Mahubiri ya Majilio mjini Vatican Mahubiri ya Majilio mjini Vatican 

Tafakari ya majilio:Roho yangu inakuonea kiu!

Mungu ni Mwamba, lengo lake ni kama kuendeleza imani kwa viumbe na kuwaondolea ile hofu katika mioyo yao: ardhi ikitetemeka hatuogopi, hata milima ikiangukia chini ya bahari. Ni mwanzo wa tafakari ya Majilio ya Padre Raniero Cantalamessa

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu, mapadri, kaka na dada, tuna zoezi na tatizo la kusuluhisha, matatizo ya kukabiliana nayo, changamoto ambazo zipewe kujibu na ambazo tumo hatarini katika kupoteza ule mtazamo au kuacha ule ukina wake wa Injili kwa maana ya uhusiano wetu binafsi na Mungu. Zaidi ya hayo, tunatambua uzoefu ambao uhusiano ni wa dhati na Mungu, na  ndiyo hali halisi ya kwanza kwa ajili ya kukabiliana na hali zote, ikiwa ni katika  matatizo yote yanayojitokeza,lakini  bila kupoteza amani na uvumilivu.

Ndiyo mwanzo wa tafakari Kwanza ya Padre Raniero Cantalamessa, Mhubiri katika Makazi ya Kipapa kwa kipindi cha Majilio ambayo ametoa kwa Baba Mtakatifu Francisko na wasaidizi wake katika  Curia ya Roma, Ijumaa  tarehe 7 Desemba 2018. Padre Cantalamessa pamoja na kufafanua hayo, amependa kuachana na masuala ya mtatizo katika kipindi hiki cha Majilio na kutumia maneno ya Mtakatifu Angela wa Foligno aliyekuwa akiwashauri watoto wake wa kiroho ili kujiunda katika umoja na kuinua roho zao kwa Mungu kwamba: "ni kuongea asubuhi kwa imani kabla ya kuanza siku ya kazi”.

Walio wachache lakini wanatafuta na kusoma ishara za kuishi ambazo ziliunda ulimwengu 

Mada ya Majilio, hata ya kwaresima Mungu akipenda, Padre Cantalamesa amesem,a itakuwa ni kuhusu Zaburi: “ roho yangu inakuonea kiu ya Mungu aliye hai (Zab 42,2) . Watu wa nyakati zetu wanakimbilia kutafuta ishara za maisha ya kuishi na ufahamu juu ya sayari. Ni utafiti halali na unaoeleweka hata kama hauna uhakika. Walio wachache lakini wanatafuta na kusoma ishara za kuishi ambazo ziliunda ulimwengu  na ndipo inaingia hatari yake, ambayo mwanadamu anaishi hata leo hii. "Ndani yake Yeye  tunaiishi na tunajimudu na tuko"! ( Mdo 17, 28 ) lakini hatutambui. Anayeishi yupo kati yetu lakini tunamwacha ili kutafuta viumbe vingine vya kufikirika na ambayo haviwezi kutenda katu kilicho cha msingi katika maisha yetu na kutokoa dhidi ya mauti.

Padre Cantalamessa anauliza: Ni mara ngapi tunalazimika kuzungumza na Mungu kwa kutumia maneno ya Mtakatifu Agostino:"wewe ulikuwa nami , lakini mimi sikuwa nawe".  Lakini kinyume chake, Mungu aliye hai  anatufatufa na hafanyi lolote zaidi ya kuendelea kuumba ulimwengu. Mumgu anaendelea kuuliza:"Adamu huko wapi"? (Mw 3,9) Sisi tunapendelea kukwepa ishara hiyo ya Mungu, aliye hai kujibu wito wake wakati akibisha hodi ili aingie katika mawasiliano mapya na kuishi naye, anathibitisha Padre Cantalamessa.

Kadhalika Padre Canatalamessa anasema, sisi tunasimamia juu ya Neno la Yesu:" tafuteni mtapata, bisheni mtafunguliwa (Mt 7,7). Ukisoma neno hilo, mara moja ni kufikiria kuwa Yesu anatoa ahadi ya kutupatia kila kitu tukiombacho na kubaki na mshangao kwa sababu mara nyingi hatuoni anatimiza. Lakini yeye alikuwa na lengo hasa moja ya kwamba: nitafuteni kwanza mtanipata na bisheni, nitawafungulia. Anatoa ahadi ya kujitoa mwenyewe, kuanzia mambo madogo madogo yale tunayo yaomba na kufikia hadi yale yanayoshindikana. Anaye mtafuta, anampata, anayebisha Yeye anamfungulia Mlango mara baada ya kumpata na kila kitu kinageuka kuwa mbadala, Padre anathibitisha.

Kurudi katika mambo

Padre Cantalamessa akitaka kuthibitisha hayo anaysema, anataja baadhi ya mifano kutoka maandiko kwamba: Biblia inatuonesha katika maandiko ambayo yanahusu Mungu kama aliye hai: yeye ni Mungu aliye hai, anasema Yeremiha (Yer 10,10; Ni mimi niliye hai, anasema Mungu mwenyewe katika Ezekieli (Ez 33,11). Katika moja ya zaburi iliyo nzuri zaidi katika masifu , iliandikwa wakati wa uhamishoni, ambapo anayeomba anasema; "roho yangu inakuonea kiu ya Mungu, Mungu aliye hai" ( Zab 42,2). Pia "Mwoyo na mwili wangu wote wamshangilia Mungu aliye hai" ( Zab 84,3)  Petro huko Kaisarea ya  Filipi alimtaja Yesu kuwa :“ Mwana wa Mungu aliye hai” (Mt 16,16).

