Tafuta

Vatican News
Papa Leone XIII aliandika Waraka wa Catholicae ecclesiae 1890 kwa maaskofu katoliki duniani unaojikita kutazama haki,msaada ubinadamu na ukomeshaji wa biashara ya utumwa Papa Leone XIII aliandika Waraka wa Catholicae ecclesiae 1890 kwa maaskofu katoliki duniani unaojikita kutazama haki,msaada ubinadamu na ukomeshaji wa biashara ya utumwa  (Vatican Media)

Waraka wa "Catholicae ecclesiae" wa Papa Leone XIII!

Kila mwaka katika Siku Kuu ya Epifania ya Bwana,maparokia yote duniani katoliki huandaa makusanyo kwa ajili ya baadhi ya majimbo mengi duniani ili kuwasaidia katika maendeleo ya kichungaji. Utamaduni huu ulianzishwa katika karne ya XIX,kwa Waraka wa Papa Leone XIII wa "Catholicae ecclesiae" kwa maaskofu katoliki duniani 1890 na kumpa nguvu zaidi Kard.Charles Lavigerie

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kila mwaka katika Siku Kuu ya Epifania ya Bwana, maparokia yote katoliki duniani na kwa namna ya pekee nchini Ufaransa huandaa makusanyo kwa ajili ya baadhi ya majimbo barani Afrika ili kuwasaidia katika maendeleo ya kichungaji. Utamaduni huu ni wa kizamani kwani ulianzishwa katika karne ya XIX, wakati Kardinali Charles Lavigerie, Mwanzilishi wa Mapadre wamisionari weupe (White Fathers) kutoka Ufaransa alipoanza utume wake barani Afrika. Huyu ni mwamasishaji mkuu katika jamii ya  kupinga utumwa na ambapo  aliwatia moyo na mshikamano kati ya wakristo wa miji mikubwa, hata yaliyokuwa yanataliwa na ukoloni wa kati ule kwa ruhusa kutoka kwa Baba Mtakatifu wa wakati ule.

Kunako mwaka 1888 Kardinali Lavigeria alianza kutafuta michango ya kifedha ili kuweza kutoa huduma katika hali iliyokuwa inaendelea ya tumwa barani Afrika na kuwasaidia watu hao waweza kuwa watu huru. Na kwa namna hiyo  aliweza kuungwa mkono zaidi na Kanisa kwani kunako tarehe 20 Novemba 1890, Papa Leone XIII alitoa Waraka wake Catholicae Ecclesiae na ambapo aliamua kila mwaka katika siku ambayo wanaadhimisha Fumbo la Epifania ya Bwana waweze kukusanya mchango wa fedha na kuutuma katika kanda za kimisionari huko Afrika, lakini si kwa ajili ya kufanya propaganda ya Mafundisho ya Kiinjili, bali ili kutoa msukumo zaidi wa watu katika kujiendeleza na kuondokana na uzito wa utumwa wa kibinadamu. Siku hiyo ilichanguliwa tarehe 6 Januari  siku hiyo kwa mujibu wa Papa katika waraka wake anasema, mwana wa Mungu kwa mara ya kwanza alizungumza na watu akiimanisha Mamajusi kutoka Mashariki ya mbali. Lakini basi ebu tuuune waraka huu wa Catholicae Ecclesiae kwa ajili ya kila asikofu katoliki duniani.

Je katika waraka wa Papa Leone XIII wa Catholiae  ecclesiae kwa maaskofu katoliki duniani unahusu nini?

Unatazama, utaratibu wa haki na ufumbuzi, usimamiaji wa kifedha na gaharama au za kidini, haki na mafanikio yatokanayo na msaada wa kukomesha biashara na dhamana ya ustawi wa jamii. Tarehe 20 Novemba 1890 Papa Leone XIII aliandika barua ya kitume ya Kanisa katoliki  kwa maaskofu duniani kote. Katika waraka huo unasema, Kanisa Katoliki linakumbatia watu wote kwa upendo wa kimama na ambalo limekuwa na moyo mkuu tangu uasili wake kama wote wajuavyo hasa kwa kuona wanafikia lengo la kukomesha na  kuondoa moja kwa moja utumwa ambao ni mzigo mzito na ukatili ambao umewakumba watu wengi na kati ya wote waliokufa. Kwa hakika kama msimamizi wa watu katika mafundisho ya Mwanzilishi wa Kanisa  na ambaye yeye binafsi katika maneno yake kwa mitume alikuwa amewafundisha watu kuishi undugu ambao unawaleta wawe pamoja na wenye kuwa na asili moja na ambapo wamekombolewa kwa thamani moja na ambao wanaalikwa wote katika heri na Kanisa linawachukua katika mikono yake watu wote weusi, ambao wamekuwa watumwa na kuwahakikishia uhuru kama ilivyotabiriwa katika nyakati na kujikita kwa lengo hilo taratibu na kwa uratibu.

