Dk.Gisotti Msemaji mkuu wa habari Vatican akizungumza na waandishi Dk.Gisotti Msemaji mkuu wa habari Vatican akizungumza na waandishi 

Dk.Gisotti Msemaji mkuu wa habari Vatican azungumza na waandishi

Tarehe 2 Januari 2019, katika ukumbi wa habari Vatican, Msemaji Mkuu wa mpito kwa vyombo vya habari Bwana Alessandro Gisotti amewasalimu waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Vatican

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Dk. Alessandro Gisotti Msemaji mkuu wa mpito  wa vyombo vya habari Vatican, asubuhi tarehe 2 Januari 2019 ameweza kuwasalimia waandishi wa habari kwa mara ya kwanza katika nafasi aliyopewa  katika ukumbi wa habari Vatican. Akianza na salam amesema: “Ninataka kushukuru wenzangu kwa ujumbe wenu nilio upokea na ambao unaonesha upendo kwangu na ulewa kwa kipindi hiki maalum cha Mawasiliano Vatican”.

Akiendelea Bwana Gisotti amesema, kama jinsi alivyo kwisha sema juu ya shughuli yake ya kipindi cha mpito aliyokabidhiwa, ataweza kuifanya kwa roho ya huduma na uwajibikaji, akitiwa moyo na imani na Baba Mtakatifu na Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Bwana Paulo Ruffini na kwa msaada wa familia yake  wakati huo huo hata  timu kubwa ya kitaalam kwa uwajibikaji wa wenzake katika kazi,  ambao asubuhi hiyo Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano  amependa kuonesha, wakati wanaendelea kufanya kazi katika  kipindi hiki cha mpito.

Kwa kuthibitisha hili ametoa ahadi ya uwajibikaji wake hai na  kufanya kazi pamoja pia wakati huo akiomba kuwa na uvumilivu kutokana na makosa ambayo yanaweza kujitokeza wakati wa kipindi hiki cha hatua za mwanzo. Hata hivyo hakusahau kutoa taarifa kwamba, wang’atuka katika nafasi hiyo, Bwana Greg Burke na Bi. Paloma García Ovejero wamethibitisha  kumpatia ushirikano wao ili kumsaidia katika hatua hiyo nyeti. Na tarehe 1 Januari 2019, tayari wameshinda pamoja katika ofisi ya Habari Vatican ili kupata maelekezo zaidi. Na amehitimisha kwa kusema, "kwa wastani ni jambo ambalo nimelipongeza na nilitaka kuwashirikisha wote".

Ikumbukwe tarehe 31 Desemba Baba Mtakatifu Francisko amekubali maombi ya kung’atuka kwa wasemaji mkuu na makamu wa vyombo vya habari Vatican, Dk. Greg Burke na Dk. Paloma García Ovejero na  badala yeke akaridhia kumteua Msemaji Mkuu wa kipindi cha mpito wa Vyombo vya habari Dk. Alessandro Gisotti ambaye hadi uteuzi wake alikuwa ni mratibu wa Mtandao wa kijamii wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

Bwana Alessandro Gisotti, alizaliwa mjini Roma  miaka 44 iliyopitia na mwenye familia ya watoto wawili. Majiundo yake katika Chuo Kikuu La Sapienza Roma na kujipatia shahada ya Sayansi ya Siasa na tangu mwaka 1999 ni mwandishi wa habari kitaaluma aliyojinyakulia kwa  shahada ya uandishi wa habari katika Taasisi ya Uandishi wa Habari ya Wajesuit  Chuo Kikuu cha Laterano Roma. Mara baada ya uzoefu wa ofisi ya Habari za Umoja wa Mataifa mjini Roma alianza kufanya kazi katika idhaa ya  Matangazo ya  Radio Vatican kunako mwaka 2000.

02 January 2019, 17:45