Tafuta

Vatican News
 Tarehe 21-24 Januari 2019 umefanyika Mkutano wa Taalimungu ulioandaliwa na Baraza la Maaskofu India kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa huko bangalore Tarehe 21-24 Januari 2019 umefanyika Mkutano wa Taalimungu ulioandaliwa na Baraza la Maaskofu India kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa huko bangalore 

India:Imani ya kikristo katika mantiki ya tamaduni nyingi!

Imani ya kikristo katika mantiki ya tamaduni nyingi ndiyo mada kuu iliyoongoza Mkutano wa Kitaalimungu,ulioandaliwa na Baraza la Maaskofu Katoliki nchini India kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, huko Bangalore tarehe 21-24 Januari 2019

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kuanzia tarehe 21-24 Januari 2019 katika Chuo Kikuu cha Madaktari cha Mtakatifu Yohane mjini Bangalore India, umefanyika Mkutano wa Kitaalimungu,ulioongozwa na mada:“imani ya kikristo katika mantiki ya tamaduni nyingi”.Mkutano huo uliandaliwa na Baraza la Maaskofu Katoliki nchini India kwa ushirikiano wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na kuwaona washiriki maaskofu 44 na Wataalimungu wa India. Wawakilishi wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, walikuwa ni Kardinali Luis F.Ladari S:I, Rais wa Baraza hilo, Askofu Mkuu J.Augustine Di Noua, O.P, Katibu Msaidizi wa Baraza hilo na baadhi ya washiriki maalum kutoka Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu.

Kadhalika Mkutano huo umeudhuriwa na Balozi wa Vatican nchini India, Askofu Mkuu Giambattista Diquattro. Kwa upande wa Baraza la Maaskofu wa India, washiriki kutoka Makanisa Matatu yanayowakilisha nchini humo yameongozwa na Kardinali Oswald Gracias, Rais wa Baraza la Maaskofu India, Kardinali Moran Mor Baselios Cleemis, Rais wa Sinodi Takatifu ya Kanisa la Siro-Malankarese, Kardinali Mar George Alencherry,Rais wa Sinodi Takatifu ya Kanisa la  Siro-Malabarese,na Askofu Mkuu Thomas Mar Koorilos, Rais wa Ofisi kwa ajili ya Mafundisho Tanzu ya Baraza la Maaskofu India. Aidha washiriki wengine wa mkutano huo ni maaskofu wakuu na maaskofu  18 wataalimungu 22, miongoni mwao wakiwa ni mapadre, watawa na walei ambao wanawakilisha Makanisa matatu kisheria  nchini humo.

Wazo ka mkutano huo lilipendekezwa 1996

Wazo la mkutano wa mwaka kati ya Maaskofu na Wataalimungu wa India lilipendekezwa kunako 1996. Baadaye wakati wa mkutano na wajumbe  wa Maaskofu wa India pamoja na wawakilishi mbalimbali kutoka Mabaraza ya Kipapa Roma, walishauriana uwepo ushiriki wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa katika Mkutano wa namna hii.  Kwa kukubali utashi huo, Baraza la Mafundisho Tanzu ya Kanisa ilishiriki mazungumzo ya Kitaalimungu na Maaskofu na Wataalimungu kwenye mkutano wa tarehe 16-22 Januari 2011.

Tangu kuanea kwa Injili nchi ya India ni hai katika shughuli za upendo, elimu na kijamii

Miaka nane baadaye, Mkutano huo umeandaliwa kwa upya kwa lengo la kukuza uelewa na udugu wa mshikamano. Katika Bara hili la India, kwa dhati upo mfano na mwendelezo wa amani kati ya watu ambao pamoja na tofauti nyingi zilizopo za lugha dini na utamaduni. Kwa sababu ya rasilimali kubwa za asili na ubinadamu, ni moja ya nchi zenye kuwa na ahadi duniani. Hiyo ni kwasababu walipokea Injili tangu  mwanzo wa ukristo,wakatoliki wa India wameweza kutoa mchango kwa namna hai ya maendeleo katika nchi hasa kwa njia ya taasisi za elimu, vituo vya afya na kuanzisha mambo mengi yenye chanzi asili cha kijamii na matendo ya upendo kwa ndugu.

