Papa Francisko, Ijumaa, tarehe 14 Desemba 2018 amekutana na kuzungumza na Rais Andrej Kiska wa Slovakia. Papa Francisko, Ijumaa, tarehe 14 Desemba 2018 amekutana na kuzungumza na Rais Andrej Kiska wa Slovakia. 

Rais Kiska wa Slovakia akutana na Papa Francisko: COP24 & OSCE

Katika mazungumzo yao, Baba Mtakatifu pamoja na Rais wa Slovakia, wamegusia mahusiano ya kidiplomasia kati ya pande hizi mbili sanjari na mchango wa Kanisa katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Slokavia hususan katika sekta ya elimu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 14 Desemba 2018 amekutana na kuzungumza na Rais Andrej Kiska wa Slovakia ambaye baadaye pia amekutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameandamana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican. Katika mazungumzo yao, Baba Mtakatifu pamoja na Rais wa Slovakia, wamegusia mahusiano ya kidiplomasia kati ya pande hizi mbili, sanjari na mchango wa Kanisa katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Slokavia hususan katika sekta ya elimu.

Baadaye, viongozi hawa wawili wamejielekeza zaidi katika masuala ya kimataifa hususan athari za mabadiliko ya tabianchi; huduma ya ukarimu na upendo kwa wakimbizi na wahamiaji mintarafu Mkataba wa Kimataifa wa Usalama wa Wahamiaji wa mwaka 2018 pamoja na Mkutano 24 wa Mkataba wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP 24 Katowice, Poland. Mwishoni, Baba Mtakatifu Francisko na Rais Kiska, wamejadiliana pia masuala ya kimataifa mintarafu amani, usalama na ushirikiano wa kimataifa Barani Ulaya, ikizingatiwa kwamba, Slovakia, mwaka 2019 itakuwa inakalia kiti cha urais wa OSCE, yaani Shirikisho la Ushirikiano wa Kimataifa la Usalama na Maendeleo barani Ulaya.

 

 

14 December 2018, 15:00