Tafuta

Vatican News
Siku ya vijana Duniani huko PANAMA 2019 inakaribia Siku ya vijana Duniani huko PANAMA 2019 inakaribia  

Kard.Farrell:Siku ya Vijana 2019 ni mwendelezo wa kile kilichotukia katika Sinodi

Tukiwa tunakaribia Siku ya Vijana Duniani huko Panama Amerika ya Kusini, Kardinali Farrell Rais wa Baraza la Kipapa la Walei, familia na maisha anasema Siku ya Vijana 2019 ni mwendelezo wa kile kilichotukia katika Sinodi,kwa maana hiyo ni mwanzo wa mabadiliko ya Kanisa. Vijana wengi kuanzia Kaskazini, mashariki, magharibi na kusini wameanza kuelekea Panama

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika mahojiano ya Kardinali Kevin Farrell Rais wa Baraza la Kipapa la Walei, familia na maisha kuhusu Siku ya vijana huko Panama, kwenye  tovuti ya Baraza hilo , Kardinali anasisitizia juu ya mkutano wa kwanza kabla ya Sinodi, pia Sinodi ya vijana iliyofanyika mwezi Oktoba 2018 katika mtazamio wa Siku ya Vijana ijayo kwamba ni kama mwendelezo wa kile kilichotukia kwa dhati katika Sinodi ya Maaskofu kuhusu vijana. Siku ya vijana 2019 ni mwanzo wa mabadiliko ya Kanisa. Kardinali Farrell anathibitisha kwamba kama kuna mtu anayefikiria Siku ya vijana inaanza kuzeeka, labda aseme ni kutokana na kwamba kuna ulazima wa mabadiliko, lakini yote hayo ni sawa  na tukio ambalo tayari limejitokeza katika Sinodi ya vijana na sasa ni mwanzo mpya. Uzoefu wa Sinodi wa kubadilishana na ushirikishano kati ya vijana na maaskofu iliyopendelewa na kuhamasishwa kwa dhati Baba Mtakatifu Francisko, ni mabadiliko na ni kusikiliza hali halisi na siyo kile ambacho kiko akilini tu bali hata kile ambacho vijana wanakabiliana katika maisha yao.

Ni lazima kuwasikiliza vijana, hata kwa wote

Kardinali Farrell aidha anawaalika kusikiliza, lakini ni suala la  kusikiliza wote na kwa namna ya pekee vijana bila kuwalazimisha kwa namna tunavyotaka wao wawe. Kwa hakika ni lazima kuwaelekeza  katika mwelekeo na kuwaongoza katika mtindo wa kimaadili na kwa mifano zaidi lakinipia wao pia ni wenye mawazo  na wanatambua namna ya kuyafanyia kazi, wanatambua ni kipi ni kibaya na kizuri, ni kitu gani kinawavutia na kile ambacho hakiwavutii. La muhimu tunatakiwa kuwasikiliza na kujifunza. Kadhalika kwa mujibu wa Kardinali Farrell anasema, vijana wanajifunza kutoka katika Kanisa na wanaweza kuigwa katika mifano yao mingi, utambuzi na zaidi hata ujasiri, shauku na utashi wa kutaka kutoka nje na kufanya jambo lolote ambalo linawahusu kama asili  ya vijana ambao wanapenda kuthubutu pia changamoto. Tunaishi katika dunia iliyochoka , haiwasiliani tena badala yake vijana wanawasiliana mara kwa mara, wanaunda mawazo mapya; kwa dhati kuna ulazima wa kufanya mang’amuzi, lakini ikumbukwe kuwa ni vijana ambao wana nguvu, shauku na utashi wa kutaka kubadilisha.

Je mifano ipi wanaweza kujifunza kutoka kwa watu wa Amerika ya Kati?

Kardinali Farrell anaeleza kuwa watu wa Amerika ya kati ni watu wakuu na wenye ujasiri. Kwa kutaka kujua zaidi anatoa mfano wa kufikiria uhamiaji, ni njia ya kukuonesha kuwa vijana hawataki kushi tena kwa njaa na ghasia bali wanafuta na kupata maeneo yaliyo bora. Na wanapoweza kupata, wanajifunza na ni wenye uwezo wa kubadilisha maisha yao binafsi na hata ya jamii. Ni matarajio ya Kardinali Farell ya kwamba wote tunaweza kujifunza kutoka katika utashi wao na kwa pamoja maana ya imani ya kina ambayo inawafanya waishi wakiwa wameungana na Mungu. Hili ni jambo ambalo katika maeneno mengine ya dunia hawafanyi uzoefu wa namna hiyo.

