Ziara ya Papa Francisko  katika Nchi za  Falme za Kiarabu kwa mwaka 2019 ni mwafaka katika mazungumzo kati ya waislam na wakristo Ziara ya Papa Francisko katika Nchi za Falme za Kiarabu kwa mwaka 2019 ni mwafaka katika mazungumzo kati ya waislam na wakristo 

Ziara ya Papa katika Nchi za Kiarabu ni hatua muhimu ya mazungumzo ya kidini

Kutembelea Falme za Nchi za Kiarabu ni hatua ya kihistoria kwa ajili ya mazungumzo kati ya wakristo na waislam kwa ajili ya amani, hivyo tunampokea Papa kwa moyo mkunjufu na tunasali na maneno ya Mtakatifu Francis wa Assisi: Bwana nifanye niwe chombo cha amani. Amethibitisha hayo Askofu Paul Hinder Balozi wa Vatican katika nchi za Uarabuni Kusini

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ziara yake ya kwanza ya Baba Mtakatifu Francisko katika Pensula ya Kiarabu, ni kipindi mwafaka cha ufunguo wa mazungumzo kati ya waislam na wakristo. Amethibitisha hayo Askofu Paul Hinder Balozi wa Vatican katika nchi za Uarabuni Kusini, ambayo inajumuishwa ndani ya Nchi za Falme za Kiarabu kama vile Oman na Yemen. Askofu Hinder akizungumza na vyombo vya Habari za kimisionari Fides anasema, Tunampokea Baba Mtakatifu Francisko kwa moyo mkunjufu na tunasali na maneno ya Mtakatifu Francis wa Assisi, “Ee Bwana nifanye niwe chombo cha amani. Tunamtakia matashi mema na kwamba ziara yake ya kitume iwe ni hatua muhimu ya safari ya mazungumzo kati ya waislam na wakristo na kuchangia kwa kiasi kikubwa uelewa wa pamoja na amani katika nchi za Mashariki.

Ziara ya Papa Francisko katika nchi za Falme za Kiarabu 

Tarehe 6 Desemba Vatican ilitangaza kuwa Baba Mtakatifu Francisko atafanya zaiara yake ya kitume ya siku tatu katika nchi za Falme za Kiarabu kuanzia tarehe 3-5 Februari 2019. Ziara hii inakuja baada ya mwaliko wa Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, Mfalme mrithi wa Abu Dhabi na pia  Makamu mkuu wa kikundi cha  Nguvu za Kijesha za Kiarabu, ili audhurie Mkutano wa mazungumzo ya kidini utakao ongozwa na mada:udugu wa kibinadamu. Katika kutangaza juu ya ziara ya Baba Mtakatifu, Mfalme mrithi Mohammed ameandika katika ukurasa wake wa tweet yake kuwa: Papa ni ishara ya amani, uvumimilivu na uhamasishaji wa undugu. Tunasubiri kwa hamu ziara ya kihistoria, mahalia ambapo tutatafuta kuzungumza na kutafuta amani ya kudumu kati ya watu. Kutokana na hiyo, Balozi wa Vatican nchini humo anathibitisha pia kuwa ziara hiyo ni jibu la dhati la mwaliko aliopewa Baba Mtakatifu Francisko kwa upande wa kikundi kidogo cha Jumuiya ya wakatoliki wanaoishi katika Nchi za Falme za Kiarabu.

Kumbukumbu ya miaka 800 tangu Mtakatifu Francis wa Assisi akutane na Sultan

Askofu Hinder pia ameelezea juu ya shukrani zake pia  kwa Serikali ya Falme za Kiarabu na ambapo wameunda tayari tume maalum ndogo ya kuwasiliana na serikali hiyo ili kuweza kuandaa mantiki zote zinazohusiana na hija hiyo ya Baba Mtakatifu Francisko.  Maandhimisho ya Misa Takatifu itafanyika tarehe 5 Februari 2019 katika Uwanja wa Makao ya umma mjini Abu Dhabi. Kutokana na hiyo anasema kuwa hiyo ni ishara muhimu kwa serikali ambayo wanaipongeza na kuitambua.

Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko, katika Peninsula ya kiarabu ni ya mara kwanza kabisa. Mada ambayo imechaguliwa kuongoza ziara ya Baba Mtakatifu imechukuliwa kutoka katika sala ya Mtakatifu Francisko wa Assisi: Bwana nifanye niwe chombo cha amani. Ziara hiyo pia inaangukia katika kumbukumbu ya mwaka ambao wanaadhisha miaka 800 tangu kufanyika mkutano wa Mtakatifu Francis wa Assisi na Sultan Malik Al-Kamil, mkutano uliofanyika nchini Misri, kunako mwaka 1219.

13 December 2018, 13:13