Rais wa Baraza la kipapa la Mawasiliano Bwana Paolo Ruffini akiwa na Papa Rais wa Baraza la kipapa la Mawasiliano Bwana Paolo Ruffini akiwa na Papa 

Ruffini:Nguvu ya kuwasiliana ya Papa inatokana na kukutana!

Baba Mtakatifu anawasiliana hasa anapokutana na wengine. Nguvu yake ya kutoa taarifa inatokana na kukutana. Ndiyo uthibitisho wa Bwana Paulo Ruffini, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano wakati wa hotuba yake kwenye mkutano mjini Roma, tarehe 3 Desemba 2018, ulioongozwa na mada ya mapatano kati ya kizazi

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu anatoa anawasiliana na hasa anapokutana na wengine. Nguvu yake ya kutoa taarifa inatokana na kukutana. Mara nyingi katika nyakati zetu mawasilinao yanajengwa juu ya migawanyo na kujidanganya, kwa maana ya hasi na usalama. Hayo yamethibitisha na Bwana Paulo Ruffini, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican, katika hotuba yake kwenye mkutano mjini Roma, tarehe 3 Desemba 2018, ulioongozwa na mada “mapatano kati ya kizazi” katika fursa ya kuwakilisha kitabu kipya chenye jina, "Hekima katika nyakati”: Mazungumzo na Papa Francisko juu ya masuala makuu ya maisha”. Akifananisha na virusi vinavyo shambulia mifupa ya binadamu na ukosefu wa uwezo wa kukutana, Bwana Ruffini amethibitisha kuwa, kujigawanya kati ya wengine ni sawa na kujigawa mtu binafsi.

Ni kuaminiana wakati wa kukutana ndipo inawezakana kujenga amani

Hata hivyo Bwana Rufini amejikita pia katika umakini wa mchakato wa ujenzi wa amani. Iwapo tunafikiria kuwa utambulisho wetu unategemea kukanusha utambulisho wa mwingine, tunajenga kuta za uhasi, na kinyume na amani. Umakini ni unapaswa kuzingatia umuhimu wa kumbukumbu. Na ndiyo kuaminiana kunaweza kusaidia katuka kukutana kwa ajili ya ujenzi wa amani dhabiti.

Kitabu kipya kinazungumzia juu ya kumbukumbu katika wakati na ambapo utafikikiri ni katika kuanza mwanzo. Kinazungumza juu ya kushirikishana katika kipindi ambacho tumepoteza uwezo huo na ambapo hatuna uwezo wa kuweza kuanzisha kwa upya wakati wetu. Kutokana na suala hili la mapatano kati ya vijana na wazee Bwana Ruffini ameonesha jinsi gani vijana wa leo wanatafuta babu na bibi zao ili wapate kusilimuliwa wakati uliopita yaani wa kizazi chetu, kizazi cha watu wazima leo hii ambao hawajuhi kusimulia. “Kitabu hiki kinaunganisha nyakati na watu na kutufanya tufikiri kwa jinsi gani elimu ni kitu tofauti cha mafunzo ambayo yanasaidia tutoke nje na ili kukutana”. Amehitimisha Bwana Rufini.

 

05 December 2018, 15:06