Vatican News
Yesu Kristo ni mkuu na anamwonesha Mungu aliye hai, anaingia katika mawasiliano na Yeye, kwa mujibu wa roho ya Injili ya Yohane Yesu Kristo ni mkuu na anamwonesha Mungu aliye hai, anaingia katika mawasiliano na Yeye, kwa mujibu wa roho ya Injili ya Yohane  (Vatican Media)

Hakuna aliyemwona Mungu na ukuta wa dhambi ulivunjwa

Katika Tafakari ya tatu ya Majilio katika nyumba Kuu ya Kipapa Padre Cantalamessa amejikita kutafakari mada ya “hakuna aliyemwona Mungu”. Mtaalimungu wa Kibizantino, Nicola Cabalas aliandika kuwa, kati yetu na Mungu kulikuwa na kuta tatu za kutengenisha. Ya kwanza ni ile ya asili; Ya pili ni ile ya dhambi na ya tatu ni kifo

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mungu aliye hai ni Mungu wa Utatu ambaye tulimtaja kipindi kilichopita. Lakini sisi tuko katika kipindi na Mungu, na ni wa milele. Je ni jinsi gani ya kushinda utofauti huu usioisha? Je ni kwa jinsi gani ya kutupia mbali daraja refu lisiloisha? Jibu lake linatokana na kile tunachojitayarisha kuadhimisha yaaani, “Neno lililofanyika mwili na akaja kuishi katikati yetu”.

 Kuta tatu za utengenishi: mwili, dhambi na kifo

Ndiyo mwanzo wa wa tafakari ya Padre Raniero Cantalamessa, Mhubiri wa Nyumba ya Kipapa katika tafakari ya tatu ya Kipindi cha Majilio kwa Mwaka 2018 ambayo ameongozwa na mada ya “Hakuna aliye mwona Mungu”. Padre Cantalamessa anasema: Aliandika mtaalimungu wa Kibizantino, Nicola Cabalas kuwa kati yetu na Mungu kulikuwa na kuta tatu za kutengenisha. Ya kwanza ni ile ya asili kwa sababu Mungu ni Roho na sisi ni mwili; Ya pili ile ya dhambi na ya tatu ni kifo. Moja ya kuta hizi, ilivunjwa vunjwa kwa sababu ya Mungu kujifanya mtu, wakati asili ya kibanadamu na asili ya Kimungu viliungana katika nafsi ya Kristo: Ukuta wa dhambi ulivunjwa juu ya Msalaba, na ukuta wa kifo kwa njia ya ufufuko. (Nicholas Cabalas, Maisha katika Kristo, III, 3). Yesu Kristo ni sehemu ya mwisho ya kukutana kati ya Mungu aliye hai na binadamu aliye hai. Kwa njia yake, katika Mungu aliyekuwa mbali amekuwa karibu na akawa Emanueli, Mungu pamoja nasi.

Hatua za kumfafuta Mungu aliye hai, katika majilio hayaa

Padre Cantalemessa amesema, hatua ya kumtafuta Mungu aliye hai ambayo wamejikita katika Majilio hayo kwa kipindi hiki imetanguliwa na fikira juu ya Mungu za Mtakatifu Bonaventura. Kama mfalsafa na mtalimungu yeye alitambua kufafabua ngazi saba ambazo roho inaelekea utambuzi wa Mungu. Na hizo ni: Maono yake kwa njia ya mzunguko wa ulimwengu; Kutafakari kwa kina Mungu katika mzunguko wa ulimwengu ulio mwepesi; Kutafakari kwa kina Mungu kwa njia ya sura yake inayovutia na mantiki zake za asili; Kutafakari kwa kina Mungu katika sura yake iliyopyaisha na zawadi za neema; Kutafakari umoja wa Mungu katika jina lake la kwanza ambalo ni lile la kuwa ni; Maono ya Utukufu wa Utatu kama Wema; Na ya hatua ya ya saba ni kuchukuliwa katika tafakari ya kina ya roho ambayo kazi ya kiakili  inaunganishwa na ile ya upendo  na kwenda moja kwa moja kwa Mungu.