Papa Leone XIII Kanisa linajikita kutoa uhuru wake kwa watumwa

Katika mchakato wa  karne nyingi, Papa Leone XIII anaandika, Kanisa halikwenda kamwe polepole katika kutoa uhuru kwa watumwa; badala yeke matunda mengi katika matendo yake yamekuwapo kwa kadiri ilivyozidi kuongeza wajibu wake. Hayo yanathibitishwa na nyaraka nyingi za kihistoria ambapo  kwa mujibu wa Papa anatoa pongezi kwa watangulizi wake, akiwataja kati yao kuwa ni Mtakatifu Gregorio Mkuu, Adriano I, Alessandro III, Innocenzo III, Gregorio IX, Pio II, Leone X, Paolo III, Urbano VIII, Benedetto XIV, Pio VII, na Gregorio XVI, ambao walijikita katika shughuli ya kuhamasisha ili suala la kukomesha  utumwa mahali ambapo kulikuwa na utumwa uweze kuondolewa mizizi yake kabisa, na mahali ambapo walikuwa wamekwisha ondoa basi vichipukiza viweze kutoa kwa mara nyinge tena.

Katika Waraka wa Papa Leone XIII unathibithisha kuwa, urithi huo mkuu uiochwa kwao na watangulizi hao husingeweza kukataliwa na ambapo hawakuwaacha bila kujihukumu na kushutumu vikali janga hili kubwa la utumwa na ili kuweza kuhamasisha zaidi katika kujadili katika barua iliyoandikwa tarehe 5 Mei 1888 kwa Maaskofu wa Brazil ambapo Papa anawapongeza kwa kile walichokifanya na zaidi kazi ya kupongezwa kwa mfano katika shughuli iliyofanyika kwa wakazi katika nchi hiyo hasa ya kuwapatia uhuru watumwa na kwa pamoja wote walionesha jinsi gani utumwa unakwenda kinyume na dini na hadhi ya mwanadamu.

Watu kufungwa minyorororo na kuwekwa kwenye masoko kama wanyama na kuuzwa

Kwa hakika, wakati walikuwa wakiandika  mambo haya, Papa Leone XIII anathibitisha kwamba walikuwa wakihisi kwa nguvu ile huruma juu ya hali ya wale ambao wamesongwa; na zaidi walikuwa wahisi mshangao mkubwa kuhusu historia za mateso ambayo wakazi wa kanda fulani za Afrika walikuwa wakikandamizwa. Ni jambo la kutia uchungu nakuogofya sana kwa  kutambua kwa dhati kwa njia ya habari za kuaminika ambapo zinazema kuwa karibia watu laki nne wa Afrika, bila kujali umri na jinsia, kila mwaka kwa nguvu kubwa wanatekwa nyara kutoka katika vijiji vyao fukara na ambapo, wanafungwa kwa minyororo na kupigwa mijeredi au fimbo wakati wa kiwa katika msafara wa kupelekwa kwenye masoko ambayo kama wanyama huwekwa kwenye maonyesho na kuuzwa.

Mbele ya ushuhuda ya wale walioona mambo haya na uthibitisho wa hivi karibuni wa wachunguzi wa Kanda yote ya Ikweta barani Afrika, Papa Leone XIII anathibitisha kwamba, walihisi ile shauku hai ya kutaka kwenda na kwa mujibu wa nguvu zao ili kuwasaidia watu wasio na furaha na kupeleka kitulizo dhidi ya taabu yao. Kwa njia  hiyo, bila kuchelewa,walimtuma mtoto wao mpendwa Kardinali Charles Marziale Lavigerie, ambaye tayari alikwisha julikana kwa juhudi zake na uhai wa kitume ili kwenda katika miji mikuu ya Ulaya aweze kuwafanya watambue uharifu wa soko hili la aibu na kuwashawishi wakuu na wananchi aweze kupeleke msaada kwa watu wengi ambao wanaishi maisha yasiyo na furaha.

