Tafuta

Vatican News
Wiki ya kuombea Umoja wa wakristo duniani 18-25 Januari 2019 Wiki ya kuombea Umoja wa wakristo duniani 18-25 Januari 2019  (ANSA)

Wiki ya kuombea umoja wa wakristo 18-25 Januari 2019!

Ijumaa tarehe 18 Januari 2019 saa 11.30 jioni masaa ya Ulaya kutakuwapo na masifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo mjini Roma, yatakayoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa uwakilishi wa viongozi mbalimbali wa kikristo wakati wa kuanza Wiki ya Kuombea Umoja wa Wakristo, inayoongozwa na mada, tafuteni kuwa wenye haki kweli

Na Sr. Angela Rwezaula –Vatican

Wiki ya Maombi kwa ajili ya Wakristo mwaka 2019 imeandaliwa na wakristo nchini Indonesia. Katika nchi ambayo idadi ya watu wake inadi milioni 265, lakini asilimia 86% ni dini ya kiislam, asilimia 10% tu ndiyo inaundwa na wakristo wa utamaduni tofauti. Katika kuadhimisha wiki hii, Baraza ka Kipapa la uhamasishaji wa umoja wa Wakristo wanaandika kuwa, ufisadi umejionesha katika mitindo mbalimbali; unashambulia katika sera za kisiasa na katika ulimwengu wa biashara, ambapo mara nyingi matokeo yake mabaya yanajionesha katika mazinginra, kwa mfano, hatari za ukosefu wa haki na kutungwa kwa sheria kandamizi. Na mara nyingi wale ambao wanapaswa kuhamasisha hakina kulinda wadhaifu ndiyo wanatenda kinyume na matokeo yake ni kuongezeka utofauti mkubwa kati ya matajiri na maskini, wakati nchi yenye kuwa na utajiri wa rasilimali, inaashia katika kashfa nyingi kuwa na watu wengi ambao wanaishi katika hali ya umaskini wa kukithiri.

Kuwa wenye haki kweli

Kwa upande wa wakristo wa Indonesia, maneno kutoka katika Kitabu cha Kumbukumbu la Torati:“ tafuteni kuwa wenye haki kweli” (Kut 16,18-20), inaangazia hali yao, kwani jumuiya nyingi za kikristo zinageuka kuwa na utambuzi wa umoja wao, iwapo inajitokeza lengo la maelewano ya pamoja na kuwa na jibu moja, la pamoja katika hli halisi ya ukosefu wa usawa. Wakati huo mbele ya ukosefu wa haki hizo, kuna ulazima kama wakristo wote kufanya tathimini za mitindo ambayo inaweza kuwahausha wote  ili kukabiliana na mtindo hii ya ukosefu wa haki. Ni katika  njia ya kusikiliza utashi wa Yesu tu aliyesema:“ ili watu wote wawe kitu kimoja” (Yh 17,21) tunaweza kweli kuwa mashuhuda wa kuishi umoja katika utofauti. Ni kwa njia ya umoja wetu katika  Kristo tunaweza kufikia hatua ya kupambania haki na kuondolea mbali ukosefu wa haki na kuwasaidia haraka iwezekanvyo waathrika wake.

Kualikwa kusali kwa ajili ya umoja

Mwaka huu mara baada ya Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 16 Januari 2019, amewakumbusha waamini na mahujaji juu ya wiki ya kuombea umoja wa Wakristo kuanzia tarehe 18-25 Januari 2019.  Mada inayoongoza maombi hayo ni “tafuteni  haki ya kweli”. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kwamba, hata mwaka huu tunaalikwa kusali ili wakristo wote warudie kuwa familia moja ya dhati kwa utashi wa Mungu anavyopenda kuwa “wote wawe wamoja”, (Yh 17, 21). Na katika kusisitiza zaidi amesema: “Uekumene siyo jambo la uchaguzi. Lengo litakuwa ni lile la kukuza muungano na maelewano ya ushuhuda wa kuthibitisha haki ya kweli na katika kutoa huduma kwa kuwasadia walio wadhaifu zaidi kwa njia ya kutoa jibu la dhati linalostahili.

Suala la uekumene ndiyo njia mwafaka ya undugu

Kumekuwapo na mchakato mzima katika kutafuta umoja na mshikamano wa Wakristo ambao kwa dhati ndiyo zana msingi katika kutangaza na kushuhudia Injili ya Kristo ambaye aliteswa, akafa na kufufukwa kwa ajili ya wote. Kwa maana hiyo kukuza njia ya uekumene ni katika kutoa huduma na mshikamano wa upendo. Na njia mwafaka ambayo Baba Mtakatifu Francisko na mapapa waliotangulia imekuwa ni mkazo kuhusu  majadiliano ya kiekumene kama chemchemi ya matumaini ya umoja wa Wakristo na ambao wako mbioni katika mwelekeo huo wa makanisa yote ambayo yanaombwa kwa ari na mali kujikita katika umoja wa imani unaofafanuliwa hawali ya yote na Sheria, kanuni za Kanisa pamoja na taalimungu.

Katika mwendelezo huo wa Wiki ya  kuombea Umoja, ni wazi ya kwamba kuna haja ya kukuza na kudumisha uekumene wa mshikamano, ili kujenga na kuimarisha utamaduni wa mshikamano katika masuala ya uchumi, utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote; katika maendeleo ya sayansi na teknolojia na hata katika masuala ya kijamii na kisiasa kama maelezo pia kamili yanavyosisitiza kutoka Baraza la Kipapa la uhamasishji wa Umoja wa Wakristo, wakiangazia  Wiki hii ambayo imeandaliwa nchini Indonesia.

Amani ya kweli inatokana na upendo wa dhati na siyo manufaa binafsi

Amani ya kweli haiwezi kupatikana kwa njia ya mtutu wa bunduki, bali kwa njia ya upendo ambao kamwe hautafuti manufaa binafsi na kwa kufanya hivyo, Wiki ya kuombea umoja wa wakristo inawezakana kabia kuwa chumvi ya mchakato wa hija ya kiekumene kuufikia ule umoja wa Kanisa na watu wote ambapo sura ya 17 ya Injili ya Yohane inaoesha wazi sehemu ya kina kirefu na siri za Utatu Mtakatifu  ambapo Mwana anamkaribia  Baba yake na kusali kwa unyenyekevu na kumtukuza Baba, wakati huo huo Yesu anaomba kwamba wote walio wake waweze kuunda mwili mmoja, kuwa moja, kama Baba na Mwana walivyo na umoja. Kwenye Dunia, kuna Kanisa moja tu, ambalo Yesu Kristo amejitayarisha kama bibi arusi wake. Mgawanyiko wote kati ya Wakristo unasababishwa na watu wenyewe na dhambi ndiyo sababu yake. Kwa maana hiyo ahadi kweli ya Kristo itatimia tu kuwa: “wote wawe wamoja ( Yh 17,21).

18 January 2019, 14:32