Vijana ni suluhisho la mambo mengi yenye kipeo katika jamii

Kadhalika Kardinali Farrell anafikiri kwamba vijana ndiyo suluhisho la mambo mengi ya kipeo cha sasa duniani na anatambua kuwa Baba Mtakatifu Francisko atawahamasisha kuwa na shauku kubwa ya kushiriki katika maisha ya dini na zaidi kuyabadili. Akigusia juu ya mada inayoongoza Mkutano huko Panama: “ ndimi mtumishi wa Bwana, nitendewe ulivyonena”, Kardinali Farrell anaonesha sura ya Mama Maria kwamba ndiyo kiini cha Siku ya vijana duniani kwa maana  Mama Maria ni mmmoja kama  kijana mwanamke wa Kipalestina aliyepata ujasiri wa kubadili dunia. Hakuna mwingine aliyetokea kama yeye kwa sababu yeye aliweza kutamka kwa ujasiri na kukubali akisema “ Tazama mimi ”. Na Neno hilo ni  sawa na neno la Mungu ambalo anamwita kila kijana leo hii duniani, ili apate kuitikia tazama mimi.

Kama Maria, vijana ni kama suluhisho na wanalo jibu, maono na kwa njia zipi waweza kufanya ili dunia iweze kuwa  bora. Ujumbe wa vijana ambao wanatasikiliza huko Panama na  iwapo wataondoka ujumbe huo ndani ya mioyo yao  kuupeleka nyumbani kwao, watatakiwa watafsiri na kujikita katika matendo ya dhati  ili kuweza kubadili dunia. Siku ya vijana itaweza kusaidia watu wote katika kusikiliza Neno ili kuweza kutambua ni kitu gani tunaambiwa, kila wakati katika maisha yetu. Kwa mujibu wa Kardinali Farell anasema, kati ya dhambi zilizo kuu duniani ni ile ya kujibagua, ubinafsi, kutumia hovyo, mambo ambayo baadaye ndiyo chazo cha ukosefu wa kutunza mazingira na ubinafsi, kadhalika hata kukosa upendo kwa wengine. Sisi sote tunao ulazima wa kuheshimiana zaidi, kuwa na huruma zaid,i pia upendo zaidi. Sisi sote tuko katika dunia hii na kujiboresha wenyewe ni sawasawa na kuiboresha dunia hiyo kwa ajili ya wote!

Zaidi ya vijana 23,000 wa Ujerumani kuudhuria siku ya vijana 2019 Panama

Ni vijana 23,000 kutoka Ujerumani wataudhuria Siku ya vijana duniani huko Panama wakisindikizwa na maakofu wakuu watatu, maaskofu saba wasadizi na idadi kubwa ya wahusika wa jimbo. Ofisi ya Mawasiliano ya Baraza la Maaskofu Ujerumani imetoa taarifa kuwa kutakuwa na uwezakano wa kukutana na vyombo va habari na baadhi ya maaskofu wengine katika mkutano, tarehe 21 Januari 2019 huko Panama ili kuweza kujua ni kitu gani kinwasubiri mahujaji na maaskofu wa Ujerumani katika Siku hii ya Dunia kwa vijana ambayo inakaribia sasa.

Baraza la Maaskofu Uswis wawakilishwa na watu 160

Na kutoka Baraza la Maaskofu huko Uswis watawakilishwa na vijana 160 ambao  kuanzia tarehe 16 Januari 2019 watakuwa wenyeji  katika jimbo ya  Penonomé, kwenye kijiji cha volkeno ya El Valle de Antón. Watasindikizwa na  Askofu  Marian Eleganti, ambaye ametanguliwa huko Costa Rica, tangu tarehe 11 Januari 2019 na Askofu Alain de Raemy ambaye ni  Askofu wa vijana. Mara baada ya misa tarehe 14 Januari 2019 wameanza safari kuelekea Panama.