Lazima kumshukuru Bwana Yesu Kristo Mwokozi

Katika barua yake Papa Leone XIII aidha anasema, tunapaswa kumshukuru Kristo Bwana, Mwokozi na mwenye upendo zaidi wa mataifa yote, ambaye kwa rehema yake hakuruhusu shahuku zao zipotea, lakini anataka kufanikiwa  na kuwa karibu kama mbegu pandwa ndani ya udongo wenye rutuba na  ambayo inahidi ukusanyaji mzuri. Kwa hakika Watawala wa watu na Wakatoliki duniani kote na wale wote wanaoheshimu haki za watu na uasili, wataungana kwa pamoja kufanya utafiti ambao ni kwa namna gani hasa umuhimu zaidi wa kuweza kukomesha baashara hiyo ya kibinadamu.

Kongamo mjini Bruxelles

Kongamano la msingi lilikuwa limefanyika mjini Bruxessels, ambalo liliwakusanya watawala wa Ulaya na mkutano mwingine uliokuwa umefanyika wa watu binafsi, lakini ambao ulikuwa na nia moja na kwa ukarimu wa mapendekezo walikutanika mjini Paris, ambao kwa hakika walionesha wazi kwamba sababu ya teso hilo la  watu weusi italindwa na nguvu na ambapo inahitahijika muundo mpya ili kuweza kukomesha janga la maskini hawa wanaonyanyaswa. Kutokana na hili, Papa Leone XIII anathibitisha kuwa ndiyo sababu hawataki kupuuza fursa mpya ambayo inajiwakilisha na pia kuwapongeza Watawala wa Ulaya na wahusika wengine wenye mapenzi mema.

Hata hivyo Papa aliandika kuwa, kwa Mungu mkuu tuombe kwa uaminifu ili aweze kutoa furaha ya kufanikiwa kwa mipango yao na kwa miundo mipya mikubwa ya kuweza kuondoa mizizi ya biashara kama hiyo ya utumwa. Lakini, pamoja na huduma ya kulinda uhuru, huduma nyingine kubwa zaidi Papa anasema inatazama Shughuli za kitume katika Baraza kuu la Vatican ambalo ni katika  mahitaji ya kupendekeza ili kufanya huduma katika kanda za Afrika na ambazo ni kujitahidi kueneza mafundisho ya Injili   kwa mwanga wa ukweli wa Mungu na uweze kuangaza watu hao ambao pia wamelala katika giza na dhiki kutokana na ushirikina kipofu, ili waweze kushiriki na kuwa sehemu ya urithi wa ufalme wa Mungu.

Shughuli hiyo Papa Leone III anathibitisha, iweze kujikita katika kuwatibu hata wao zaidi na kuwa na bidii kubwa, kwa sababu ya watu wale ambao wamepatikana kutokana na mwanga wa kiinjili, watakuwa wameondokana na minyororo yao ya utumwa wa kibinadamu. Kwa hakika mahali penye desturi na sheria za kikristo, mahali ambapo dini inawafundisha watu kuheshimu haki na kuheshimu hadhi ya kibinadamu; mahali ambapo kuna uenezi mkubwa wa roho ya upendo kindugu ambayo Kristo alitufundisha, hapawezekani kuwa na utumwa, wala ukatili wala ushenzi; badala yake ni kushamiri ukunjufu wa utamaduni na uhuru kikristo unaofuatana na ustaarabu.

Wamisionari ambao tayari wamekwenda katika kanda za kitume

Papa Leone XIII anaandika kuwa, tayari watu kadhaa wa kitume kama walinzi wa Kristo, wamekwenda katika kanda kwa ajili ya afya ya ndugu, lakini pia aliweza si kutokwa jasho tu bali hata kutoa maisha yao. Hata hivyo, mavuno ni mengi, lakini wafanyakazi ni wachache; kwa maana hiyo ni muhimu kwamba wengi zaidi kwa kuongozwa na roho ile ile ya Mungu, bila hofu au hatari, au usumbufu, wala uzito wa kazi ngumu, wanaendelea kuwapo katika maeneo hayo na ambapo kuna zoezi la biashara ya aibu na ili wapate kupeleka kwa wenyeji hao mafundisho ya Kristo yanayowafikia pamoja na uhuru wa kweli. Picha ya hiyo Papa anaongeza kuandika, inahitajika shughuli kubwa yenye mvuto  kwa maana ya kuwa na zana  sawa na ukubwa wake.

