Cerca

Vatican News
Padre Marco Pozza na Noa, Achinoam Nini mwimbaji wa kutoka Israeli katika mahojiano kuhusu Salam Maria Padre Marco Pozza na Noa, Achinoam Nini mwimbaji wa kutoka Israeli katika mahojiano kuhusu Salam Maria  

Tv2000:Papa anazungumza juu ya uvumilivu na kutafakari Magnificat!

Kipindi cha kumi cha Sala Maria na Baba Mtakatifu ambacho kitakuwapo Jumanne 18 Desemba saa 3.15 usiku, masaa ya Ulaya katika Luninga ya Baraza la Maaskofu Italia (Tv2000). Katika kipindi hiki, Baba Mtakatifu Francisko anasema, anayeteseka kwa uvumilivu, anaunganisha mateso ya Mungu katika Kristo

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Anayeteseka kwa uvumilivu, anaunganisha mateso ya Mungu katika Kristo. Baba Mtakatifu Francisko anaanza namna hiyo akihojiana na Padre Marco Pozza Mtaalimungu na msimamizi wa Kanisa dogo la wafungwa huko Padova, Italia katika mwendelezo wa kipindi cha Salam Maria, (AVE MARIA) kipindi ambacho kimeandaliwa kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Tarehe 18 Desemba 2018, saa 3.15 masaa ya Ulaya, mazungumzo ya kpindi cha kumi kinajikita hasa juu ya mada ya uvumilivu na wazo ambalo linazungukia hali halisi ya maisha kama vile, wagonjwa ambao wanakubali ugonjwa, wazee walio peke yao ambao wanapokea hali halisi kwa uvumilivu, wafungwa na watu wengi wengi  ambao wanapokea na kuvumilia machungu hayo.

Matumaini au uvumilivu?

Baba Mtakatifu anasema kuwa, anapofikiria ishara za matumaini, neno moja linalomjia akilini ni lile la uvumilivu. Kujikita katika suala la uvumilivu, ni ule uwezo wa kuchukua juu ya mabega na mambo mengi ya maisha, lakini pia ni kubeba na matumanini  kwa kutazama mbele. Ni kuwa na upendo mkuu wa kuweza kuwa uvumilivu. Hasiyekuwa na pendo mkuu wa kikristo hawezi kufikia hatua ya kuwa na uvumilivu, Baba Mtakatifu anatthibitisha.

Sambamba na Maria

Baba Mtakatifu pia anasema kuwa Kanisa ni mwanamke. Wao kama makleri, ni wanaume lakini wao siyo Kanisa. Kanisa ni mwanamke na kwa sababu ni mchumba. Maria ni mwanamke ni mchumba wa Yosefu, kwa kupokea Roho Mtakatifu kwa ukamilifu na hivyo Mama wa Kristo na wa Kanisa. Hii ya mwaishoina maana ni mchumba wa Kristo. Kina uelewa wa umama katika Kanisa na ambao unatokana na umana wa Maria, upendo wa Kanisa ambaye anakuja kwa  huruma ya Maria.

Wageni

Katika kipindi ambacho kimegawanyika katika sehemu 11 na msingi wake ni Baba Mtakatifu Francisko akielezea juu ya Sala inayojulikana duniani kote, pamoja na kipindi hicho pia wameunganishwa watu wa utamaduni , sanaa na tamasha. Katika kipindi cha kumi, kitamwona  msanii mmoja ambaye ni mwimbaji wa Muziki aitwaye Noa na mwandishi wa habari Federica Angeli.

Kadhalika kufuatia na Maneno ya tafakari na majibu ya Baba Mtakatifu Francisko akiwa na Padre Marco Pozza wametengeneza Kitabu kinachoitwa “Ave Maria ya Papa Francisko, kinachopatika katika maduka ya Vitabu, Vatican na Rizzoli mjini Roma.

18 December 2018, 12:30