Tafuta

Vatican News
Ofisi ya Sadaka ya Papa inajikita kusambaza mifuko yenye mablanketi mazito, hata kuongeza vitanda  katika nyumba za kulala watu wasio kuwa na makazi mjini Roma Ofisi ya Sadaka ya Papa inajikita kusambaza mifuko yenye mablanketi mazito, hata kuongeza vitanda katika nyumba za kulala watu wasio kuwa na makazi mjini Roma 

Dharura ya baridi:Juhudi za mfuko wa sadaka ya kitume!

Shughuli za ofisi ya sadaka ya kitume mjini Vatican inaendelea kijikita kwa kasi kuwasaidia maskini katika mji wa Roma. Kufuatia na wimbi la baridi kali, wamekazana kusambaza mifuko yenye mablanketi mazito, hata kuongeza vitanda katika nyumba za kulala watu wasio kuwa na makazi mjini Roma

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ofisi ya Sadaka ya Papa mjini Vatican, haijakutwa bila kuwa na maandalizi kwa kipindi maalum cha wimbi la baridi ambayo inazidi kuishambulia mji wa Roma na kwingineko. Ofisi ya Sadaka Vatican, imeongeza jitihada za kukabiliana na dharura hiyo kwa maskini , hasa wale wasio kuwa na makazi kwa kuwapatia mablanketi mazito ya kukabiliana na hali ya hewa hasa wasio jiweza ili kuwafariji mateso yao japokuwa wengine bado wanapendelea kulala barabarani.

Nafasi zaidi za vitanda kwa wale wenye kuhitaji

Katika kituo kiitwacho Zawadi ya huruma cha kulala, ofisi kuu ya sadaka Vatican, imeongeza hata vitanda vya kuweza kulala wale wenye kuhitaji ili wajikimu na kuthibiti baridi kali. Jengo hilo linaendeshwa na watawa wamisionari wa upendo wa Shirika la Mama Teresa wa Kalkuta, mahali ambapo watu wa kujitolea wanafanya uzoefu wa kuwasaidia watu wengi ambao wanalala mara nyingi barabarani. Anayebisha hodi pale anaweza kubaki hata mwezi mmoja, lakini pia lazima aondoke  na kusubiri miezi mingine kabla ya kurudi tena. Huo ni utaratibu ulio wekwa kwa ajili ya kumsaidia mgeni aweze kujitafiti na kutafuta njia mbadala au kurikifiria zadi kama mtu wa kuweza kujikimu maisha yake binafsi. Watu hao pia wanawahikikishia wanapata hata chakula cha usiku wakifika kulala.

Kanisa la Mtakatifu Calisti Roma limefunguliwa

Hata kipindi cha baridi mwaka huu, kama ilivyojitokeza hata miaka iliyopita, wamefungua milango ya Kanisa la Mtakatifu Calisti nje ya mji wa Vatican, karibu na parokia ya Mtakatifu Maria Trastevere Roma ni Kanisa linaloendeshwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio.

Katika eneo hili, vipo vitanda karibia 30 ambavyo vimewekwa kwa ajili yao hata chakula cha jioni kwa wageni hao. Kadhalika ndani yake kuna kituo cha kiitwacho, Watu wa amani. Ni mahali ambapo unapata sehemu ya kufulia nguo kwa watu masikini, kwani ni zawadi iliyotolewa na Baba Mtakatifu Francisko ikiwa ni mashine sita za kufua nguo, sita za kukausha na zaidi hata pasi za umeme kwa ajili ya kunyosha nguo zao. Kadhalika kila Jumanne na Alhamisi kwa wiki kuna ugawaji wa chakula cha moto katika jiko moja kwenye Kanisa la Mtakatifu Maria Mkingiwa dhambi ya asili na msimamizi wa Kanisa hilo ni Kardinali Konrad Krajewski ambaye ndiye Msimamizi  Mkuu wa Sadaka ya Papa Vatican, wakati huo huo kuna hata ugawaji wa chakula katika kituo kikuu cha Treni mjini Roma.

Kufikiria hata kwa wanyama wanaoishi na watu wasio kuwa na makazi

Habari nyingine zaidi ni kwamba wakati wa kufikiria watu wasio kuwa na makazi, shukrani pia ziwandee mkakati wa Chama cha Kijeshi cha Malta  (Smom) na clinic moja ya wanyama iliyopo Ostia Lido, kwani Mkuu wa sadaka Vatican amefikiria hata wanyama wanaoishi na watu wasio kuwa na makazi. Kwa wanyama hao, wamependekeza mpango wa upimaji bure wa wanyama katika manispaa ya Roma kila Domenika ya tatu ya kila mwezi kuanzia saa 4.00 asubuhi  hadi saa 6.30 mchana masaa ya Ulaya.

05 January 2019, 11:11