Uwakilishi wa nchi za Falme za Kiarabu kukutana na Papa Francisko katika nyumba ya Mtakatifu Marta Vatican  Uwakilishi wa nchi za Falme za Kiarabu kukutana na Papa Francisko katika nyumba ya Mtakatifu Marta Vatican  

Urafiki kuongeza nguvu kati ya Kanisa na Uislam!

Baada ya siku 20 tangu ziara ya Baba Mtakatifu Francisko katika nchi za Falme za Uarabuni,uwakilishi kutoka katika Pensula hiyo umefika Vatican na kumweleza juu ya matunda ya kwanza ya maamuzi ya Hati iliyotiwa saini tarehe 4 Februari na Imam mkuu wa al-Azhar

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Dk.Gisotti Msemaji mkuu wa habari Vatican ameviambia vyombo vya habari kuwa Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa  Falme za nchi za Uarabuni Sheiki Abdallah Ben Zayed Al Nahyan,  tarehe 25 Februari 2019 saa 6.30 mchana masaa ya Ulaya.

Katika fursa hiyo hawa wamepata kuzungumza kwa karibia dk 45. Waziri Ben Zayed amependa kumtaarifu Baba Mtakatifu juu ya maamuzi ambayo serikali za Falme za Uarabuni wamechukua ili kuhamasisha kwa makini Hati iliyotolewa juu ya udugu wa kibinadamu kwa ajili ya Amani duniani na kwa ajili ya kuishi kwa pamoja, ambayo ilitiwa saini na Baba Mtakatifu Francisko na Imam wa  Al-Azhar Ahamad al-Tayyib (Abu Dhabi, tarehe  4 Februari  2019).

Hata hivyo wathibitisha kuwa, baadhi ya mambo yameshaanza na mengine yako katika mchakato wa matendo. Hata uwakilishi huo umemzawadia Baba Mtakatifu Kasanduku ndani mwake kukiwa na mawe yaliyo andikwa kwa lugha ya kiarabu, ikielezea ujumbe ambao unahusiana na upendo,uvumilivu na udugu.

Na Baba Mtakatifu Francisko ametoa zawadi ya sanaa ya mchongo wa karne XVII unaoonesha kazi ya ujenzi wa Uwanja wa Mtakatifu Petro na album kubwa nne za picha kwa ajili ya Rais na makamu wa Nchi za Falme za Uarabuni, zenye picha nzuri sana za ziara ya Baba Mtakatifu Francisko katika nchi hiyo hivi karibuni. Na mwisho wa mkutano na Baba Mtakatifu Francisko amepata chakula cha pamoja na Waziri huyo na wawakilishi kutoka nchi za Falme za uarabuni.

26 February 2019, 10:55