Tafuta

Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani limemwandikia Papa Francisko ujumbe wa shukrani na matashi mema. Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani limemwandikia Papa Francisko ujumbe wa shukrani na matashi mema. 

Ujumbe wa Maaskofu Katoliki Marekani kwa Papa Francisko

Kardinali Daniel N. DiNardo katika ujumbe wake, anaendelea kusema, umoja na ukaribu huu unapania kuwapatia hekima na nguvu ya kuweza kukabiliana na changamoto pevu zilizoko mbele yao katika maisha na utume wa Kanisa. Katika kipindi hiki cha mafungo, ndani mwao wamebeba mateso na mahangaiko sanjari na matumaini ya watu wa Mungu, hasa wale ambao wametaka tamaa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Kardinali Daniel N. DiNardo, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani, USCCB, mwanzoni mwa mafungo yanayoendeshwa na Padre Raniero Cantalamessa, Mhubiri wa nyumba ya kipapa kwa kuongozwa na kauli mbiu “Akaweka watu kumi na wawili, wapate kuwa pamoja naye, na kwamba awatume kuhubiri” kama sehemu ya mchakato wa toba na wongofu wa kichungaji na kimisionari, amemwandikia ujumbe Baba Mtakatifu Francisko, akimwomba awasindikize Maaskofu Katoliki Marekani walioanza mafungo yao hapo tarehe 2-8 Januari 2019 ili waweze kujenga na kudumisha umoja na mshikamano wa dhati katika urika wao kama Maaskofu pamoja na kujenga mafungamano ya dhati na Kristo Yesu.

Kardinali Daniel N. DiNardo katika ujumbe wake, anaendelea kusema, umoja na ukaribu huu unapania kuwapatia hekima na nguvu ya kuweza kukabiliana na changamoto pevu zilizoko mbele yao katika maisha na utume wa Kanisa. Katika kipindi hiki cha mafungo, ndani mwao wamebeba mateso na mahangaiko sanjari na matumaini ya watu wa Mungu, hasa wale ambao kwa namna moja au nyingine, wamejisikia kukatishwa tamaa na Kanisa.

Kardinali Daniel N. DiNardo anamshukuru Baba Mtakatifu kwa kukazia umoja na mshikamano katika urika wa Maaskofu na kwamba, maisha na utume wa Kanisa kwa siku za usoni ni neema na baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu na matumaini yanayobubujika kutoka kwa Kristo Yesu, msingi thabiti wa matumaini ambayo kamwe hayawezi kuteteleka. Kwa njia ya sala na sadaka zao, Maaskofu wa Marekani wanapania pia kujenga umoja na mshikamano na Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Kardinali Daniel N. DiNardo, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani, USCCB, anahitimisha kwa kusema, ushuhuda wa upendo na mshikamano kwa maskini na wale wote wanaoteseka sehemu mbali mbali za dunia, kutoka kwa Papa Francisko unawatia shime kusonga mbele, ili kukuza na kudumisha umoja na mafungamano katika Kanisa la Kiulimwengu.

Maaskofu USA: Toba
04 January 2019, 12:39