K ati ya wageni waalikwa ni Bi Letizia Moratti katika kipindi cha nane cha AveMaria, kichoendeshwa na Padre Marko Pozza msimamizi wa Kanisa dogo la wafungwa Padova Italia K ati ya wageni waalikwa ni Bi Letizia Moratti katika kipindi cha nane cha AveMaria, kichoendeshwa na Padre Marko Pozza msimamizi wa Kanisa dogo la wafungwa Padova Italia 

Katika Tv2000 Papa anazungumzia juu ya kifo!

Kipindi cha nane kuhusu AveMaria, katika TV2000, Papa Francisko anathibitisha kuwa, dhambi kubwa ni kufikiria kuwa kamwe hakuna kifo. Kipindi hicho kitafanyika tarehe 4 Novemba 2018, saa 3.05 za usiku masaa ya Ulaya

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika mwendelezo wa vipindi 11 vinavyoendelea katika Luninga ya Baraza la Maaskofu Italia(tv2000), kuhusu AveMaria, tarehe 4 Novemba 2018 saa 3.05 za usiku masaa ya Ulaya, kitakuwa ni kipindi cha nane Papa Francisko anathibitisha kuwa dhambi kubwa ni ile ya kufikiria hakuna kifo kamwe. Kiini cha tafakariya kipindi hiki, ni kuhusu sehemu ya sala ya salam Matia inayojulikana na watu wengi duniani, kuanzia sas ana saa yak ufa kwetu amina. Mwendesha Kipindi hicho Padre Marco Pozza msimamizi wa Kanisa dogo la Magereza mjini Padova Italia, atakua na wageni Letizia Moratti, Sofia Cantisani na Talita Paula Leite.

Ukweli katika sala ya Salam Maria

Katika utangulizi wa kupinidi hicho, Baba Mtakatifu anakumbuka Shetani na Eva, na kuwaalika kutafakari juu ya kifo. Ni kipindi kigumu kufikiria juu ya mauti lakini ndiyo hali halisi ya mwisho wa safari ya binadamu. Kipindi cha maisha ya dhambi. Mwingine anaweza kusema kuwa hatakufa, kwa sababu hafikiri, na hivyo huko ni kujidanganya anathibitisha Baba Mtakatifu. Kama ilivyo katika mwanzo wa sala ya Salam Maria kuwa na ukweli dhati  wa wokovu, ndivyo inaishia na ukweli wa dhati wa hali ya binadamu, ambayo ni tunda la dhambi.

Amani

Baba wakati wa mazungumzo na Padre Pozza amethibitisha kuwa: “Wakati  wa kifo, ni nitamwomba mama Maria awe nami karibu na kunipa amani. Hata hivyo Katika mazungumzo yao amemweleza jisni gani aliwahi kufanya uzoefu wa kuomba kifo chema , na hasa katika kipindi cha mafunod yao seminarini, maana ili kuwa ni kawaida enzi zile. Wakati wa Mafungo yalikuwa yanaanza kwa kuomba uhuruma ya Bwana, na maelezo kamili ya wakati wa kufa. “Ilipokuwa inafikia hatua ya kutokwa na  jasho, ndipo ulikuwa ukitamka, Yesu wa huruma, utuhurumie. Ilikuwa ni kawaida kwa kipindi hicho na ilikuwa hali halisi”, Baba Mtakatifu amebainisha.

Vijana na utamaduni wa hewa

Baba Mtakatifu akifafanua zaidi amekuwa na wazo hata kwa vijana na hisia zao za upweke na kuachwa. “katika utamaduni wetu na mapendekezo yetu, tumeondoa mizizi kwa vijana. Tunawanya wakute utamaduni usio wa dhati, utamaduni wa maji , kwa kutumia neno la mfalsafa moja, amesema kuwa auite utamaduni wa hewa, usiokuwa na mizizi. “Ninafikiri ustaarabu wetu una makosa,Vijana leo hii wanahitaji kusimika mizizi japokiwa Mama Maria hakupoteza mizizi yake”.

Haki

Katika kuendelea ufafanuzi wa suala hili la kifo Baba Mtakatifu ameelezea hata suala la kujiua. Kujiua binafsi, ni kama vile kufungua mlango wa wokovu, japokuwa anabainisha kuwa na utambuzi ya kwamba katika tendo la kujiua binafsi, ndani yake hakuna uhuru kamili.  Na hatimaye ameelezea kwa ufupi juu ya kielelezo cha “ Dada kifo “neno lililotumiwa na Mtakatifu Francisko wa Azizi ambapo amethibitisha kupenda  kwa jinsi  ya kufikiria kifo kama tendo la haki ya mwisho. Dhambi inalipwa kwa njia hiyo, lakini inafungulia wokovu kwa upande mwingine. Kupenda kifo, Baba Mtakatifu amesema, siyo sehemu ya utamaduni wake, lakini kila  mmoja wetu anao utamaduni wake na anaweza kuufanya.

04 December 2018, 15:02