Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu John Bonaventure Kwofie, C. S. Sp kuwa askofu Mkuu wa Accra nchini Ghana Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu John Bonaventure Kwofie, C. S. Sp kuwa askofu Mkuu wa Accra nchini Ghana  (Vatican Media)

Ghana:Jimbo Kuu la Accra limempata Askofu Mkuu mpya!

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu John Bonaventure Kwofie, C. S. Sp kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuuu Katoliki Accra nchini Ghana. Hadi uteuzi wake alikuwa ni Askofu wa Jimbo Sekondi-Takoradi

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu John Bonaventure Kwofie, C. S. Sp kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Accra nchini Ghana. Hadi uteuzi wake alikuwa ni Askofu wa Jimbo Sekondi-Takoradi. Askofu Mkuu Mteule John Bonaventure Kwofie, C.S.Sp., alitangazwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa askofu wa Jimbo la Sekondi -Takoradi kunako tarehe 3 Julai 2014, wakati akiwa ni Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu huko Afrika ya Magharibi.

Alizaliwa tarehe 26 Aprili1958 huko Powa katika Jimbo la Sekondi – Takoradi, Ghana. Majiundo yake ya kufalsafa katika Chuo cha Roho Mtakatifu cha Isienu –Nsukka nchini Nigeria (1981-1983). Tangu 1983-1994 alimaliza mwaka wa kichungaji katika Parokia ya Rosari Takatifu huko Suema, Jimbo Kuu la Kumas nchini Ghana. Kunako 1984-1988 aliendelea na masomo ya Taalimungu katika Seminari ya Mtakatifu Paulo huko Gbanga nchini Liberia na kupata shahada.

Alifunga nadhiri kunako tarehe 2 Agosti 1987 na kupewa daraja Takatifu la Upadre kunako tarehe 23 Julai 1988 Kumasi. Mwaka 1991-1995 aliendela na Masomo ya Biblia Takatifu mjini Romana  na kunako 1995-2004 amewahi kuwa  Makamu wa Rais wa Baraza la Watawa kwa Upande wa Afrika na kuongoza tena kwa miaka miwili  kadhalika kuwa  Mkuu wa Chama cha Mashirika ya Afrika ya Magharibi; Mwaka 2004-2012 amewahi kushika nafasi ya Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu kabla ya kuchaguliwa kuwa Askofu wa Sekondi – Takoradi.

02 January 2019, 16:30