Vatican ina uhusiano wa kidiplomasia na nchi 183 duniani. Vatican ina uhusiano wa kidiplomasia na nchi 183 duniani. 

Vatican ina uhusiano wa kidiplomasia na nchi 183 duniani!

Vatican ina uhusiano wa kidiplomasia na nchi 183 duniani. Mabalozi wakazi wanaoishi mjini Roma kwa sasa ni 89, wengine, ni mabalozi wanaowakilisha nchi zao wakiwa wanatoka nje ya Roma. Kuna Mashirika ya Kimataifa kama vile, Shirikisho la Nchi za Kiarabu pamoja na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Takwimu zinaonesha kwamba, Vatican ina uhusiano wa kidiplomasia na nchi 183 duniani. Mabalozi wakazi wanaoishi mjini Roma kwa sasa ni 89, wengine, ni mabalozi wanaowakilisha nchi zao wakiwa wanatoka nje ya Roma. Kuna Mashirika ya Kimataifa kama vile, Shirikisho la Nchi za Kiarabu pamoja na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR. Tarehe 26 Juni 2018, Vatican na nchi ya San Marino wameridhia kwa pamoja mkataba wa ushirikiano na Kanisa ili kutoa fursa ya kufundisha dini shuleni. Tarehe 23 Agosti 2018 Vatican na Benin zimeridhia mkataba wa ushirikiano kati ya Serikali na Kanisa na kwamba, kwa sasa Serikali ya Benin inalitambua Kanisa kisheria!

Tarehe 22 Septemba, 2018 Vatican na China vimetiliana sahihi mkataba wa muda unaotoa fursa na uwezo kwa Kanisa kuteuwa Maaskofu mahalia. Kwa mara ya kwanza, Baba Mtakatifu Francisko anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwawezesha Maaskofu wote nchini China kuwa na umoja na Khalifa wa Mtakatifu Petro, tayari kusonga mbele kwa ari na moyo mkuu katika mchakato wa uinjilishaji wa familia ya Mungu nchini China.

Tarehe 16 Julai 2018, Vatican iliridhia Mkataba na  Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO kuhusu umuhimu wa utamaduni kama chombo cha kujenga na kudumisha amani na maridhiano kati ya watu, hasa mwaka huu, 2019 UNESCO inapoadhimisha kumbu kumbu ya Miaka 70 tangu kuanzishwa kwake. Ushirikiano huu unapania kujenga na kudumisha haki msingi za binadamu, demokrasia na utawala wa sheria Barani Ulaya. Itakumbukwa kwamba, tarehe 21 Machi 2018 Vatican imeridhia mkataba wa kufundisha elimu ya juu Barani Asia na kwenye Visiwa vya Pacific. Na hatimaye, tarehe 30 Novemba 2018Vatican pia imejiunga na malipo ya huduma kwa kutumia Euro, maarufu kama (SEPA).

 

08 January 2019, 09:01