Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amtembelea Baba Mtakatifu mtaafu Benedikto XVI Baba Mtakatifu Francisko amtembelea Baba Mtakatifu mtaafu Benedikto XVI  (Vatican Media)

Papa Francesco ametakia matashi mema ya Noeli Papa Benedikto XVI

Tarehe 21 Desemba 2018 Baba Mtakatifu amekwenda kumtembelea Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XIV katika fursa ya kumtakia matashi mema ya sikukuu ya Noeli 2018

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ilikuwa karibia saa 12.15 za jioni masaa ya Ulaya, siku ya Ijumaa tarehe 21 Desemba 2018, kama afanyavyo kila mwaka, Baba Mtakatifu Francisko alikwenda katika Monasteri ya “Mater Ecclesiae” ili kutamkia matashi mema ya Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XIV.

Hata hivyo mwezi Oktoba 2018 Papa Francisko na Papa Benedikto XVI walikuwa wamekutaka katika jengo hilo, kwenye moyo wa Bustani za Vatican wakati wa mkesha wa kutangazwa kwa Mtakatifu Paulo VI, Askofu Oscar Romero na wenye heri watano wa Kanisa. Na vile vile kabla ya hiyo inakumbukwa, ilikuwa ni fursa ya kuhitimisha Mkutano hapo Juni mwaka huu, ambapo makardinali 14 wapya walikwenda kumtembelea Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI ili kukutana naye na kusali kwa pamoja, ishara ya undugu.

22 December 2018, 12:46