Kanisa Katoliki limekamilisha vituo vya afya kama ifuatavyo:hospitali 5,287, zahanati  15,397 na makazi 15,722 ya wazee na walemavu wenye kuhitaji duniani kote Kanisa Katoliki limekamilisha vituo vya afya kama ifuatavyo:hospitali 5,287, zahanati 15,397 na makazi 15,722 ya wazee na walemavu wenye kuhitaji duniani kote  

Askofu Mkuu Jurkovič anasisitiza huduma ya Afya kwa wote ili kufikia malengo endelevu!

Katika Mkutano wa 144 wa Tume ya Utendaji wa Shirika la Afya ulimwenguni,Vatican inatoa wito wa kuhamasisha wadau wote ili kuchukua hatua za kukuza huduma za afya zilizo msingi na katika kuhudumia afya ya wote

Na Sr.Angela Rwezaula – Vatican

Askofu Mkuu Ivan Jurkovič Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa,zilizoko Geneva,ametoa hotuba yake tarehe 28 Januari 2019 katika Mkutano wa Tume ya Utendaji ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kuhusu mada ya huduma ya afya kwa wote. Askofu Mkuu anathibitisha utambuzi wa majukumu na nafasi iliyo nayo Shirika la Afya ulimwenguni,pamoja na UNICEF na Serikali ya Kazakhstan kwa kukubali kuwa mgeni wa Mkutano wa Kimataifa uliokuwa unahusu Huduma msingi ya Afya:Kutoka Alma-Ata, kuelekea chanjo ya afya duniani na Malengo ya Maendeleo Endelevu,uliofanyika Oktoba 2018.

Askofu Mkuu anasema kwamba uwakilishi wake unapongeza na kuwa na shauku kubwa ya wito,uliotolewa katika Azimio la huko Astana,kwa ajili ya kupyaisha huduma msingi za afya ambazo katika miongo minne iliyopita,imesisitizwa kwa haraka sana na Azimio la Alma-Ata. Aidha  amesema kuwa Vatican inathibitisha wito wa kuhamasisha wadau wote ili kuchukua hatua ya kujenga huduma za afya msingi katika  kuhudumia ili kufikia chanjo ya afya ya wote.

Tangu mchango uliotolewa na Bodi ya Utendaji mwaka wa 2018, Mashirika Katoliki kwa mujibu wa  kisheria yamejikita katika kukamilisha na kuendeleza utoaji wa huduma ya vituo vya afya kama ifuatavyo: hospitali 5,287, zahanati  15,397 na makazi 15,722 kwa ajili ya wazee, watu walemavu na ambao wanaoishi na magonjwa magumu ya kudumu na ulemavu mwingine katika kila kona ya dunia. Sehemu kubwa ya mpango wa vituo vya afya vinavyopatikana, pia vinaungansiha na kuwa kitovu kwa akili ya watu wote wenye kuhitaji lakini pia kwa namna ya pekee kwa wale wote ambao ni masikini zaidi na walio pembezoni mwa jamii.

Vituo hivi vinatoa huduma kwa njia ya utambuzi kwamba,maisha ya binadamu ni matakatifu,tangu kutungwa kwa mimba hadi kifo chake cha kawaida, kwa ngazi ya jumuiya hadi ustawi wa wote. Kama ilivyo kwa mujibu wa Ripoti  Mkurugeniz Mkuu kuhusiana na  mada hiyo ili kuweza  kufikia maisha mazuri na ustawi kwa miaka yote. Hatimaye Askofu Mkuu amehitimisha akiunga mkono maneno ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi akiunganisha na maneno ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Siku ya Afya duniani mwaka 2018, ni haki kwa wote kupata huduma ya afya kwa njia ya kukuza thamani ya haki na mafao ya pamoja,wakati huo huo ni wema wa wote hasa kwa kila mtu.

28 January 2019, 15:16