Vatican News
Mkutano uliofanyika tarehe 19 Desemba 2018, huko Hanoi, ulikuwa ni Mkutano wa saba wa Kikundi cha kazi kishirikishi kati ya Vietnam na Vatican Mkutano uliofanyika tarehe 19 Desemba 2018, huko Hanoi, ulikuwa ni Mkutano wa saba wa Kikundi cha kazi kishirikishi kati ya Vietnam na Vatican  (Vatican Media)

Vietnam na Vatican wamefikia makubaliano katika mkutano wa saba!

Sehemu zote mbili wamejadiliana na kufikia makubaliana juu ya masuala yanayotazama wakati ujao kwa ngazi ya mahusiano kati ya Vietnam na Vatican. Hii ni suala linahusu kutoka uwakilishi wa Vatican usio wa kudumu kufikia uwakilishi wa kudumu wa Vatican

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mkutano uliofanyika tarehe 19 Desemba 2018, huko Hanoi, ulikuwa ni Mkutano wa saba wa Kikundi cha kazi kishirikishi kati ya Vietnam na Vatican, ulioudhuriwa na viongozi kwa pamoja na Makamu waziri wa kudumu wa Mahusiano na nchi za Nje na Mwakilishi wa Vietnam, Bui Thanh Son, Askofu  Antoine Camilleri Katibu Msaidizi wa Mahusiano na nchi za nje na ambaye alikuwa ni mkuu wa msafara wa wajumbe wawakilishi  Vatican. Mkutano huo ulifanyika katika hali ya kindugu na heshima kwa wote, kwa mujibu wa vyombo vya habari Vatican.

Mandeleo chanya katika mahusiano ya nchi zote mbili

Katika mkutano wao, sehemu zote mbili zimepata nafasi kubwa na kamili ya kushirikishana kwa karibu juu ya mahusiano ya Vietnam na Vatican  kwa kuunganisha masuala yanayotazama Kanisa Katoliki nchini Vietnam. Sehemu zote mbili wameezea kutambua kuwa mahusiano ya Vietnam na Vatican yameweza kupata maendeleo chanya ya hivi karibuni, kwa namna ya pekee katika kudumisha mawasiliano mara kwa mara na mashauriano katika ngazi zote, ikiwa ni pamoja na mikutano ya ngazi ya juu na kubadilishana maoni wakati wa mikutano ya Kundi la Kazi la Pamoja kati ya Vietnam na Vatican, ziara za kichungaji nchini Vietnam na mawakilishi wa kipapa asiyekuwa na makao, Askofu Mkuu Marek Zalewski.

Mazungumzo na imani

Katika Mkutano huo aidha pande zote mbili wamekubaliana kuwa mahusiano kati ya Vietnam na Vatican yanapaswa kuendelea kudumishwa kwa misingi ya kanuni za pamoja zinazoshirikishana pamoja na majadiliano mazuri, kwa lengo la kujenga mahusiano ya uaminifu na kuimarisha mahusiano kwa ajili ya faida ya sehemu zote mbili za Jumuiya Katoliki ya Vietnam.

Mkataba wa uwakilishi wa kudumu wa Vatican

Wakiendelea na mkutano huo pande zote mbili zilijadiliana na kufikia makubaliano juu ya masuala muhimu ya kukuza wakati endelevu kwa kiwango cha mahusiano kati ya Vietnam na Vatican  kwa kutoka  mwakilishi hasiye wa kudumu na kuwa na  mwakilishi wa kudumu  na walishirikishana hayo wakiwa na uhakika kwamba hatua hiyo inaweza kusaidia kuendeleza na kukuza  kwa kina mahusiano kati ya sehemu zote mbili.

Kukubaliana na ujumbe wa Papa

Kadhalika sehemu zote mbili wamesema kuwa ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa Jumuiya Katoliki ya Vietnam kuhusu “kuiishi Injili katika moyo wa Taifa” na mkatoliki mwema ni kama mzalendo mwema” ambapo  ni msingi muhimu kwa ajili ya maisha ya jumuiya. Vatican imeonesha kupendezwa na pia kutoa shukrani kwa upande wa Vietnam kwa ajili ya kuwa na  umakini ambao viongozi wakuu wa serikali ya Vietnam wanatoa kwa Kanisa Katoliki la Vietnam kwa miaka ya hivi karibuni. Pia wameonesha kuwa Vatican inafuatilia kwa umakini, mwenendo wa maisha ya jumuiya katoliki nchini humo na kuwatia moyo Kanisa Katoliki la Vietnam ili kuchangia kwa ajili ya wema wa pamoja na maendeleo mema ya nchi kwa ujumla

Shughuli za Chama na Serikali ya Vietinam

Kwa upande wa Vietnam imesema kuwa, Chama na Serikali ya  Kivietinam wanajitahidi kutekeleza kwa kikamilifu mfumo wa kisiasa ili kuheshimu na kuhakikisha uhuru wa dini na imani ya watu; kuwatia moyo na kuwezesha jumuiya ya katoliki, katika kufanya kazi kwa kufuata sheria za Kivietinam, na kushiriki kikamilifu katika maendeleo  na kujenga uchumi katika kijamii ya kitaifa.

Majadiliano juu ya jimbo na uteuzi wa maaskofu

Pande zote mbili pia zilijadili masuala yanayohusiana na mgawanyiko wa Majimbo na uteuzi wa Maaskofu huko Vietnam. Kadhalika sehemu zote mbili   pia zilikubaliana kufanya Mkutano wa nane wa Kundi la Kazi la Pamoja kati ya Vietnam na Vatican mjini Roma. Lakini tarehe ya mkutano itapangwa kwa njia ya mikondo ya  kidiplomasia. Katika fursa hiyo ya mktano , ujumbe wa Vatican pia uipata kutembelea Waziri Mkuu Nguyen Xuan Phuc na Rais wa Kamati ya Serikali ya Mambo ya Kidini, Vu Chien Thang. Kadhalika Wajumbe pia waliudhuria sherehere za kusimikwa rasmi Askofu Mkuu Joseph Vu Van Thien wa Jimbo Kuu la Hanoi.

 

 

 

 

 

 

20 December 2018, 16:02