Tafuta

Kardinali  Pietro Parolin Kardinali Pietro Parolin 

Kard.Parolin:Vijana jitahidi kubadili dunia!

Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican amesisitizia wito wa Papa kuwa, vijana lazima wajikite katika maisha ya kweli ya kisiasa na ambayo ni katika kutoa huduma kwa jumuiya nzima. Amethibitisha hayo katika mahojiano na Vatican News, siku chache kabla ya safari ya Baba Mtakatifu Francisko kuelekea katika Siku ya Vijana Panama

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Wito kwa vijana ili waweze kujikita kwa dhati katika maisha ya kweli ya kisiasa na ambayo ni huduma kwa jumuiya pia kuhangaikia wema wa pamoja ndiyo msisitizo ulitolewa na Kardinali Pietro ParoliN Karibu wa Vatican katika mahojiano na mwandishi wa Vatican News, Massimiliano Manichetti kabla ya safari ya Baba Mtakatifu Francisko huko Panama katika Siku ya Vijana Duniani. Karidinali akijibu swali kuhusu Roho ya Baba Mtakatifu Francisko katika Siku ya Vijana kwa mara ya tatu akiunganisha na Sinodi ya vijana iliyopita, mahali ambapo alisema ni kutembea kwa pamoja, Kardinali Parolin anasema, siku ya vijana duniani inayofanyika Panama inaadhimishwa mara baada ya Sinodi ya Maaskofu mwezi Oktoba uliopita, kwa maana hiyo roho ya Papa iliyomwongoza katika Sinodi hiyo, ndiyo pia itamwongoza Baba Mtakatifu wakati anajiandaa kufunga mkanda kukutana na vijana kwa kwa siku mbili za mwisho. Ni roho ya furaha kubwa anasisitiza!

Kardinali Parolini anasisitiza pia kuwa hiyo ni kutokana na kwamba katika Siku za Sinodi mjini Vatican, waliishi kipindi cha shauku ya kweli na kubwa na kusaidiana na vijana washiriki hivyo roho hiyo inataangaza kukutana na washiriki wote wa Siku ya vijana Panama. Kadhalika Kardinali Parolin anaamini  roho hiyo itatimilizika hasa katika baadhi ya maelekezo nyeti, kwa maana awali ya yote vijana ni sehemu ya Kanisa na ndiyo uthibitisho msingi ulitolewa na Sinodi. Vijana siyo wasikilizaji wa nje, bali ni wajumbe  waliojaa na kubeba jina kamili la Kanisa, ambao wanaishi maisha na kushiriki utume wake.

Mbele ya Kanisa na hali zake, lazima liweze kuongeza juhudi mara dufu. Jitihada zinazojikita katika mambo ambayo tayari yapo kwenye Hati ya mwisho ambayo ni ndefu na nzito, lakini ambayo kwa ufupi inaweza kutafsiriwa kwa maneno ambayo ni kusikiliza na kusindikiza. Kusikiliza ina maana ya kusikilizana  pamoja katika Kanisa au sehemu mbalimbali za Kanisa. Ni lazima kusikiliza Kanisa na shauku za vijana, mawazo yao, kwa upande mwingine  hata vijana wanaalikwa kusikiliza Kanisa ambalo kwa wakati huo linawasindikiza. Kusikiliza na kusindikiza vyote viwili vinatafisiriwa kama mapendekezo msingi wa Kanisa ambao ni wa kukutana na  Bwana Yesu na kufundishwa naye.

Katika ujumbe kwa njia ya Video ambao Baba Mtakatifu Francisko anasema kwa wanapanama na kuwakumbusha Ndiyo ya Maria, kwa maana nyingine anasema Kardinali Parolin, ndiyo mada kuu ya Siku ya vijana ambapo  anawashauri vijana wawe na utambuzi wa nguvu zao zinazoweza kuibadili dunia. Kardinali  anaamini kwamba, wote wanataka kubaidili dunia na hakuna yoyote hasiye tamani kuona dunia iliyo bora. Lakini inabidi kutazama kwa jinsi gani ya kuibadili dunia. Kutazama Bikira Maria, maana yake ni kuitikia mwitikio wake wa Tazama Mimi hapa, baada ya pendekezo la Bwana, ndiyo inakuwa mwelekeo wa dhati na wa mtindo, kama msingi wa kujiweka tayari katika usikivu wa kina wa mapenzi ya Mungu aliyofanya ndani ya maisha ya Maria. Kujiweka tayari katika utashi huo, kwa kutambua kuwa si kwa kulazimishwa kwa nguvu, mabavu na  ghasia na utafikiri ni tamasha la kubadili dunia, badala yake dunia inaweza kubadilishwa siku hadi siku katika mipango ya Mungu kupitia historia ya watu ambao daima imejaa  na mipango yake ya furaha na wokovu. Kwa maana hiyo kutazama Maria ni kukubali kufanya kama yeye na kubadili dunia kama yeye alivyoibadili  kwa njia ya kumzaa Yesu.

