Cerca

Vatican News
Kardinali Joao Bráz de Aviz ameshiriki Jibilei ya dhahabu ya Chama cha Muungano wa Mama wakuu wa mashirika (ARU) nchini Uganda Kardinali Joao Bráz de Aviz ameshiriki Jibilei ya dhahabu ya Chama cha Muungano wa Mama wakuu wa mashirika (ARU) nchini Uganda 

Uganda:Jubilei ya dhahabu ya Muungano wa mashirika ya kitawa!

Kardinali Joao Bráz de Aviz ambaye ni Rais wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume amewahimiza watawa wawe divai mpya katika huduma. Amesema hayo wakati wa Mahubiri yake katika kilele cha Jubilei ya Dhahabu ya Chama cha Mama Wakuu wa Mashirika ya watawa ya kike (ARU) Uganda. Misa iliudhuriwa na maaskofu 20 na watawa wote kutoka majimbo 19

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kardinali João Bráz de Aviz, amewahimiza watawa nchini Uganda kufuata mwaliko wa Baba Mtakatifu Francisko kwa watu waliojiweka wakfu ili kuimarisha Maisha yao katikawakfu. Baba Mtakatifu alisema maisha ya wakfu ni hazina katika Kanisa, lakini wakati huo huo, Papa  pia anawaalika kuimarisha kwa kina  maisha  ya kitawa.  Kardinali Joao Bráz de Aviz ambaye ni Rais wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na kazi za Kitume, amesema hayo wakati wa Mahubiri yake katika Jubilei ya Dhahabu ya Umoja wa Mama Wakuu wa Mashirika ya watawa ya kike (ARU) nchini Uganda. Kardinali amekwenda huko kutokana na mwaliko wa Shirikisho la Watawa nchini Uganda.

Divai mpya katika viriba vipya

Kardinali amejikita katika  mahubiri yake kwa kuongozwa na masomo ambayo yalikuwa yanatoka katika Kitabu cha Nabii Isaya 63,7-9, somo likiwa linakumbusha kumshukuru Mungu kwa fadhila yake ya upendo na upendo wa  kila mmoja wakati huo huo, somo la pili lilikuwa linatoka Barua kwa  Wafilipi 2,1-14 ambalo  likiwa linakumbusha kwamba, jambo muhimu zaidi ya yote ni kuweka upendo kati yetu  na Injili kutoka Mtakatifu Yohane 15,9-14 ilikuwa likifafanua kwamba, anayependa sana ndiye anayetimiza amri za Mungu. Kardinali akiendelea na mahubiri yake anasema: Baba Mtakatifu anakumbusha kuwa divai mpya ya Yesu Kristo, lazima iwekwe katika divai mpya ya ngozi. Je ni wakina nani wenye  ngozi mpya ya divai? Kardinali ameuliza. Ili kujibu swali hili ametazama  mantiki nne msingi za maisha ya kitawa na ambazo amezitaja kuwa, mafunzo na  madaraka, utii na uhusiano kati ya wanaume na wanawake na fedha, amefafanua kuwa ndivyo divai mpya inayotakiwa kupyaishwa!

Kwa mujibu wa Kardinali, De Aviz anasema, kwanza divai ya ngozi ni mafunzo, ambayo lazima yazingatiwa kwa dhati. Ni lazima kuwa na mafunnzo ya kimaadili ya Yesu na karama ya kila mwanzilishi wa shirika na kusisitiza zaidi kwamba  huo ndiyo msingi wa kwanza. Amelinganisha mafunzo hayo  katika kazi, kama mfinyanzi na kueleza kuwa, moja ya fadhila muhimu ya mtu ambaye amefundishwa vizuri anaonesha kuwa na upole. Ni mfinyanzi ambaye ana uwezo wa kukipatia chungu umbo ambalo anataka mwenyewe anayefinyanga. Mtu anayejiruhusu mwenyewe kufundwa huwezekana hata kuundwa kwa mtindo wa ambao ni kama Yesu mwenyewe alivyoutoa na kwa njia hii, mtu hujiunda  mwenyewe au  kwa njia ya mwanzilishi. Kama watawa amesema kuwa ni muhimu sana kwao kujifungua katika malezi, na ambayo lazima yafanywe na jumuiya nzima ya watu walio tiwa wakfu. Jambo muhimu zaidi, amesisitizia pia  juu ya walimu wa mafunzo kwa watawa na kwamba wao wanapaswa kuwasimulia juu ya uzoefu wao kama walimu kwa wale wanao wafunda.

Kuna haja ya kufuata njia aliyoiishi Yesu

Pili, Kardinali amesema kuna haja ya kuchunguza mamlaka na utii kwa sababu Yesu ametufundisha jambo muhimu sana. Kwa upande wa Yesu,  mamlaka  si kuwa na nguvu na wala kutawala, lakini badala ya yake ni kuhudumia. Amenukuu mafundisho ya Yesu na kusema kuwa, “ikiwa unataka kuwa wa kwanza, lazima uwe wa mwisho”, kwa sababu unaitwa kupenda daima. Kwa namna hiyo amethibitsha kuwa, kuna haja ya sisi kujiuliza jinsi gani tunavyoweza kuishi kwa kufuata njia ambayo Yesu aliishi! Akiendelea na ufafanuzi huo Kardinali alikumbusha kuwa,  wakati wa mateso  na kifo chake, Yesu alilia kwa Baba yake kwa namna alivyo kuwa akiteseka pamoja na kwamba alikuwa bado anamtii. Na hivyo:“Nasi tunapaswa kufanya hivyo”, na kusisitiza kardinali kuwa: “Lazima tuwaambie wakuu wetu matatizo yetu na vitu ambavyo vinatuhusu sisi”. Kardinali amesisistiza kuwa ni muhimu kwao kuwaambia matatizo yao wakuu wao na wasiogope kuzungumza tangu Roho Mtakatifu anapotaka kusema kupitia kwao na kwamba hii itawasaidia kufanya maamuzi mazuri kuhusu wao wenyewe. Hata hivyo Kardinali ameonya kuwa wanapaswa kuwa na mizizi iliyosimika kwa Mungu wakati wanapotaka kusema mambo hayo yanayowahusu na mwengine.  Zaidi ya hayo, amesisitiza, kwamba haipaswi kuwepo hali ya ukuu na  wengine wa chini kwa kuwa katika Yesu ni kuishi kindugu na ndiyo njia ya kuishi kama Wakristo.