Washiriki 40 wa Siku ya vojana kutoka nchini Norway

Vijana 40 wakisindikiza na mapadre wanne kutoka  nchini Norway wameanza safari tarehe 15 Januari 2019 kuelekea Panama. Katika Video ya Jimbo la Oslo Iselin,waliyoitoa katika mtandao, kijana mmoja mshiriki wa Siku ya Vijana anasema kuwa: “sisi wakatoliki ni idadi ndogo nchini Norway, lakini  ni uzuri gani wa kuweza kusafiri ili kuona hali halisi ya ukubwa wa Kanisa. Ni kujifunza zaidi juu ya jumuiya katoliki na kutambua uwepo wa Mungu kati yao wakatoliki. Vijana hawa watapata mapokezi katika Jimbo la Puntarenas, huko San José, Mji Mkuu wa Costa Rica.

Danimark ni vijana  75 walioondoka kwenda Panama na askofu Kozon. Wameondoka na picha ya “Amen” 

Vijana 75 kutoka nchini Danmark pamoja na Askofu Czeslaw Kozon wa Copenaghen  na mhusika wa masuala ya kichungaji Padre Lasper Baadsgaard -Jensen wameanza safari tarehe 14 Januari kuelekea katika siku ya vijana Panama. Vijana hawa wamekwenda na zawadi moja waliyo iandaa katika miezi iliyopita chini ya uongozi wa Sr. Theresa Piekos, picha  fulani ilitengenezwa na vitu vidogovidogo vyenye rangi ikiwa ina maanisha ishara ya watu katika dunia hii na ishara ya jumuiya kubwa ya ulimwengu wa Kanisa na familia kubwa ya Mungu. Picha  picha hii waliyoitengeza wameipatia jina la “ Amen”, ikiwa na maana ya “ndiyo  ya Maria katika Mpango wa Mungu  na inaeelezea juu ya mfululizo wa ishara nyingi ambazo zinajikita kufafanua mafundisho ya Baba Mtakatifu Francisko juu ya Mama Maria.

Hata hivyo kikundi kidogo cha vijana walikuwa wamemkabidhi kopi ya picha Baba Mtakatifu mwezi Septemba mwaka jana na Baba Mtakatifu Francisko alikuwa amebariki mpango huo wa Uinjililishaji kwa ajili ya Siku ya Vijana duniani huko Panama.Picha hiyo imeweza kuchorwa katika masweta yao waliyo vaa vijana wakati huo huo, picha hiyo itakabidhiwa familia itakayowakaribisha vijana hao katika sehemu yao ya kwanza kabla ya kuunganika kwa pamoja. Kwa namna ya kusema picha hii itatoa ujumbe wa furaha ya Injili kwa familia zitakazo wakaribisha watu Panama. Picha hiyo pia imetengenezwa kadi ndogo ambazo vijana wataweza kuwazawadia vijana wenzao watakaokutana nao katika Siku ya vijana duniani.

Vijana 130  kutoka nchi za Kibaltiki wakiwa na  Maskofu wawili

Na katika nchi za  kibaltiki vijana na watu wazima 130 wakiwa na maskofu wawili wamefika tayari katika jimbo la Santiago de Veraguas, kilometa 250 kabla ya kufika Panama, ambao walianza safari tarehe 12 Januari 2019 ili kushiriki siku hii maalum kwa vijana. Kikundi cha watu 130 ni mchanganyiko wa vijana na watu wazima kutokana na kwamba kipindi hiki kwa vijana katika nchi hizo imekuwa vigumu kutokana  kuotkana na masomo shuleni. Hata hivyo haikukosekana miezi ya maandalizi waliyoongoza na mada:“jigundue utambulisho wako”, jiuliza juu ya swali kama vile wewe ni nani, unajihusisha vipi katika jamii, imani yako inatokana na nini.

Mpango wa maandilizi yao ulijikita katika vijana kufuata utashi wao hasa kwa namna ya pekee kutazama dunia ya taaluma kwa mfano katika sekta ya afya. Kwa wale wote ambao hawakuwa na bahati ya kwenda Panama, lakini wanataka kuona kile kinachoendelea, huduma ya kitaifa kwa upande wa kichungaji imependekeza kutumia njia hii yanani  kwenda katika kisiwa cha Homeland mwishoni mwa wiki tarehe 25- 27 Januari 2019 “wjd@home”  yaani (siku ya vijana nyumbani), ikiwa na maana ya kufuatilia katika mtandao.

15 January 2019, 09:07