Cerca

Vatican News
Siku kuu ya Mtakatifu Antonio  Abate kufanyika  mjini Vatican tarehe 17 Januari 2019 Siku kuu ya Mtakatifu Antonio Abate kufanyika mjini Vatican tarehe 17 Januari 2019 

Kard.Comastri:Maisha ya Mt.Antonio yana ukaribu na wakulima!

Kila tarehe 17 Januari ya kila mwaka Mama Kanisa anakumbuka siku ya Mtakatifu Antonio Abati msimamizi wa mifugo na baba wa wamonaki. Katika misa kwenye Kanisa la Mtakatifu Petro iliyoongozwa na Kardinali Angelo Comastri, amewahimiza wafugaji na wakulima kuiga mfano wa mtakatifu huyo, maana anaye mtegemea Mungu hana hofu kamwe

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 17 Januari siku ambayo Kanisa linaadhimisha kumbukumbu ya Mtakatifu Antonio Abati, msimamizi wa wanyama na baba wa wamonaki, imekuwa sasa utumaduni wa kuiita Siku ya wafugaji ambapo uandaliwa katika Uwanja wa Pio XII na Chama cha Cordiretti na Vyama vingine vya wafugaji nchini Italia(Aia).

Banda la wanyama chini ya anga la jua

Katika siku hiyo tukio lilianza saa 9.30 asubuhi massa ya Ulaya kwa kuandaa banda la mifugo, mahali ambapo waweleweza kuweka kila aina ya wanyana katika mabanda hayo kama vile ng’ombe, ngamia, nguruwe, kondoo, kuku, bata, na kila wanyama wa kufugwa na haya wale ambao ni nadra , lakini wanafugwa kwa ajili ya kuendeleza aina hiyo ya ndege au wanyama wasiweze kupotea. Kwa maana hiyo wawakilishi wa wafugaji kutoka nchini kote Italia walikuwapo mjini Roma. Wakati huo mwenyekiti wa vyama vya wakulima na wafugaji amemshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa utayari wake na umakini wa kulinda mazingira na wanyama, na zaidi kwa ajli ya  hivyo wosia wa Laudato Si. Amesema hayo akihojiana na Vatican News.

Mahubiri  katika misa kwenye Kanisa la Mtakatifu Petro

Saaa 5.00 masaa ya Ulaya Misa takatifu kwa ajili ya wafugaji katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, imeoongozwa na Kardinali Angelo Comastri Makamu wa Papa katika mji wa Vatican. Katika mahubiri yake amewasalimia watu wote na kuwashukuru wafungaji wote kutoka nchini Italia na kuwaonesha kuwa katika Altare waliweka sanamu ya Mtakatifu Antono Abati ambaye aliishi kati ya miaka1500. Na tangia wakati huo kila mwaka wanasali pamoja, familia nzima na maisha yanakuwa mema hasa kuwa  karibu na Mungu. Na hii i wazi kwamba iwapo familia au watu binafsi wanakaribia Mungu hawawezi kuogopa kitu.

Anayemkaribia Mungu hazeeki

Kardinali akizungumzia juu ya Mtakatifu Antonio Abati aliyeishi kati huko Misri miaka 1700, anasema wenzake wakuu ambao walijona ni  wenye nguvu  na ,tawala wa dunia nzima Deoclazio kwa sasa, amesahauliwa, lakini Mtakatifu Antonia Abati bado anakumbukwa na amebarikiwa kwa sababu alimkubatia Mungu na kujikita kuendelea kwa nyakati, kamwe hazeeki.

Mtakatifu Antonia alitambua kuwa Mungu ndiyo tajiri wa kweli wa maisha na alitambua kuwa Mungu alikuja kwetu kukutana nasi kwa njia ya Yesu ambaye kwa mkono wake ulionyooshwa anatuvuta kwake ili tuondokane na ukatili. Mara baada ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Kardinali Comastri na wawakilishi wa wafugaji na wakulima wote walielekea katika Uwanja wa Pio XXI kwa kuhitimisha kama utamaduni wa baraka kwa wanyama wote.

18 January 2019, 15:56