Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko akiwa na Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa kikristo Baba Mtakatifu Francisko akiwa na Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa kikristo 

Kard.Koch:Damu ya wafidini haigawi,inaunganisha wakristo wote!

Vatican News imefanya mahojiano ya Kardinali Kurt Koch Rais wa Baraza la Kipapa la kuhamasisha umoja wa kikristo katika fursa ya kuanza Wiki ya Kuombea Umoja wa Wakristo ambapo anasema uekuemene siyo uchaguzi bali ni ulazima kwa wakristo kutafuta umoja kwa njia ya kusali

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mahojiano na Vatican News na Kardinali Kurt Koch Rais wa Baraza la Kipapa la kuhamasisha umoja wa Kikristo katika fursa ya kuanza Wiki ya Kuombea Umoja wa Wakristo anasema, uekumene siyo suala la uchaguzi au kupendelea, bali ni ulazima kwa wakristo. Historia nzima imewagusa wengi katika majeraha, migawanyiko na mipasuko, lakini leo hii ni lazima kutafuta umoja hasa kwa njia ya kusali.

Wiki ya Kuombea Umoja wa wakristo ilianzishwa 1908

Kardinali Koch anasisitizia umuhimu wa Wiki ya Maombi kwa ajili ya umoja wa Wakristo ambayo imeongozwa na mada ya kutafuta kuwa wenye haki, ambayo imetolewa katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati 16,18-20 na kwa maana hiyo Kardinali katika mahojiano yake anasema, Baba Mtakatifu atashiriki masifu ya jioni saa 11.30 masaa ya Ulaya katika Kanisa kuu la Mtakatifu Paulo Roma. Kiutamaduni, Baba Mtakatifu hufunga siku hiyo kwa maadhimisho hayo siku ya mwisho, lakini kwa mwaka huu, tarehe hiyo, Baba Mtakatifu atakuwa katika Siku ya Vijana Duniani. Wiki ya Maombi inayoanza tarehe 18-25 Januari kwa kawaida inahitimishwa katika Siku Kuu ya uongofu wa Mtakatifu Paulo. Siku hiyo ilianzishwa kunako mwaka 1908 na Mchungaji Paul Wattson Graymoor (New York) Marekani, kama Siku ya Nane ya Maombi kwa ajili ya umoja akiwataka wote waweze kujikita katika matendo ya dhati ya umoja.

Aidha Kardinali Koch ameelezea juu ya Wiki ya Kuombea umoja wa wakristo ambayo imeandaliwa na wakristo wa Indonesia ambayo wanawakilishwa na idadi ndogo sana na yenye kuwa na ugumu wa safari lakini inayohitaji uvumilivu wa kuweze kufikia upeo. Hata hivyo pia anakumbusha kuwa kwa mfano mwaka huu wanaadhimisha miaka 20 tangu kutaagaza mafundisho ya pamoja juu ya haki, iliyotiwa sahini na Shirikisho la Kiluteri duniani na ambapo pia wameongezeka ushirikisho wa Wametodisti, Mageuzi na Waanglikani. Pamoja na Makanisa ya Kiorthodox anaongeza kusema Kardinali Koch kuwa, wote tuko katika mwendo kwa mantiki kidogo mgumu wa mahusiano kati ya ukuu na upamoja.

Moyo uliofunguka kwa ajili ya uekemene

Akiendelea na ufafanuzi wake kwenye mahojiano, Kardinali Kurt Koch anakumbusha kuwa baada ya Mtaguso wa Vatican II,  mababa watakatifu wote, wamekuwa na moyo ulio wazi wa kiekumene. Na Baba Mtakatifu Francisko hata leo hii anazidi kuelezea juu ya mantiki mbili. Ya kwanza inaelezea juu ya ukuu wa utatu kwa kukumbusha kuwa Papa anaomba daima kutembea pamoja  kusali pamoja na kushirikana.

Mantiki ya pili ni uekumene wa damu, kwa sababu leo hii wakaristo wengi wanateseka zaidi kuliko hapo karne za kwanza, na asilimia 80 za watu wanauwawa kwa ajili ya kutetea imani yao. Wakristo hawateswi kwa sababu ni waluteri, waanglikani, wametodisti, wakatoliki, waorthodox, bali wanateswa kwa sababu wao ni wakristo. Damu ya wafidini wengi leo hii haigawanyi badala yake inaunganisha wakristo wote, amesisitiza Kardinali Kurt Koch.

 

18 January 2019, 15:30