Kwa upande wana wa  Israeli, inaonekana ni jinsi gani walikuwa wanajua kutengenisha kati ya Mungu na Miungu  ya watu iliyokuwa ni ya kifo. Kinyume na Mungu wa Biblia ni Mungu anayepumua na pumzi yake (ruah) ni Roho Mtakatifu. Aidha ametumia mfano mwingine wa Musa alipoona kichaka kinaungua, na jinsi gani sauti ya Mungu ilimweleza kuwa “mimi ni Mungu wa Baba yako na ndipo Musa aligeuka kuwa mkunjufu na kuitikia wito akaweza kuingia katika fumbo. Katika sehemu hiyo Mungu anaonesha jina lake kuwa ni yeye, kwa maana ya kulezea kuwa “ mimi ni yule ambaye nipo hata leo, tena na tena na nitakuwapo  kwa ajili yenu. Hii ni uthibitisho wa dhati na siyo wa kufikirika tu. Kwa maana hiyo sisi hatupo mbali na yule aliye hai, kwa maana anathibitisha, hata katika sehemu nyingine ya Biblia kuwa “mimi ni hai”. 

Mungu ni hisia ya uwepo, yeye ni mwamba kweli

Nini maana ya kelezea Mungu aliye hai? Kuanzia katika Biblia, Padre Cantalamessa amependa kufafanua zaidi,  ili asiweze kuangukia katika wazo la Mungu. Kile ambacho kinaweza kufanyika mbele ya Mungu aliye hai na zaidi kupitia ishara za utambuzi wa watu walizofanya, zinathibitisha kuwa uwezi kujifungia maisha katika mawazo tu. Suala la Mungu ni jamba ambalo ni tofauti kabisa na lingine, ambalo linaweza na wakati mwingine kuwa gumu kulieleza. Sura ya Biblia ambayo inazungumzia  Mungu ni kwamba yeye ni mwamba. Maelezo mengi ya Biblia, ina uwezo wa kuunda hisia hizo za kuonesha uhai wa Mungu aliye juu yetu sote, yaani Mungu ni mwamba. Kutokana na hili, tutafute nasi kuonja utamu kama maandiko matakatifu yasemayo kuwa asali itokayo mwambani ( tz Dt 32,13) amaethibitisha Padre Canatalamessa.

Mwamba pia unaoneshwa katika Biblia kama jina maalumu la Mungu hadi kufikia kuandikwa kwa elufi kubwa” Yeye ni Mwamba kamili na kazi yake (Dt 32,4) Bwana ni mwamba mkuu (Is 26,4) . Kadhalika, Biblia inaongeza kusema kuwa: Yeye ni mwamba wetu, mwamba, wangu. Ikiwa na maana ni mwamba kwa ajili yetu na siyo dhidi yetu, Bwana ni mwamba wangu ( Zab 18,3) mwamba wangu anilindaye (Zab 31,4) mwamba wa wokovu wetu( zab 95,1). Watafsiri wa kwanza wa Biblia, wale 70 waliogopa mbele ya ukuu wa sura ya namna hiyo ya Mungu, ambaye alikuwa anaonekana kama hasiyepitika na baadaye  wakaweka badala ya mwamba kuwa ni  nguvu, kimbilio, wokovu.  Lakini licha ya tafsiri hizo, Mungu bado anabaki katika asili yake ya kuwa mwamba. Mwamba siyo wasifu wa kufikirika tu, bali ni Mungu kwa ajili yetu.

Mwamba wetu umetengenezwa na ngazi, kwa ajili ya kutafuta kimbilio na si tu kwa ajili ya kuonekana kwa mbali. Mwamba inavutia na kupendwa. Iwapo Mungu ni mwamba, binadamu lazima awe mpanda mwamba. Yesu alisema: jifunzeni kutoka kwa wakuu wa nyumba;tazameni wavuvi: Mtakatifu Yakobo anaendelea akisema tazamaneni wakaulima  na sisi tunaweza kuongeza: Tazameni wapanda mwamba. Iwapo usiku unaingia au dhuruba inakuja, hawawezi kushuka bali kujibamiza katika mwamba huo wakisubiir dhoruba ipite. Msisitizo wa Biblia juu ya Mungu  ni Mwamba, lengo lake ni kama kuendeleza imani kwa viumbe  na kuwaondolea ile hofu katika mioyo yao: ardhi ikitetemeka hatuogopi , hata milima ikiangukia chini ya bahari, zaburi inasema; na sababu hiyo inajitafsiri kuwa Mwamba wetu mkuu ni Mungu wa Yakobo ( Zaburi 46,3.8)

Mungu yupo anatosha!

Maandishi ya kwanza ya Mtakatifu Francisko wa Assisi, yaliyo andikiwa na Toma ya wacelano anaelezea kipindi cha giza na ambacho alikuwaanakiona kama   mwisho wa maisha yake, hasa kuona vizingiti vya maisha ya ndugu wengine waliokuwa wamekengeuka. Kutokana na matatizo hayo alikuwa anasubri wokovu wake kwa Mungu na mabapo alisema hata kama shirika lingeweza kupungua mafrati wake wafikia hata watatu, Mungu angebaki kuendelea kuwa msaada wake thabiti daima. Amehitimisha tafakari yake akiwashauri warudie maneno hayo marahisi katika Kanisa au katika maisha yetu tunajikuta kuwa na hali kama hiyo ngumu ya  Mtakatifu Francis wa Assisi  na kurudia kusema kama yeye kwamba: "Mungu yupo na anatosha"!

07 December 2018, 15:48