Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amemteua Askofu Henry Aruna kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Kenema lililoko nchini Sierra Leone. Papa Francisko amemteua Askofu Henry Aruna kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Kenema lililoko nchini Sierra Leone.  (Vatican Media)

Askofu Henry Aruna ateuliwa kuwa Askofu wa Kenema, Sierra Leone

Askofu Aruna alipadrishwa tarehe 16 Aprili, 1993. Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI tarehe 7 Januari 2012 akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Makeni, Sierra Leone na kuwekwa wakfu tarehe 5 Januari 2013 na Askofu mkuu Protase Rugambwa. Tarehe 18 Julai 2015 akateuliwa na Papa Francisko kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Kenema.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Henry Aruna kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Kenema nchini Sierra Leone. Hadi kuteuliwa kwake, alikuwa ni Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki Kenema. Itakumbukwa kwamba, Askofu Henry Aruna alizaliwa kunako tarehe 2 Agosti, 1964, huko Yemandu, Jimboni Kenema. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi katika falsafa na taalimungu, akapadrishwa tarehe 16 Aprili, 1993 kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Kenema, nchini Sierra Leone.

Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI tarehe 7 Januari 2012 akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Makeni, Sierra Leone na kuwekwa wakfu tarehe 5 Januari 2013 na Askofu mkuu Protase Rugambwa. Tarehe 18 Julai 2015 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Kenema. Katika maisha na utume wake wa Kipadre amewahi kushika nafasi mbali mbali za uongozi kama Paroko Msaidizi, Jaalimu, Dekano na mchumi wa Seminari kuu ya Mtakatifu Paulo iliyoko mjini Freetown. Aliwahi pia kuwa ni Katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Sierra Leone na Mkurugenzi mkuu wa Mashirika ya Kipapa nchini Sierra Leone.

26 January 2019, 15:19