Tafuta

Vatican News
Zaidi wa waathirika 20 wamekufa nchini Colombia kufuatia na shambulizi la kigaidi karibu na chuo cha Polisi Zaidi wa waathirika 20 wamekufa nchini Colombia kufuatia na shambulizi la kigaidi karibu na chuo cha Polisi 

Papa Francisko atuma salam za rambi rambi nchini Colombia!

Ni masikitiko ya kina ambayo yameelezwa na Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake wa rambi rambi kwa zaidi ya waathirika 20 wa shambulizi la kigaidi mjini Bogota nchini Colombia, Alhamis tarehe 17 Januari 2019

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa masikitiko makubwa juu ya taarifa ya mashabulizi ya kigaidi yalitokea tarehe 17 Januari 2019 huko Bogota nchini Colombia. Katika ujumbe wake ulioandikwa na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican kwa niaba yake na kumtumia Askofu Mkuu wa Bogota Rubén Salazar Gòmez, anaeleze masikitiko makubwa hasa ya ukatili wa namna hiyo usiyo wa kibinadamu ambao umesababisha uchungu na vifo.Katika shambulizi lililotegwa bomu dhidi ya Shule ya Kitaifa ya Polisi wamekufa watu zaidi ya 20 na zaidi ya watu 68 wamebaki wamejeruhiwa.

Baba Mtakatifu Francisko anawaombea wale wote walioathirika na shambulizi hili na kupoteza maisha yao katika tendo hili lisilo la kibinadamu. Na anaonesha ukaribu wake kwa wote waliojeruhiwa, familia na jamii nzima ya Colombia. Anashutumu vikali  ghasia hizi kipofu na ambazo zinadhuru vibaya viumbe. Anasali kwa Mungu ili kuweza kuendelea katika ujenga maelewano na amani katika nchi na duniani kote. Na mwisho anawatumia baraka wa waathirika wote, familia na nchi nzima ya Colombia.

Taarifa  zaidi kufuatia na shambulizi la kigaidi ni kwamba limetokea siku ya Alhamis tarehe 17 ambapo walengwa wake walikuwa  ni maafisa wa usalama na wanafunzi katika kitengo cha Polisi waliokuwa wakipewa shahada. Katika shambulizi hilo la bomu watu zaidi ya 20 wamefariki na wengine 68 kubaki wamejeruhiwa. Nchi mbalimbali zinaendelea kutuma salama za rambi rambi kwa serikali ya Colombia na familia za wahanga waliofariki katika shambulizi hilo. Shambulizi hilo litekelezwa na watu walio lipua bomu lililokuwa ndani ya gari lililokuwa limetegezwa karibu na shule moja ya Polisi mjini Bogota.

 

 

 

18 January 2019, 16:06