Tafuta

Zahanati mpya ya Papa inayopatikana katika nguzo za Mtakatifu Petro kwa ajili ya watu wasio na mahali pa kulala na mahujaji  Zahanati mpya ya Papa inayopatikana katika nguzo za Mtakatifu Petro kwa ajili ya watu wasio na mahali pa kulala na mahujaji  

Papa Francisko ametoa zawadi ya zahanati kwa wasio na nyumba!

Zawadi ya Baba Mtakatifu Francisko katika fursa ya Noeli ni kituo cha afya kwa ajili ya watu wasio kuwa na mahali pa kulala na mahujaji wanaofika kwenye mikutano mjini Vatican. Kito hicho kinaitwa "Mama wa Huruma"

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kufutia na sikukuu ya Noeli, Baba Mtakatifu Francisko ametoa zawadi kwa watu wasio kuwa na mahali pa kulala, kituo cha afya kitachowekwa karibu na nguzo za Mtakatifu Petro. Kituo hicho kitaitwa jina la Mama wa Huruma, kitachukua nafasi ya Mtakatifu Martino, ambacho kilikwisha anza kufanya kazi yake mwaka 2016. Kitasaidia hata mahujaji wakati wa kufanya mikutano ya Papa.

Zawadi ya Baba Mtakatifu kwa watu wasio kuwa na mahali pa kulala

Mkuu wa kitengo cha sadaka ya Kitume, amethibitisha ufunguzi wa kituo kidogo cha afya chini ya nguzo ya Bernini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, ambacho kinachukua nafasi ya kile cha Mtakatifu Martino, ambacho kilianza kufanya kazi yake tangu mwaka 2016. Kituo cha Afya kimepewa jina jipya “Mama wa Huruma” kwa mujibu wa andiko lilobandikwa juu ya maingilio. Hiyo ni zawadi iliyotolewa na Baba Mtakatifu kwa watu wote wasio kuwa na nyumba ambao daima wapo katika nguzo mjibi Vatican na ambao watapata huduma ya afya na haya huduma nyingine ambazo zilikwisha anza kama vile kuoga, kufua nguo na kinyozi.

Kituo cha afya kitakuwa na madaktari na pia kupima baadhi ya magonjwa

Kazi ambayo imefanyika na kuhitimishwa kwa siku hizi, imepangwa na kutimizwa na Mamlaka ya Vatican, kwa uendeshaji wa Kitengo cha huduma ya usafi na Afya Vatican. Ndani ya jengo hilo vimetengenezwa vyumba vitatu vyenye kuwa na vyombo vyote vya madaktari na ofisi kuu, vyumba viwili vya bafu na chumba cha mapokezi vimewekwa upande wa kulia wa nguzo. Kila kitu kimefanyika kwa udhati na kwa heshima kubwa, lakini pia kwa kutumia mbinu za kisasa na kuzingatia mahitaji muhimu ya afya na usafi. Vyumba vina vifaa na mitambo mpya ili kuweza kutoa huduma ya kwanza ya matibabu kwa kutumia baadhi ya vyombo vya upimaji.

Kituo cha afya kitatoa hata huduma ya kwanza kwa mahujaji wakati wa mikutano ya Papa

Aidha katika taarifa zaidi inasema kuwa, Kituo cha afya kinachofunguliwa kwa watu wenye kuhitaji kwa siku tatu kwa wiki: Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi. Kuanzia asubuhi kwa wale wanaoishi katika maeneo, na siku zinazobaki, kituo kitafunguliwa kwa huduma ya kwanza kwa mahuji wakati wa mikutano na Baba Mtakatifu iwe uwanja wa Mtakatifu Petro au katika Kanisa Kuu.

Huduma hii itatolewa na watu wa kujitolea madaktari na watu wahusika wa afya

Huduma katika kito cha afya itaendeshwa na watu wa kujitolea ambao ni madaktari bingwa, watu wanaohusika na Afya kwa upande wa Vatican na Chuo Kikuu Torvegata Roma, kadhalika watu wa kujitolea wa vyama vya Mshikamano wa madawa, Chama cha Italia cha Magonjwa ya miguu. Zaidi katika kituo hicho cha afya kitatumika kufanyiwa mazoezi kwa wanafunzi na wanafunzi ambao wanajiandaa katika utaalam wa Kitivo cha Madawa kutoka Chuo Kikuu cha Tor Vergata Roma.

22 December 2018, 14:57