Tafuta

Vatican News
Msemaji mkuu wa mpito wa  vyombo vya habari Vatican Bwana  Alessandro Gisotti Msemaji mkuu wa mpito wa vyombo vya habari Vatican Bwana Alessandro Gisotti 

Dk.Gisotti ateuliwa kuwa Msemaji mkuu wa muda wa Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amekubali maombi ya kung’atuka kwa wasemaji wakuu wa Vatican na badala yao ameridhia uteuzi wa Dk.Alessandro Gisotti kuwa msemaji mkuu wa Vatican katika kipindi hiki cha mpito!

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amekubali maombi ya kung’atuka kwa Msemaji mkuu na Makamu wake wa vyombo vya habari Vatican, Dk. Greg Burke na Dk. Paloma García Ovejero na kumteua Msemaji Mkuu wa muda wa Vyombo vya habari Dk. Alessandro Gisotti ambaye hadi uteuzi wake alikuwa ni mratibu wa Mtandoa wa kijamii wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

Bwana Alessandro Gisotti, alizaliwa mjini Roma  miaka 44 iliyopitia na mwenye familia ya watoto wawili. Majiundo yake katika Chuo Kikuu La Sapienza Roma na kujipatia shahada ya Sayansi ya Siasa na tangu mwaka 1999 ni mwandishi wa habari kitaaluma aliyojinyakulia kwa  shahada ya uandishi wa habari katika Taasisi ya Uandishi wa Habari ya Wajesuit  Chuo Kikuu cha Laterano Roma. Mara baada ya uzoefu wa ofisi ya Habari za Umoja wa Mataifa mjini Roma alianza kufanya kazi katika idhaa ya  Matangazo ya  Radio Vatican kunako mwaka 2000.

Tangu 2011 hadi 2016 amekuwa Makamu mratibu wa matangazo ya  Radio Vatican. Amefuatilia shughuli hizi kwa kwa kipindi cha Mapapa watatu wa Roma na katika ziara mbalimbali za kimataifa na nchini Italia. Tangu mwaka 2017 ni mtaribu wa Mtandao wa Kijamii wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican. Ameandika habari nyingi zinazohusu habari za Kanisa kwa namna ya pekee hata kitabu kiitwacho “Maneno kumi ya mhubiri mwema kwa mujibu wa Papa Francisko”, kikiwa na utangulizi Kardinali Luis Antonio Tagle kilichotolewa mwaka 2016.

Kufuatia na kung’atuka kwa Bwana Greg Burke na makamu wake Paloma García Ovejero na kuchanguliwa kwa msemaji mkuu wa muda, naye  Bwana Paulo Ruffini, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano anasema kuwa  amekubali uamuzi wa  Bwana Greg Burke na Paloma García Ovejero pia na Baba Mtakatifu kupokea maombi yao  ya kujiuzuru kwao. Kwa miezi michache ambayo wameweze kufanya kazi pamoja, anawapongeza kwa juhudi zao za kitaaluma, kibinadamu na imani yao. Anawashukuru sana kwa kazi waliyotenda kufikia leo hii. Leo hii mbele ya maamuzi yao  kwa uhuru,  Bwana Ruffini anathibitisha kuwa hawezi kwenda kinyuma na maamuzi waliyo fanya. Shughuli hiyo ambayo Bwana Greg na Paloma, walipewa na kuelekezwa  na monsinyo  Edoardo Vigano aliye kuwa mkurugenzi wa kwanza na baadaye makamu  baada ya mageuzi ya mfumo mpya wa mawasiliano ya Vatican kwa maamuzi ya Baba Mtakatifu .

Shughuli yao yenye maana imetoa mchango mkubwa katika safari ya mageuzi ambapo kwa mijibu wao wenyewe wanasema kwamba, ili uweze kufikia ukamilifu, unahitaji hatua za haraka za usuhuda, roho ya huduma kwa Kanisa na kila mantiki inayoizunguka. Kwa hakika katika roho hiyo ya huduma na uaminifu kwa Baba Mtakatifu, Bwana Paolo Ruffini aanathibitisha ataipeleka mbele katika hali hiyo nyeti ya safari muhimu ya mchakato wa mageuzi. Mwaka unaofunguliwa mbele, Bwana Ruffini anathibitisha,ni mzito wenye kujaa  matukio muhimu ambayo yanahitaji nguvu kubwa ya mawasiliano. Ni matumaini ya kwamba Bwana Alessandro Gisott, pamoja na kuwa mratibu wa Mtandao wa kijamii wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, alikuwa tayari ni Makamu mratibu wa Matangazo ya Radio Vatican na ambaye atatambua namna ya kuongoza ndani ya kuwa msemaji mkuu wa Vyombo vya habari wakati wa kusubiri  muundo mpya utakaofanyika kwa haraka iwezekanavyo!

Shukrani za Bwana Alessandro Gisotti: Ninamshukuru Baba Mtakatifu kuwa na imani ya kuniaminisha katika kipindi hiki nyetu kwa ajili ya mawasiliano ya Vaticvan. Niko tayari kushirikiana na Rais wa Baraza la Mawasiliano Bwana Paolo Ruffini. Ndiyo meneno aliyothibitisha mara baada ya kuteuliwa kwake Bwana Alessandro kuwa Mkurugenzi wa ndani wa Mawasiliano Vatican. Aidha anawashukuru Bwana Greg Burke na Bi Paloma G. Ovejero, kwa uhusiano wao na urafiki. Anaungana na Rais kuwashukuru sana kwa kazi walizozifanya kwa kipindi cha miaka miwili na nusu kujikita katika uongozi wa kuwa wasemaji wakuu wa vyombo vya habari Vatican.

Anaahidi kujikita kwa dhati kwa shuguli yaliyo kabidhiwa kwa kadiri ya uwezo wake, katika roho ya huduma kwa Kanisa,na kwa Baba Mtakatifu ambaye amekuwa na fursa ya kujifunza kutoka kwake akiwa karibu na Padre Federico Lombardi kwa karibu ya miaka 20.Aidha anathibtisha jinsi anavyotambua vema wajibu aliopewa wa ndani na kwa namna ya pekee unawajibisha sana, lakini kwa utambuzi wa thamani ya wafanyakazi wote wa  chombo hiki anatiwa moyo kutokana na fursa nyingi anazoponeza katika taaluma na kujitoa binafsi.

31 December 2018, 13:46