Katika mkutano huu wa imani huko Panama kutakuwa na vijana  wa asili  elfu moja kwa mara ya kwanza kushiriki siku ya vijana duniani. Baba Mtakatifu akiwakatika  ziara yake ya kitume huko Mexico aliomba msamaha kwa watu hao wa asilia na kwamba si kuwatazama kwa sintofahamu, au dharau, kama anavyoita tabia hiyo kuwa ni  utamaduni wa ubaguzi.Je Baba Mtakatifu Francisko atasema nini kwa vijana na katika dunia? Kardinali Parolin anathibitisha kuwa hii ni hali halisi ambayo  watu wa utamaduni wa asilia  wameteseka katika mchakato wa kihistoria hasa kwa kudharauliwa kutokana na wale amabo wamekuwa wakijina ni wenye utamaduni wa hali ya juu, lakini ambao leo hii wanasetesema na utamaduni wa ubaguzi, na ambao Baba Mtakatifu anazidi kutoa wito kila mara akisema kuwa huo ni moja ya mabaya mengi katika kipindi cha nyakati zetu.

Kadhalika Kardinali Parolin anaamini kwamba  ujumbe utakuwa ni ule ule wa watu waweze kuthamanisha tamaduni hizi. Tamaduni  ambazo kwa hali halisi zinaweza kupokea,  lakini pia hata kuweza kuchangia mambo msingi. Vijana wa tamaduni asilia wanaweza kutoa mchango msingi wa maendeleo na na uendelevu wa dunia yetu. Yeye binafsi amefanya uzoefu katika nchi  hizi mahali ambapo kuna tamaduni za asilia enzi za utume wa nchi za nje Kama Balozi wa Vatican nchi za nje na kwa maana hiyo anataka kuwahakikishia vijana wasiwe na aibu kuonesha jinsi walivyo, badala yake wajivunie kwa sababu wanaweza kupeleka mchango mkubwa na wa maana ya maisha yanayojikita katika uhusiano. Wasihangaikie kutaka kuwa nacho, badala yake ya kuwa na msimamo wa mahusiano. Kuwa na mahusiano anasema, ndiyo nguvu zao za kina na kusimika mizizi katika mitindo ya kileo, lakini wabakie  na thamani zao asilia.

Kijiografia, Siku ya vijana inafanyika mahali ambapo kuna matatizo ya kijamii, kiuchumi, kisiasa, uhamiaji wa kulazimisha ghasia na biashara haramu. Vijana kwa kutazama mfuasi wa Mtume Petro kwa matumaini, ujumbe wa Kanisa unaweza kuwarudishia imani kwa upya? Kardinali anaamini kwamba, wote tunayo mahitaji ya imani na matumaini leo hii. Kuna haja ya kutafuta suluhisho la dhati, katika uwezo wa kupanga, kufikiria katika dunia tofauti, katika dunia iliyo bora, mahali ambapo kuna uwezekano wa kuheshimu na kuthamanisha hadhi na haki ya kila mmoja. Kutokana na vigezo hivyo Baba Mtakatifu awali yote kama afanyavyo katika mikutano yake na vijana, atatoa ujumbe wake  kuwa: “msikate tamaa, endelea mbele; mnatambua ya kuwa mnaweza kufanya lolote, mnaweza kujihusisha na historia na mambo yake” na mbele ya mabaya mengi wanayofanya uzoefu, kardinali amethibtisha.

Na hatimaye Kardinali Parolin amependelea kurudia  kutoa ujumbe wa Baba Mtakatifu wakati kwa Siku ya amani duniani, ambapo alisema kuwa: “tambueni kwamba siasa, zaidi ya ujitolea kwa vijana wengine ambao wanajikita katika juhudi hizo  ni kambi ambayo mnaweza kujikita na kuibadili dunia”. Kwa hakika Baba Mtakatifu katika ujumbe wake juu ya siasa ana maana ya kwamba siasa ni huduma katika jumuiya, jamii  na ambayo inajikita kwa ajili ya wema wa pamoja na kila mmoja. Ktukana na hayo ni kujikita katika mantiki hiyo ambayo inaweza kuwa dhana msingi yenye thamani ya kufanya kazi ili kuboresha dunia hii.

KUBORESHA DUNIA
21 January 2019, 10:34