Tafuta

Vatican News
Inabidi kukuza na kuhamasisha utamaduni wa Tiba Mbadala ili kupambana na utamaduni wa ubaguzi dhidi ya wagonjwa yasiyo na tiba na eutanasia Inabidi kukuza na kuhamasisha utamaduni wa Tiba Mbadala ili kupambana na utamaduni wa ubaguzi dhidi ya wagonjwa yasiyo na tiba na eutanasia 

Qatara:Askofu mkuu Paglia anasema ni lazima kupambana na utamaduni wa ubaguzi!

Mkutano ulioanza tarehe 22 Januari 2019 huko Qatar unahusu mazungumzo ya waislam na wakristo katika mtazamo wa tiba mbadala na maisha. Ni tukio la kujifunza kwa pamoja katika mpango mkubwa wa Baraza la Kipapa la Maisha ili kueneza na kuhamasisha njia ya tiba mbadala duniani

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, Rais Taasisi ya Kipapa ya Maisha amefungua Jukwaa la siku mbili, Jukwaa iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Georgetown Washington na Doha na mpango (WISH) wa Chama cha Qatar, kuanzia tarehe 22 Januari 2019. Kiini cha Mkutano huo ni tiba mbadala na mwisho wa maisha kwa mantiki ya kiislam na kikristo.

Tiba mdala kama haki

Askofu Mkuu Vincenzo Paglia katika hotuba yake ameanza kufafanua jinsi ya mchakato wa kuanzishwa tiba mbadala karibu ya nusu karne iliyopita na kuonesha umuhimu wa mada ndani na nje ya madawa, kwa nyakati za sasa ambazo watu wanagusa kwa mikono yao na kuonja baguzi na uondoaji wa watu walio wadhaifu zaidi kama vile wale wanaoteseka na magojwa magumu, walemavu au magonjwa yasiyotibika. Tiba mbadala inawakilisha haki kibinadamu amesema na ambayo inataka kupinga zaidi utamaduni wa ubaguzi ambao unataka kuendeleza eutanasia na kuliona kama jambo la kawaida na kutojali wengine. Na ili kuweza kupamba na utamaduni wa ubaguzi ni muhimu kuhamasisha utumaduni wa tiba mbadala amekazia. Kwa kujikita katika kutimiza hili, Askofu Mkuu Paglia anathibitisha kwamba ni dharura nyeti ya kuweza kutafakari na kukabiliana kwa kina masuala magumu ya kibinadamu na changamoto kubwa za maadili zilizopo mbele yetu, kwa kulinganisha na masuala yanayohusu mwisho wa maisha. Kwa siku hizi mbili kazi ya jukwaa ilikuwa inaelekeza namna ya kufanya utafiti wa mchango unaotolewa na tiba mbadala katika uhusiano wa watu wenye kuhitaji msaafa na ambao unatokana na msingi wa roho ya kibinadamu.

Mchango mmoja wa dini

Akikabiliana na mada ya mchango wa dini mbalimbali katika kutoa uhai wa dhati kwenye mfumo huu wa kusindikiza watu wagonjwa au karibia na kufa, Askofu Mkuu Paglia ameonesha uwezo mkubwa wa dini ambazo zina uwezo wa kuofuka kila  pembe ya mwanadamu, lakini pia hata utendaji wa dini ambazo zinajieleza kati ya nguvu za kweli na tiba mbadala. Utambuzi wa mtu kujifungulia kwa aliye juu, unathibitisha kuwa maisha ya binadamu hata kama ni madhaifu kutokana na kushambuliwa na magonjwa bado ni yenye thamani isiyokuwa na kifani. Tiba mbadala bado inauwezo mkubwa wa kujikita ndani ya maono ya mtu,ambapo katika tamaduni kubwa za kidini zinalinda na kuhamasisha. Huo ndiyo mchango wa kina na wa dhati ambao wanaweza kuupokea ikiwa  na maana ya kutoa chachu na kuigwa inaweza kuwakilisha leo hii kwa wote pendekezo la dhati linalpjikita ndani ya mantiki ya umaskini wa upendo kwa binadamu na kipeo cha mahusiano ya kijamii ambayo kwa ujumla yanarudi nyuma na kutoshirikishana kijamii na kukumbwa hata mitindo ya kijumuiya kuanzia na familia.

Kuna haja ya kuwa na udugu katika nyakati za sasa

Akikumbuka Maneno ya Baba Mtakatifu Francisko ya hivi karibuni wakati wanaadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Kipapa ya Maisha, ambapo Baba Mtakatifu anabinisha kutafuta namna ya kufanya ubunifu wa udugu mpya ambao ni changamoto ya mafundisho ya kibinadamu na kijamii katika nyakati zetu. Askofu Mkuu Paglia katika hotuba yake amesema, dini zote zina uwezo wa kuwa na neno moja maalum la kuweza kusema. Zoezi la kulinda mwingine na kazi ya uumbaji ndiyo tabia msingi wa kuweza kufanya ili kupambana na warararuaji na uhalibifu ambao mara nyingi umejionesha kwa binadamu ( si tu kwa ajili ya kazi ya uumbaji na mazingira, lakini pia hata dhidi ya ndugu na zadi anapofikiriwa kama kizingiti au hana faida kwa sababu ya mafao binafsi). Kwa maana hiyo, Jumuiya za tiba mbadala zinashuhudia mtindo mpya wa kuishi na kuweka kitovu cha mtu wema wake ambao si tu binafsi, bali hata kwa jumuiya nzima katika upamoja unaotarajiwa. Katika jumuiya ya wema wa pamoja inatafuta ustawi wa wote. Tiba mbadala inawakilisha haki ya binadamu na mipango ya kimataifa inatafuta hilo leo hii; lakini kiukweli haki ya binadamu inaendelea kutambuliwa na kupokelewa kama mjumbe wa jamii na kama sehemu moja ya jumuiya nzima, amehitimisha hotuba yake.

24 January 2019, 16:31