Vatican News
Ilikuwa tarehe 22 April 1984 mara baada ya kufunga Mlango wa Jubilei ya Wokovu, Mtakatifu Yohane Paulo II aliwakabidhi Msalaba wa vijana ishara ya upendo wa Yesu Ilikuwa tarehe 22 April 1984 mara baada ya kufunga Mlango wa Jubilei ya Wokovu, Mtakatifu Yohane Paulo II aliwakabidhi Msalaba wa vijana ishara ya upendo wa Yesu 

Siku ya Vijana ilianzishwa na Mt.Yohane Paulo II na kuwakabidhi msalaba!

Historia ya Siku ya Vijana duniani, inakwenda sambamba na Hija ya Msalaba. Msalaba mkubwa ulipendekezwa na Mtakatifu Yohane Paulo II wakati wa Jubilei ya Mwaka Mtakatifu wa Wokovu 1984 ambapo mara baada ya kufunga Mlango wa Jubilei aliwakabidhi vijana msalaba huo kama ishara na kielelezo cha upendo wa Yesu

Sr. Angela Rwezaula –Vatican

Kwa kutazama siku ya vijana duniani inayokaribia kuanza tarehe 22 -27 Januari 2019 huko Panama 2019, vijana wengi wameshafika na wengine wako njiani kuelekea katika siku hii maalum, ambayo inaunganisha vijana wa makabila yote duniani kote kuadhimisha kwa pamoja uzuri wa kuwa mwanadamu na kushuhudia imani yako inayokupatia uhuru. Mwaka huu vijana wote wataongozwa na sura ya Mama Maria kijana kama wao, mpalestina ambaye aliweza kuitikia wito wa ndiyo kwa Bwana mara baada ya kuitwa kwake katika utume waka maalum ambao ulileta ukombozi hapa duniani. Lakini siku hiyo ya vijana chimbuko lake ilinzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II, na wakati huo huo akawakabidhi Msalaba, ambao unaongozana na vijana hao katika kila maadhimisho yote ya Siku ya vijana duniani. Wakati wa kuanzisha siku hiyo, Mtakatifu Yohane Paulo II alisema, “vijana wapendwa, wakati wa kuhitimisha mwaka Mtakatifu  ninawakabidhi ninyi ishara ya upendo wa Bwana Yesu kwa ajili ya binadamu ili kuwatangazia watu wote kuwa ni kwa njia ya Yesu tu aliyekufa na kufufuka wanaweza kuwa na wokovu”.

Msalaba unakabidhiwa vijana

Mtakatifu Yohane Paulo II alitamka maneno hayo tarehe 22 Aprili 1984, katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, mara baada ya kufunga Mlango Mtakatifu wa Jubileo ya Wokovu. Msalaba mkubwa wa mti wenye urefu wa mita 3,8 ulikuwa umewakwa kushoto mwa altare,mara baada ya kuwa mwanga wa imani kwa mwaka mzima na kukabidhiwa katika mikono ya mahujaji wa dunia, ambapo Mtakatifu Yphane Paulo II alisema kuwa,”itakuwa ni tangazo na mkutano, utakaogeuka kuwa msalaba wa Siku ya Vijana”.

Msalaba wa Mwaka Mtakatifu uliondolewa na kupeleke katika Kituo cha Mtakatifu Lorenzo,kituo kilichoanzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II amabo tangia wakati huo Msalaba huo hutumzwa hapo mara baada ya mzunguko wake. Kwa mara ya kwanza msalaba huo ulitua katika nchi ya Ujerumani.

Vijana 300,000 na Baba Mtakatifu

Tangu tarehe 31 Machi 1985 katika Dominika ya Matawi, msalaba huo unakatisha katika mabara matano kuanzia Uwanja wa Mtakatifu Petro ukiwa umezungukwa na umati wa vijana karibia 300.000 na msalaba wa Mwaka Mtakatifu kwa dhati umeleta mkusanyiko mkubwa wa vijana hata katika fursa ya Mwaka wa kimataifa wa vijana uliotangaza na Umoja wa Mataifa ambapo Mtakatifu Paulo II aliweweze kushuhudia

Kuanzishwa rasmi na siku mbili za vijana (kijimbo na kimataifa)

Mwezi Desemba mwaka huo wakati wa Mtakatifu Yohane Paulo II akiwatakia heri na baraka za Noeli Kuria nzima ya Vatican alithibitisha kuwa: “bado machoni pangu ninao mtazamo  na sura ya mkutano mkubwa wa vijana wa rangi zote kutokana pande zote. Hii si kusema kuwa  ni wimbi lisilo na jina wala idadi, lakini ni uwepo hai wa watu ambao walishiriki kwa dhati furaha ya kushangaa na iliyowekwa katika matendo ya umoja wa upendo na imani kwa Kristo Bwana”. “Hii itakuwa ni Siku ya Vijana duniani, ambayo itaadhimishwa Dominika ya Matawi kwa maandalizi na ushirikiano wa Baraza la Kipapa la Walei”. Kutona na hiyo ndipo ikazaliwa Siku mbili za Vijana duniani, ambazo zinaadhimishwa kila mwaka kwa ngazi ya kijimbo na kwa muda wa miaka 2 au 3 katika sehemu mbalimbali za dunia kwa mantiki ya Mkutano wa Vijana duniani na Papa.

 

 

18 January 2019, 16:00