Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu amenteua Askofu Mpya wa Jimbo katoliki la  Torit Sudan Kusini Baba Mtakatifu amenteua Askofu Mpya wa Jimbo katoliki la Torit Sudan Kusini 

Sudan Kusini:Mhs.Padre S.Martin Mulla ni Askofu Mteule wa Torit

Tarehe 3 Januari 2019 Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Stephen Ameyu Martin Mulla, kuwa Askofu wa jimbo Katoliki la Torit, Sudan Kusini

Tarehe 3 Januari 2019, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Stephen Ameyu Martin Mulla, kuwa Askofu wa jimbo Katoliki la Torit, Sudan ya Kusini. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Mteule Mulla alikuwa ni Profesa na Decano wa Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo huko Juba.

Askofu mteule Padre Stephen Ameyu Martin Mulla, alizaliwa huko Alodu Jimbo Katoliki la Torit, Sudan Kusini kunako tarehe 10 Januari 1964. Alijiunga na Seminari ndogo ya Torit, kati ya (1978- 1981) na baadaye akaendelea na seminari ya Wau, tangu 1981- 1983.

Aliendelea na Seminari Kuu ya Kitaifa ya Mtakatifu Paulo na Falsafa huko Bussere Wau 1984-1987. Taalimungu Munuki (Juba) tangu 1988-1991). Alipewa daraja Takatifu la Upadre, tarehe 21 Aprili 1991 katika Jimbo katoliki  la Torit Sudan ya Kusini. Baada ya upadrisho alishika nafasi mbalimbali katika jimbo lake kwa ajili ya watu wa Mungu hadi kufikia uteuzi wa kuwa Askofu wa jimbo la Torit Sudan Kusini.

03 January 2019, 16:18