Askofu Mkuu Auza juu ya Baba Mtakatifu Francisko ni ile ya ujasiri wa hali ya juu na ulinzi wa kibinadamu, na haki ya mwingine zikiwemo haki za dini, la sivyo anasema haiwezekani kuwapo mazungumzo ya kweli. Ni lazima kwa namna hiyo kujua historia na utamaduni wa wengine na matatizo yanayotokana na ukosefu wa utambuzi wa kile ambacho wengine wanaamini.” Mazungumzo ya kweli yanatakiwa kila mmoja awe na shauku ya kujijua, ya kukua na kuwa na ufahamu wa kina wa pamoja anasema Askofu Mkuu Auza.  Kadhalika mazungumzo pia yanahitaji yawe ya kina na haki kidugu. Udugu wa kweli unasadia maelewano ya kidini ya dhati na amabayo yanaweza kusaidia kudumisha maendeleo fungamani na mshikamano.

Matokeo ya mazungumzo ya kidini

Akisisitiza zaidi juu ya mtindo huo wa mazungumzo ya kidini  amejikita Askofu Auza hawali ya yote kuonesha jamii nzima ambayo inapaswa kukabiliana na masuala muhimu, kama vie kufanya kazi yenye hadhi katika nyakati za kipindi kigumu, mahali ambapo panaonesha mpasuko wa kijamii. Na  sehemu ya pili ambayo inatakiwa kufanyiwa kazi pamoja ni katika mipango ya kusaidia maskini,katika elimu ya watoto yatima na mambo mengine ya msaada. Na hii inajikita katika ulimwengu ambao unatafuta kumwondoa Mungu kwenye maisha ya umma, hivyo ushirikiano kati ya waamini utasaidia kuhakikisha ya kuwa Jina la Mungu lisiweze kusahaulika, hata upendo wa Mungu hasa kwa wale wenye kuhitaji na wasiweze kuwa na ubaridi kamwe katika maisha ya kibinadamu.

Matokeo ya tatu  ya mazungumzo ya kidini ambayo Askofu Mkuu Auza anabainisha katika hotuba yake ni mtindo wa mazungumzo ya kidini, ambao unasaidia uwezekano wa ushuhuda wa dhati dhidi ya virugu za chini chini za kidini, ambapo dini zinasaidia kusafisha vumbi ambalo wakati mwingine linajitokeza, hivyo si kusaidia tu katika kushinda ukosefu wa maelewano ya pamoja na ambayo yanaweza kuonekana katika ndugu kama adui, badala yake yanaweza kuonesha thamani za kidini na ambazo zinaweza kuonesha na kuendelezwa kati ya kizazi na kizazi ili kuhakikisha kuwa zinahamasisha maelewano na siyo chuki. Mwisho Askofu Mkuu Auza anathibitisha kwamba, mazungumzo ya kidini yanatoa ushuhuda mkubwa wa kidini na umuhimu wa ukuu wa Mungu na kibinadamu, kwa maana hiyo ni matarajio yake kwamba, majadiliano haya  kwa ngazi ya juu katika mwelekeo wa hatua ya kijumuiya yanaweza kweli kusaidia katika maendeleo ya dhati na amani.

 

 

06 February 2019, 15:00