Tafuta

Vatican News
Watu wa asili wa Amazon walipokutana na Papa huko Puerto Maldonado mwaka 2018 Watu wa asili wa Amazon walipokutana na Papa huko Puerto Maldonado mwaka 2018  (Vatican Media)

Harakati za Papa Francisko katika utetezi wa utamaduni wa watu asilia!

Mwaka 2019 ni mwaka wa kimataifa wa lugha za asili msingi kwa ajili ya haki za binadamu, amani na maendeleo endelevu. Kwa mujibu wa Wosia wa Laudato Si wa Baba Mtakatifu Francisko, unasema kupotea kwa utamaduni ni hatari kubwa kama vile hata kupotea kwa aina za wanyama na mimea

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mwaka 2019 ni mwaka wa kimataifa wa lugha za asili, msingi kwa ajili ya haki za binadamu, amani na maendeleo endelevu. Kwa mujibu wa Wosia wa "Laudato Si" wa Baba Mtakatifu Francisko, unasema kupotea kwa utamaduni ni hatari kubwa kama ili pia hata kupotea kwa aina za wanyama na mimea.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa mwaka 2019 ni mwaka wa kimataifa wa Lugha za Asili kwa sababu, Lugha ni msingi kwa mantiki ya kulinda hali za binadamu, kujenga amani na mandeleo endelevu, kwa kuhakikisha utamaduni na  mazungumza ya utamaduni yanakuwapo japokuwa na utafauti wake. Licha ya hayo kunzia thamani yake ya kina katika dunia nzima, lugha inaendelea kupoteza msimamo wake kwa kasi kwa sababu ya mantiki tofauti. Na sehemu kubwa ya lugha za watu ni wale wa asili.  Kwa vyovyote, lugha za asili,  ni kama chanzo cha mawazo na mtazamo wa binadamu,na ambapo huathirika sana hasa kwa upande wa  kupata elimu ya juu katika lugha ya kitaifa au kimataifa na msingi wowte ule ni kuanzia elimu ya msingi katika lugha ya asili.

Papa anasema tuokoe utamaduni wa watu kama ilivyo hata viumbe wengine

Katika waraka wa Laudato Si ulioandikwa mwaka 2015, kwaajili ya kulinda mazingira, Kipengele cha 145, Baba Mtakatifu Francisko anaelezea kuwa kupotea kwa utamaduni unawezekana kuwa mkubwa kama vile kupungua kwa aina  ya wanyama au mimea. Katika kipengele kinachofuata, katika  maana hiyo anasisitiza kuwa ni muhimu kuwa makini hasa kwa upande wa jumuiya za asili na tamaduni zao.

Mkutano wa watu wa asili huko Amazoni mwaka 2018 nchini Peru

Maneno ya Baba Mtakatifu yanayokumbukwa huko Puerto Maldonado nchini Peru, tarehe 19 Janauri 2018 katika mkutano wa watu wa asili wa Amazoni, uliofunguliwa na ushuhuda wa familia moja ya kiasili na mkutano huo ulikuwa umezungukwa na makabila ya watu mbalimbali wa asili wa Harakbut na Wampis. Baba Mtakatifu alisema:“sisi tunataka watoto wetu wasome, lakini wanataka shule zifute utamaduni wetu, lugha zetu, lakini sisi hatutaki kusahau hekima ya mababu zetu. Baba Mtakatifu akisisitizia na maelezo hayo alisema njia moja ya kutunza utamaduni usipoteee ni kuendeleza lugha bila kusita.

 Baba Mtakatifu anawashauri maaskofu wahamasishe elimu ya utamaduni na lugha zaidi ya moja

Katika hotuba hiyo, Baba Mtakatifu aliwaomba Maaskofu wa Amazon na ambao mwezi Okotba 2019 watakuwa na Sinodi yao ya kwanza inayohusu Bara la Amerika, kwamba, “Ninawaomba kama jinsi ambavyo mnaendelea kufanya hata katika maeneo ambayo yako pembezoni,na ili wahamasishe nafasi za elimu na utamaduni, kujifunza lugha zaidi ya mbili shuleni na katika taasisi za mafunzo na vyuo vikuu. Hata hivyo anawapongeza kwa shuguli zilizoanzishwa na Kanisa la Peru kuhusu Amazon kwa ajili ya kuhamaisha watu wa asili. Alitaja vyama na mashirika mbambali yanayojikita katika shule hizo.

Umoja wa Mataifa wanasema lugha za asili zinapotea

Wajibu maalum katika mwaka 2019 kwa ajili ya Umoja wa Mataifa ni ile ya kujikita kukuza luga za asili  na ambazo ndiyo sehemu kubwa ya watu kwa zaidi ya lugha 6700 zinazozungumzwa duniani kote na kama urithi mkubwana ambao unapaswa kulindwa hali na ustawi wa wale ambao wanafanya indelee kuwa hai , yaani watu wa asili.

Hata hivyo kwa mujibu wa Shirika la Umoaj wa Mataifa la Elimu Sayansi na utamaduni (UNESCO), lugha za asili ni utambulisho wa makabila mbalimbali ya dunia na hazina muhimu kubwa katika maisha ya jamii. Tayari mwaka 1994 Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa ulitangaza tarehe 9 Agosti kuwa Siku ya watu wa Asili Duniani kwa lengo la kuadhimisha utofauti wao na kuwasha mwanga zaid juu ya ukiukwaji na ukosefu wa haki ambao unazidi kuwakumba kwa karne nyingi za ukoloni na mauaji.

Lugha zinazozungumzwa na watu milioni 570  wengi wao ni maskini

Kwa dhati ni  asilimia 5 ya watu wote duniani, ambapo milioni 570 ya watu waliogawanyika kati ya watu elfu tano walioko katika nchi 90  dunaini, lakini asilimia 15 ya watu hao ni masikini. Hawa ni kati ya watu waliothirika  na ambao hawana ulinzi duniani. Kutokana na hiyo, hata mwaka 2017, Umoja wa Mataifa iliweka mkataba wa haki ya watu wa asili, mkataba unaotaka kwa dhati kuweka ulinzi  na kupinga kila aina ya ubaguzi dhidi yao, kwa namna ya pekee katika mazoezi ya hutumiaji wa kujieleza kama utambulisho wao.

Hatari zinazoashiria mwaka 2100 ni  kati ya lugha asilimia 50 na 90

Lugha tunayozungumza ndiyo inajieleza jinnsi tulivyo na kwa namna tunavyoka kuhusiana na dunia. Inakadiriwa kuongezeka kwa idadi kubwa ya watu wanaoongea lugha inayotawala kama kingereza, kichina na kispanyola, kulinganisha na lugha ambazo hazijulikani kufikia karne hii, kupotea lugha duniani kati ya asilimia 50 na 90.

03 January 2019, 16:58