Mantiki ya tatu ni uhusiano kati yao

Mantiki ya tatu ambayo amefafanua amesema watawa wanahitajika kuzingatia kuhusiana na maisha yao yaliyowekwa wakfu katika uhusiano kati ya wanaume na wanawake. Ni muhimu kwao  kuelimishwa  kuhusu uhusiano wao  na ujinsia wa kuishi maisha yaliyo wekwa wakafu na utakatifu ambao pia unahusu hata wanandoa  katika kuishi usafi na useja. Mungu alituumba sisi wanaume na wanawake wenye hadhi sawa. Mwanamke sio muhimu kuliko mwanaume, hivyo mwanamke lazima awe sawa na mwanaume. Kwa kuzingatia mafundisho ya Mtakatifu Paulo juu uhusiano kati ya Yesu na Mwili wa Kanisa,  kama vile Yesu alivyo kichwa cha Kanisa na akatoa maisha kwa Kanisa zima.

Suala la fedha

Kardinali pia amezungumzia kuhusu fedha kwa watawa kwamba:  Hatuwezi kumtumikia Mungu na fedha na kwa maana hiyo, tunapaswa kumtumikia Mungu wakati huo,  fedha lazima zitumike katika kutumikia Mungu. Hata hivyo kwa haraka amebainisha kuwa jambo hili ni rahisi tu kulielewa kwa mtu  ambaye anaishi umaskini huo. Lakini katikati ya watawa wote, ni lazima kuangaliana na kuthaminiana kama ndugu kaka na sada, na hiyo itaweza kuwasaidia kuishi maisha halisi ya wakfu wao.

Mitindo mbalimbali ya maisha ya watawa

Kardinali aidha amejikita kutazama siku za nyuma juu ya Barua ya Baba Mtakatifu Francisko aliyowaandikia watawa kwa  mwaka 2015, barua iliyokuwa inangazia mwaka wa Maisha ya kitawa kunako mwaka 1995, ambapo Baba Mtakatifu alikuwa anawaalika watawa kutazama “nyakati zilizopita kwa shukrani na kwamba, "nyakati zilizopita ni za Mungu na historia yetu ni muhimu sana”. Kutokana na hili, Kardinali amefafanua juu ya historia ya mitindo ya maisha ya watawa kuwa:"tangu mwanzo wa karne ya kwanza kulikuwa na wanawake waliojitakasa wenyewe katika useja wa Kanisa na lilikuwa ni shirika la mabikira. Na kati ya watawa hawa wapo wengine ambao wanatoka katika Mashirika ya kisekulari na mitindo mingine mingi yenye idadi kubwa leo hii. Wanaume na wanawake leo hii wa Mashirika ya Kisekulari wanabaki katika ulimwengu na wanajihusisha na fani mbalimbali, lakini pia wameweka wakfu kwa Mungu katika kufuata ushauri wa kiinjili wa  nadhiri ya useja. Kundi jingine la watawa Kardinali Aviz amebainisha, lilikuwa ni Wahermitis. Hawa mara nyingi wanakaa wamejitenga lakini daima wanamtafuta Mungu.

Wamonaki wanaishi katika Monasteri na watawa katika jumuiya

Makundi mawili ya watawa, Kardinali Aviz amefafauia ni Wamonaki na Mabruda na Wawawa. Wamonaki wanakaa katika Monasteri zao kwa kutumia muda mwingi katika sala na kutafakari, wakati sehemu kubwa ya wanaume na wanawake waliowekwa wakfu wanajikita katika shughuli za utume wa kazi, ambao wameweka nadhiri za kiinjili na kuishi katika jumuiya mbalimbali. Ingawa maisha ya watawa ni ya zamani kama Ukatoliki nchini Uganda, Kardinali Avis amepongeza Umoja wa mama wakuu  Watawa nchini Unganda (ARU) kwamba umoja huo unachukua sura  zaidi ya kuratibu. Akifafanua amesema ARU ilianzishwa karibia sawa na kipindi cha Mtaguso wa Pili wa Vatican, kwa maana hiyo kushirikiana na Halshauri hiyo ni ishara ya umoja kati yao wote. Aliongeza kusema ARU tayari imesaidia kuunda watu waliowekwa wakfu, ambao ni chanzo cha furaha kubwa.

Muungano wa Mama wakuu wa mashirika nchini Uganda ulianzishwa kunako mwaka 1968 ukiwa na wajumba karibia 100 wa washikirika  na jumla ya watawa 6,000 wa kike na kiume  wakihudumu nchini Uganda. Katika madhimisho ya Ekaristi Takatifu, wameshiriki maaskofu 20 na ziadi ya mapadre 40. Jubilei ya dhahabu ilifanyika katika Kanisa Kuu la Lubaga jijini Kampala na kuwashirikisha maelfu ya watawa wa kike na kiume kutoka katika majimbo yote 19 ya Uganda.

11 December 2018, 16:26