Tafuta

Vatican News
Familia Takatifu ni nyumba ya sala na upendo, ni nyumba ya kuheshimu na kulinda Familia Takatifu ni nyumba ya sala na upendo, ni nyumba ya kuheshimu na kulinda 

Papa:Familia ni nyumba ndogo ya sala na shule ya Injili!

Baba Mtakatifu Francisko anasema kuwa, sala ya Familia Takatifu ya Nazareth inafanya hata familia yetu kuwa mahali pa muungano wa sala; Familia Takatifu ya Nazareth ni shule ya kweli ya Injili na Kanisa dogo la nyumbani

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika kuadhimisha  sikukuu ya kila mwaka ya Familia Takatifu ya Yesu Maria na Yosefu, ni vema kutafakari kwa kina utakatifu wa familia hiyo. Baba Mtakatifu Francisko anasema kuwa Sala ya Familia Takatifu ya Nazareth inafanya hata familia zetu kuwa mahali pa muungana na mkutano wa sala; Familia Takatifu ya Nazareth ni shule ya kweli ya Injili na Kanisa dogo la nyumbani.

Familia ni Kanisa la nyumbani

Mada ya familia leo hii inayoshikamana na iliyo na matatizo ndiyo wazo kuu la mara kwa mara la Baba Mtakatifu  Francsiko. Inatosha kufiria katika Mkutano wa III wa Sinodi ya Maaskofu iliyofanyika kuanzia tarehe 5-9 Oktoba 2014, iliyoongozwa na mada: Changamoto za Kichungaji juu ya familia kwa mantiki ya uinjilishaji; na kama ilivyokuwa Mkutano mkuu wa XIV wa Sinodi ya Maaskofu iliyofanyika kuanzia tarehe 4-25 Oktoba 2915 ikiongozwa na Mada: Miito na utume wa Familia katika Kanisa na katika dunia ya sasa; hadi kufikia kutoa Wosia wa kitume wa Amoris laetitia ulitolewa kunako tarehe 19 Machi 2016. Tarehe 3 Oktoba 2015 wakati wa mkesha wa sala ya kuombea Sinodi, Baba Mtakatifu alisisitiza kwamba, ili kuweza kutambua familia leo hii ni lazima kuingia hata sisi ndani ya fumbo la Familia ya Nazareth, katika maisha yake yaliyofichika, ukawaida na upamoja, kama ambao ni sehemu kubwa ya familia zetu na mateso yao na furaha zao rahisi (…)

Ndani ya familia inavutwa hewa ya kumbukumbu ya kizazi na mizizi yake iliyosimikwa inaruhusu kwenda mbali. Ni mahali pa kufanya mang’amzi, mahali pa kuelemisha na kutambua ishara za Mungu juu ya maisha binafsi na kuyakumbatia kwa imani. Ni mahali pa kupewa zawadi bure; ni mahali pa uwepo umakini kindugu mshikamano na mahali ambamo tunafundishwa kuondoa ubinafsi wetu na kuotka njeili kumpokea  na kumkaribisha mwingine.

Mwana wa Mungu anazaliwa ndani ya familia

Zawadi ya familia imetolea na Bwana duniani tangu mwanzo alipomuumba Adamu na Eva na kuwapatia utume wa kuzaa na kuongezeka na kujaza nchi; zawadi ambayo Yesu mwenyewe ameithibitisha kwa kuweka mhuri na Injili yake. Katika Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 17 Desemba 2014 aliweka bayana kwamba, tendo la  Mwana wa Mungu kujifanya mtu linafungua mwanzo mpya wa historia ya ulimwengu wa mwanamke na mwanaume. Na mwanzo huo unajikita katika umbu la familia huko Nazareth.

Yesu angeweza kuja duniani kwa mtazamo  wa ukuu au kama mpiganaji shujaa na  mfalme mkuu, lakini anakuja kama mtoto katika familia. Mungu alichagua azaliwe katika familia ya binadamu, katika kijiji kilicho kuwa kimesahulika kwa Utawala wa Kirumi. Familia ya Nazareth haikuwa familia isiyo ya kweli, kwa maana ilifanya uzoefu wa matatizo na mateso, kama ambayo yanatokea hata leo hii kuazania kaskazini na kusini mwa dunia nzima, lakini  familia hiyo ilikuza utakatifu wa kawaida, na ndio maana  familia ya Nazareth hata leo inatuwajibisha kugundua wito na utume wa kila familia na kufanya upendo uwe wa kawaida na siyo chuki; upendo uwe wa kawaida kwa maana ya kusaidiana pamoja na siyo utofauti na uadui.