Kwa hakika haiwezekani kutazamia hilo bila kuwa na uwezekano wa mkubwa wa Taasisi za kimisionari, wa kufanya safari ndefu, wa ujenzi wa makazi, kufanya uchaguzi na makubaliano kati ya makanisa na mambo mengine ya  lazima. Papa Leone XIII alionesha ulazima wa kusaidia baadhi ya gharama hizo kwa miaka kadhaa mpaka maeneo hayo ya uinjilioshwaji yanafikia hatua ya kujitegemea. Papa alibainisha kuwa, Mungu alitaka kuwa, wao wawe na zana za kuweza kustahimili uzito huu, lakini kwa kutumia utupu mkubwa na uwezo wao huo waliokuwa wakijita kwa kutumia sauti kama ya Baba, Baba Mtakatifu na ambapo alitoa wito kwa ndugu wote maaskofu  na wakatoliki wote, akiwataka wawe na upendo wao mtakatifu katika matendo yao ya ukarimu. Kwa dhati kuna haja ya  kila mtu kushiriki, hata kwa mchango mdogo, ili uzito huo uweze kugawanyika kati ya wengi na kuwa mwepesi.

Na  katika yote ili kuenea neema ya Kristo, kuenea kwa neema ya Kristo na ambapo hatimaye amani, msamaha wa dhambi na zawadi yoyote yenye thamani iweze kutua kwa watu hawa.  Kufuatia hilo Papa Leone XIII aliandika kuwa kila mwaka mahali ambapo wanaadhimisha fumbo la Epifania, makusanyo ya fedha yawe kwa ajili ya shughuli iliyokubushwa. Amechagua siku hi ina siyo nyingine kwa sababu kama wanavyotambua maaskofu wote, Siku ile Mtoto wa Mungu kwa mara ya kwanza alijionesha kwa watu wote, wakati wa safari ya Mamajusi na ambapo Mtakatifu Leone Mkuu mtangulizi wake aliwaita kuwa hao ni matunda ya kwanza ya wito na imani. Ni matumaini ya Papa Leone XIII kwamba Kristo Bwana, aliyeongozwa na upendo na kwa maombi ya watoto ambao walipokea mwanga wa ukweli wakati wakiheshimu umungu wake, waangaziwe hata wale wasio kuwa na furaha na ambao ni sehemu ya kubwa ya binadamu na awaondolee matope ya tabia za ushirikina na hali chungu ambayo wamelala katika maovu kwa muda mrefu.

Matumizi ya fedha za kimisionari kwa mujibu wa Papa Leone XIII

Fedha ambazo zikusanywe siku hiyo katika makanisa na makanisa madogo chini ya mamlaka ya maaskofu, ziwakilishwe mjini Roma katika Baraza la Kipapa la Uinjilishi wa watu. Itakuwa ni shughuli ya Baraza hilo kugawa fedha hizo miongoni mwa vituo vya kimisionati vilivyopo au vitakavyoanzishwa katika Kanisa la Afrika na zaidi katika maeneo yaliyo athiriwa na ili kuweza kuwakomboa watumwa. Kadhalika  kama wanavyokumbuka fedha hizo ni kwa ajili ya kudumisha na kukuza hadhi ya mwandamu. Sadaka nyingine itakayobaki iweze kutumika kwa busara kati ya wale wanaohitaji zaidi ambalo Baraza la Kipapa linatambua mahitaji ya kimisionari.

Hatimaye Papa Leone XIII akihitimisha waraka wake anasema, hana shaka kwamba Mungu mwingi wa rehema na  neema atapokea zawadi ambazo zitatolewa kwa ajili watu wasio kuwa na furaha wa Afrika, huku akiwahimiza maaskofu kujikita kwa dhati katika utashi wa kazi yao ili kweli maazimio hayo yaweze kuimarika na kuridhisha. Vilevile alikuwa anaamini kwamba  msaada huo wa kipindi kifupi na maalum ambacho waamini wametoa kwa ajili ya kukomesha janga baya la biashara ya utumwa  wa  kibinadamu na kwa ajili ya wajumbe wa kueneza Injili katika maeneo ambayo bado haijafika Injili hautapunguza kwa dhati ukarimu ambao umetokana na kuhamasishwa kwa misheni katoliki, na kwa msaada wa fedha zilizokusanywa na Taasisi ya mwanzilishi wa Lion nchini Ufaransa, anayejulikana kama mwanezaji wa Imani( Yaani Kardinali Ravigerie). Shughuli hii ni mwafaka na ambao unahimiza tayari waamini na unawakilisha fursa ya kutoa shukrani kwa upya  kwa wale wote ambao watajikita katika kufungua mikono yao ya wema ili kuweza kuchanua mafanikio mazuri. Na kwa maaskofu wote, makleri na waamini wote, Papa Leone XIII aliwakabidhi shughuli ya kuchungaji kwa dhati na kuwapa Baraka ya kitume.

11 January 2019, 15:12