Salam za Rais wa Baraza la maaskofu India na Rais wa Baraza la Kipapa la Mafundisho tanzu pia mada zilizochaguliwa kuongoza vipindi vitano kwa siku tatu

Mwanzo wa ufunguzi wa Mkutano huo, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini India amewakaribisha wote kuudhuria akisisitizia juu ya lengo la mkutano huo. Aidha Rais wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, ametoa mwelekezo kwa kuwataka waweze kuzungumza juu ya wito maalum wa taalimungu kwa ajili ya kuhamasisha imani katoliki. Kwa kuzingatia mantiki ya India, mada zilizochanguliwa katika vipindi vyote vitano vya Mkutano hui wamekabiliana na baadhi ya changamoto za kichungaji kwa Kanisa leo hii kwa mfano:maana ya wokovu wa kikristo katika dunia ya tamaduni nyingi; baadhi ya tafakari kuhusu Ujumbe wa Placuit Deo uliotolewa na Askofu Mkuu J. Augustine Di Noia, O.P.; Kutumwa na kujengwa juu ya mwamba, kuwa na chachu katika kuweka usawa kati ya zawadi za uongozi na karama katika zizi dogo la India  uliowakilishwa na Profesa Francis Gonsalves, S.I.; Changamoto za tamaduni nyingi nchini India zilizodadavuliwa na Askofu Thomas Dabre; na jibu kutoka kwa Askofu Barnabas Mar Jacob, O.I.C.;Uinjilishaji na ushirikiano wa dini zote  kutoka katika misingi ya Biblia na Baba wa Kanisa ulitolwa na Profesa Thomas Manjaly; na jibu kutoka kwa Profesa Sr. Metti Amirtham; Kuishi imani ya kikristo kwa mantiki ya dini nyingi na tamaduni nyingi ulitolwa na Askofu Mkuu Felix Machado.

Majadiliano hai kuhusu mada hizo

Uwakilishi wa mada hizo umefuatiwa na majadiliano hai, inayoelekeza kwa kina uelewa wa mada mbalimbaki kwa kuzingatia hali halisi maalum nchini India na changamoto ambazo Maaskofu na Wataalimungu wanapaswa kujibu. Kwa maana hiyo roho ya wazi ya mazungumzo, heshima na kubadilishana mawazo na uzoefu, viwaongoza kwa hakika katika majadiliana na hata kupongezana kwa juhudi nzima. Masuala tofauti ya nafasi na utume wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na ushirikiano wa Baraza la Maaskofu na Tume za Mafundisho vimeweza kuwekwa bayana kwa  washiriki wote katika mkutano huo. Kadhalika Misa zilizoadhimishwa kwa siku hizi ziliendana na Ibada za makanisa yaliyomo ndani ya nchi  ambapo zimeweza kweli kuleta furaha ya asili kwa namna ya kuonesha umoja katika utofauti wa Kanisa nchini India.

Na zaidi wakati wa Chakula cha mchana na jioni kwa siku tatu imekuwa ni fursa na uwezekano wa kufanya tafakari ya kina ya kuwasiliana moja kwa moja na washiriki kwa kujenga urafiki kati yao. Washiriki wa Mkutano huo wamethibitisha kupendezwa sana na ukarimu wa makaribisho katika Chuo Kikuu cha Madaktari huko Bangalore India. Na mkutano wa  Kitaalimungu umekuwa na utajiri mkubwa sana kwa washiriki, kama vile Maaskofu na wataalimungu wenyewe ambao wamealikwa kushirikiana kwa dhati katika utume wa pamoja wa Kanisa. Mkutano umehitimishwa ukiwa na matumaini ya kwamba, Watu wa Mungu waliounganika chini ya usimamizi wa Maaskofu, utaendelea kuchangia kwa dhati wema wa pamoja katika nchi hiyo kubwa!

25 January 2019, 16:29