Wakati endelevu unapitia ndani ya familia

Ziara nyingi za kitume za Baba Mtakatifu zimekuwa zikijikita sana na mikutano na familia nyingi duniani. Katika ziara yake nchini Sri Lanka na Ufilippini kuanzia tarehe 12-19 Januari 2015, kwa mfano wakati wa kutoa hotuba yake katika uwanja wa Mal ya Asia mjini Manila, Baba Mtakatifu aliweka angalisho la ukoloni mpya wa itikadi ambao unatafuta kuharibu familia na aliweza kutaja baadhi ya itikadi hiyo katika nchi  ambazo zimezidi kushambulia maisha ya familia leo hii, na zaidi idadi ya uzito unaozidi kusumbua maisha ya familia leo hii, kugawanyika kwa familia kutokana na uhamiaji na kutafuta ajira, umasikini na kama ilivyo hata kuongezeka  kwa vishawishi vingi kwa upande wa baadhi ya taasisi za ndoa na zinazijihusisha katika mahusiano, utamaduni na ukosefu wa ufunguzi wa maisha. Katika hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko anakumbusha kuwa, wakati endelevu unapitia katika familia na kila hatari inayoshambulia familia, ni hatari inayohatarisha jamii yenyewe.

Familia kiwanda cha matumaini

Katika familia ni kujifunza kusali; katika familia ni kujifunza kupenda na kuifanya familia kila siku kuwa ya namna ya pekee kwa ishara ndogo za umaskini na mambo madogo ambayo yanafanya maisha daima yawe na radha ya familia. Imani inakua hasa ikifanyiwa uzoefu wa kuiishi na kutanda zaidi upendo. Baba Mtakatifu anasema hayo wakati wa kuhitimisha Mkutano wa VIII wa familia, tarehe 27 Septemba 2015 huko Philadelfia nchini Marekani na kwa maana hiyo alisisitiza kuwa, familia zetu, nyumba zetu ni mahali mwafaka ambamo imani na maisha yanakua katika imani. Familia zipo mahali popote  na zinaalikwa kuendelea kukua na kwenda mbele, nasisitiza tena Baba Mtakatifu tarehe 25 Agosti 2018, wakati wa Sikukuu ya Familia katika Uwanja wa mpira Croke mjini Dublin Ireland, wakati wa fursa ya Mkutano wa IX wa Familia duniani. Familia inazidi kwenda mbele japokuwa na matatizo na vikwanzo, kama vile walivyofanya kizazi kilichopita. Wote wote wanafanya kuwa sehemu ya mnyororo mrefu wa familia yenye asili tangu mwanzo uasili tangumwanzo na inayotembea katika nyakati. Familia zetu ni tunu msingi na hai ya kumbukumbu  na watoto wake ambao kwa namna moja nao wanakua nakugeuka kuwa wazazi, baadaye bibi na babu. Na kwa njia yao tunapokea utambulisho na thamani na imani.

Kuitikia ndiyo kamilifu

Maria na Yosefu walifungua mikono  katika ishara kuu ya Mungu na  ndiyo inapaswa kuwa leo hii hata kwa wale ambao wanachagua kuungana katika muungano wa ndoa. Watoto ni zawadi kubwa Baba Mtakatifu anasisitiza, tarehe 16 Juni 2018 alipokutana na wawakilishi wa Jukwaa la vyama vya Kifamilia nchini Italia wakati wanaadhimisha mwaka wa 25 tangu kuanzishwa kwa jukwaa hilo. Baba Mtakatifu anathibitisha. watoto wanapokelewa kama walivyo na  kama Mungu anavyo waumba na kama Mungu anavyoruhusu hata kama wakati mwingine ni wagonjwa. Vile vile Baba Mtakatifu Francisko wakati huo huo  alishutumu vikali suala la kuua watoto kwani ni lazima kuheshimu maisha ili watoto waweze kulindwa na kuwa na utulivu tangu kuumbwa kwao. Katika karne iliyopita anasema  duniani kote, watu walikuwa wakitoa kashfa juu ya kile kilichofanywa na utawala wa udikteta zamani ambao walibagua rangi, lakini leo hii hivyo hivyo wanafanya kwa kuvaa gloves nyeupe.

31 December 2018, 10:32