Tafuta

Vatican News
Masuala ya kimaadili na umarufuku wa kuondoa kizazi Masuala ya kimaadili na umarufuku wa kuondoa kizazi  

Vatican:Marufuku kuondoa kizazi makusudi!

Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, wameandika barua kwa mara nyingine tena kuthibitisha baadhi ya kesi ambazo kwa mantiki ya kimaadili ni marufuku kuondoa kizazi(total abdominal hysterectomy) kama si kwa mujibu wa uthibitisho wa madaktari juu kizazi chenye matatizo hadi kufikia kuharibu hata kiumbe kingine

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, wameandika barua kwa mara nyingine tena, itiliyotiwa saini tarehe 10 Desemba 2018 na Rais wake Kardinali Luis F. Ladaria, S.I. na Askofu Mkuu Giacomo Morandi,Katibu wa Baraza hilo ili kuthibitisha jibu kamili la  mashaka juu baadhi ya kesi ambazo ni marufuku kuondoa kizazi.

Uthibitisho wa barua ta tarehe 31 Julai 1993

Barua hiyo inasema, tarehe 31 Julai 1993, Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, lilitangaza jibu kuhusu mashaka yaliyokuwa yapo kuhusiana na  baadhi ya kesi kama vile ya kuondoa kizazi na masuala mengine. Katika majibu hayo na ambayo hadi leo hii yanahifadhi thamani yake,na ado yanafikiriwa kuwa muhimu kimaadili hasa wa kuondolewa kwa kizazi iwapo tu, kizazi hicho kinaharatisha maisha  au afya ya mama na kwa kuzingatia kuwa ni marufuku kufanya hivyo iwapo suala hilo linatumika moja kwa moja kuondoa kuzazi au kufunga mirija ya kizazi kwa sababu ya kuzuia mama asishike mimba.

Katika miaka ya hivi karibuni barua inasema, Vatican, imeweza kutafakari juu ya baadhi ya kesi hizo zinazotazama suala la utoaji kizazi hasa kwenda kinyume na malengo yake yaliyokuwa yamethibitishwa kunako1993, kwa maana hiyo inatazama hali halisi  ya kazi ya uumbaji. Mashaka na jibu linalosindikizwa na waraka huu uliotolewa na ambao unatangazwa kwa upya ni kutaka kutoa msisitizo wa kuzingatia kwa upya utimilifu wa majibu yaliyotolewa  kunako mwaka 1993.

Waraka wa Baraza la Kipapa umeonesha swali lililokuwa limetolewa

Mashaka: Je iwapo tumbo la uzazi liko katika  hali ya kutoweza kufanya kazi yake ipaswavyo na wataalam bingwa wamefikia hatua ya mwisho kwa  uhakika kwamba kizazi hicho kinaweza kuleta matatizo ya mimba kutoka kabla ya wakati, ni ruhusa kutolewa kizazi (hysterectomy)?

Jibu:Ni ndiyo kwani siyo sababu ya kufanya utasa

Mashaka yalikuwa kwa baadhi ya kesi kuu zilizokuwa zimetolewa katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, ambayo yalikuwa  yanakwenda kinyume na majibu hasi yaliyokuwa yametolewa tarehe 31 Julia 1993. Suala msingi ambalo linatoa utofauti na uhakika na madaktari bingwa ambao ndiyo wanathiobitisha kuwa, kizazi kinaweza kuharibu mtoto kabla ya kuzaliwa. Kutokana na hiyo haina matatizo na wala hatari kubwa au ndogo, japokuwa hatari ipo iwapo familia inafanya jambo hilo kwa makusudi mazima na misingi wa kutokutaka kuwa na watoto.  

Suala la kufanya utasa ni marufuku Barua inathibitisha na  hasa kwa viungo vinavyofanya  kazi ya uzazi, na  ni ubaya wa kumfanya mtu tasa kama njia ya kukataa maisha. Hilo ni tendo baya dhidi ya kukataa maisha wanathibitisha (bonum prolis). Katika kesi iliyochukuliwa maanani inatambuliwa kuwa viungo vilivyodhurika na havina uwezo wa kuhifadhi hadi kufikia kuzaa mtoto, kwa maana ya kufikia uaasili wake wa kuzaa. Lengo la mchakato wa uzazi ni kuweka dunia kiumbe, lakini katika suala hili, kiini hai hakiwezekani. Na ni kwa maana ya kujikuta mbele suala ya  la kiungo kutofanya kazi au hatari ya viungo kutofanya kazi.

Uhakika wa madaktari mbingwa

Jibu la utaalamu wa madaktari hauwezi kuhesabika kama ni wa kuthibiti uzazi kwa sababu  hiyo ni mantiki ambayo hakuna uwezo wa kiungo hicho kufanya kazi na matokeo yake inakuwa ni tendo la kuharibu. Kuondoa kizazi chote chenye uvimbe uliokaa vibaya( Fibroid) ambacho hakina uwezo wa kuzaa,(Total abdominal hysterectomy) kinaweza kusababisha utasa wa moja kwa moja, hivyo ni  marufuku iwapo tendo hili litafanyika kinyume na yaliyotajwa.

Aidha, jibu la kuwa na mashaka haimaanishi kwamba uamuzi wa kuondoa kizazi huwa ni bora zaidi, lakini ifanyike tu  chini ya masharti yaliyotajwa hapo juu, kwa maana ni uamuzi wa kisheria, lakini mbali na hiyo kuna uchaguzi mwingine (kwa mfano, kukimbilia katika kipindi kisicho cha kupata mimba au kujizuia kwa jumla). Hata hivyo hiyo inahusu uamuzi wa wanandoa kufanya  majadiliano na madaktari na mwongozo wao wa kiroho, au kuchagua njia ya kufuata, kwa kutumia vigezo vya kawaida vya kupima, hasa inapobidi kuingilia pia matibabu kwa kesi yao na mazingira yao. Baba Mtakatifu Francisko katika mkutano wa awali alimsikiliza Rais wa Baraza la Kipapa la Mfundisho ya Tanzu ya Kanisa na kuridhia jibu lililotajwa hapo awali na aliamuru kuchapishwa kwake.

03 January 2019, 16:11