Tafuta

Askofu Mkuu Auza Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa New York Askofu Mkuu Auza Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa New York 

Askofu Mkuu Auza:Jitihada za Vatican kuhusu mazungumzo ya Israeli na Palestina!

Askofu Mkuu wa Bernadito Auza Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa New York Marekani, wakati wa hotuba yake kwenye kikao cha majadiliano kuhusu masuala ya ya Israeli na Palestina, amekazia umuhimu wa Jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha usimamizi wa maeneo matakatifu

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu majadiliano ya hali halisi ya nchi za Mashariki, ikiwemo hata masuala ya Palestina kilichofanyika mjini New York Marekani tarehe 22 Januari 2019, Askofu Mkuu Bernardito Auza, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za umoja wa Mataifa ameanza hotuba yake akimshukuru Rais wa Jamhuri ya watu wa Domenican kwa utangulizi wa hotuba yake ya kufungua majadiliano kuhusu hali halisi ya Nchi za Mashariki kwa namna ya pekee nchi ya Israeli na Palestina.

Akitazama Ujumbe wa Siku ya Amani Duniani kwa mwaka 2019, ambao umeongozwa na mada ya siasa safi huduma ya Amani, Askofu Mkuu Auza anasema Baba Mtakatifu Francisko analinganisha Amani  kama maua mazuri, lakini yanayosumbuliwa na upepo wa nguvu chini ya ardhi. Picha hiyo inaelezea wazi hali halisi ya kudumu kati ya nchi ya Israeli na Palestina,ambako inajulikana kwa jinsi gani amani imekuwa suala tete sana na ambayo kwa kudumu muda mrefu inaathiri na uharibifu mbaya, uchochezi na mashambulizi, ukiukwaji wa haki za binadamu na vitendo vingine vinavyoathiri jitihada, pia mateso yasiyosemekana, ambayo yamesababisha vifo vya raia wasiokuwa na hatia na wala wasioweza kujikinga.

Kwa mantiki hii, Vatican inaendelea kutoa wito kwa viongozi wa nchi zote mbili  ya Israeli na Palestina ili kufungua mazungumzo na kuanza kwa upya safari ya amani ambayo inaweza kuleta mwafaka wa kusitisha migogoro iliyodumu kwa miaka katika ardhi hiyo na ambayo siyo nyumba ya watu hao tu, bali hata ni historia kubwa ya utamaduni muhimu kwa dunia nzima na nyumba ya tasaufi ya dini zote tatu zinazomkiri Mungu mmoja yaani wayahudi, Wakristo na waislam. Kwa kutoa shukrani za dini hizi zenye maana yake, Vatican inaomba kuwepo na usimamizi wa uhakika kutika jumuia ya kimataifa kwa ajili ya mji Mtakatifu wa Yerusalem ambao ulikabidhiwa na Mkutano mkuu wa 181 kunako mwaka 1947. Pamoja na umuhimu msingi wa mahali patakatifu, kuna hatari ya kubadili maana ya maeneo hayo kuweka katika mgogoro wakisiasa  na kuwa moja ya kile kinacho husu dini na utambulisho. Askofu Mkuu Auza anasisitiza kwamba hali hii lazima iepukwe ili isije kuhusishwa zaidi katika utafutaji wa suluhisho la kisiasa linalohitajika, kwa maana hiyo bado inabaki umuhimu kwa wale ambao wanasimamia ofisi za kisiasa ili watumie mamlaka yao kwa namna ya kuwajibika kuweza kushinda migogoro na kushiriki katika mazungumzo yaliyo wazi, ya haki ili hatimaye kuweza kupatikana amani halisiya kudumu!

Katika Ujumbe Urbi et Orbi wa Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Kilele cha Siku ya Amani dunia tarehe 1 Januari 2019 na pia ujumbe wa tarehe 25 Desemba 2018 alisisitiza kwamba, ili kuwepo na Amani ya kweli inapaswa pawepo na uwiano kati ya nguvu na hofu. Lakini Amani ya kweli na ya kudumu kwa upande mwingine ni tunda la mipango ya kisiasa inayotokana na uwajibikaji, pia mwingiliano wa mwanadamu;moja huenda juu zaidi ya matatizo ambayo yanaonesha kwa wakati huu hasa wa kuwa na mchanganyiko wa mizizi ya kutokuamiana, kuwa na hofu za wengine au wageni na wasiwasi juu ya usalama wa mtu binafsi. Na kwa upande mwingine Baba Mtakatifu anathibitisha kuwa, mpango wa kisiasa kwa wenye jukumu haujali jitihada za kulinda maisha ya wananchi wote, bila kujali asili au ushirikiano wa dini na kuunda masharti muhimu kwa ajili ya baadaye hasa haki kwa ajili ya wote.

Aidha Baba Mtakatifu Francisko anasema katika suala hili, ni muhimu kutopoteza hali halisi ya kibinadamu huko Gaza na maeneo mengine yaliyovamiwa, pamoja na kuonyesha jibu la ukarimu wa jumuiya ya kimataifa kwa upande wa kuwa na upungufu wa kifedha ambao wanakabiliwa nao Shirika la Usaidizi na Kazi la Umoja wa Mataifa kwa upande wa wakimbizi wa kipalestina (UNRWA) mwaka 2018. Msaada kwa wale wanao hitaji ni lazima kwenda mbele daima zaidi ya masuala ya kisiasa na misaada kwa  ajili ya wakimbizi wa Palestina;  pia wanapaswa kuruhusiwa kuendelea na maisha yao kwa kuzingatia hali halisi ambayo bado inabaki kwa muda mrefu bila kupata suluhisho. Askofu Mkuu Auza ameongeza kusema,kwa kutaja matatizo makubwa ya kibinadamu yanayoathiri sehemu kadhaa za Mashariki ni mwafaka katika jukwaa hilo kurudia ujumbe wa maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyotoa akizingatia makaribisho na ukarimu, ambao umetolewa, hiyo  si kutokana na kile kinachozidi, lakini alisema kuwa ni sadaka za wazalendo wa Lebanon na Yordan kwa ajili ya kupunguza mateso ya wanaoathirika na migogoro katika kanda, ikiwa ni pamoja na wakimbizi wa Palestina.

Akihitimisha hotuba yake Askofu Mkuu Auza pia amethibitisha kwamba, katika Mkutano wa  hivi karibuni kwa viongozi wa kidiplomasia wakati wa tukio la kiutamaduni wa kubadilishana za salamu za Mwaka Mpya, Baba Mtakatifu Francisko ameonesha matumaini kwamba, majadiliano kati ya Waisraeli na Wapalestina yanawezekana, ili makubaliano ya mwisho yaweze kufikiwa na kutolewa majibu yanayotoa matarajio halali ya watu wote kwa kuhakikishia uwiano wa Mataifa mawili, ambayo yamesubiri kwa muda mrefu na kutamaniwa amani. Uwajibikaji wa pamoja  katika sehemu ya jumuiya ya kimataifa ni muhimu sana na lazima kufikia lengo hilo, kama vile kuhamasisha amani katika kanda nzima. Ni matashi ya Askofu Mkuu Auza kuwa Baraza la Usalama katika ufunguzi wa majadiliano hayo unaweza kuchangia kifikia lengo la kudumu la makubaliano na mwafaka wa masuala ya wapelestina.

23 January 2019, 13:59