Padre Cantalamessa anathibtisha hayo kwa kutumia maneno ya Waebrania: “Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya (Ebr 1, 1-2).  Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu; (Ebr 1,3). Anaongeza kuthibitisha kuwa: Hii ni kutokana na mtazamo wa ukuu wake na mambo hayo ya kimungu. Na kwa upande wa mtazamo wa maisha, habari njema ni sasa ambaye lazima wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu. (Mdo 17,27), anakwenda kutamfatu Mungu anayeishi; Ni mungu anayeshuka kumtafuta mtu ili aweze kukaa katika moyo wake. Yeye hadi sasa unaweza kukutana naye na kumwabudu katika Roho na ukweli kwa maana yeye anasema; Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake na kufanya makao kwake. (Yh 14,23). Hakuana afikaye kwa Baba ila kwa njia yangu.

Aliye fanya ukweli huo yaani Yesu Kristo ni mkuu na anamwonesha Mungu aliye hai na ambapo inaingia katika mawasiliano na Yeye, katika moyo huo wa Injili ya Yohane. Tunamwamini Yesu kwa sababu atusaidie kufanya utafiti wa Mungu aliye hai, zaidi ya kitu kilicho rahisi na ili kufkira uzoefu wa kuwa na utambuzi na hisia hai. Bila kupoteza ushuhuda wake ni lazima kukimbilia katika maneno yake rahisi ambayo Yesu mwenyewe anajionesha moja kwa moja kumwakilisha Mungu. Kila moja ya maneno hayo yana uwezo wa kutufikisha juu ya fumbo na kutufanya tuone upeo usio na mwisho.

Wasio mjua Kristo wamebaguliwa? Hawataona wokovu?

Tunasoma katika Injili ya Yohane: Yesu alisema, mimi ni njia, ni ukweli na maisha, hakuna ajaye kwa Baba ila kwa njia ya mimi. Hapa tunatakiwa kusimama na kutafakari kwa kimya Padre Canatalamessa amebainisha. Hakuna ajaye kwa Baba ila kwa njia ya mimi. (Yh14, 6: Kusoma sehemu hii katika mantiki ya majadiliano ya ya kidini, maneno hayo yanaweza kutufanya tujikite katika ukimya. Je ni jinsi gani ya kufikiria sehemu ya ubinadamua ambao hawajui Kristo na Injili yake? Je hakuna kati yao watakwenda kwa Baba? Je hao wamebaguliwa kwa njia ya Kristo na kwa maana hiyo hawatakuwa na wokovu?

Padre Cantalamessa amethibitisha kuwa jambo moja ni la uhakika ya kwamba kila mtaalimungu wa kikristo katika dini anathibitisha kuwa: Kristo ametoa maisha kwa ajili ya kuwaokoa wengi, na kwa ajili ya upendo wa watu wote na kwa sababu hiyo  kila Kiumbee aliyeumbwa na Baba yake, ni ndugu yake. Yeye hakufanya utofauti. Kujitoa kwake sadaka, ni kwa ajili ya ulimwengu mzima. Na Yesu mwenyewe anathibtisha kuwa: Nami nitakapoinuliwa kiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu (Yh 12, 32); na Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. (Mdo 4, 12).

Zaidi ya wokovu wa wale ambao hawakumjua Kristo ingekuwa vizuri kuhangakia  wale ambao wanaamini, wokovu wa wale ambao wamemtambua Kristo, lakini wanaishi utafikiri hajawapo , wamemsahau kwa kila kitu hasa katika ubatizo wakeo , wanakuwa kinye na Kanisa, na kila aina ya tendo la dini. Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye. Mtakatifu Francis wa Assis kwa mara nyingine tana katika kipinid chek, alisema kila wema unaoptaikaka kwa watu, wapagani, au ahaya vyote vinakwenda kwa Mungu kisima cha wema.

Nafasi ya Yesu Kristo anaye mwonesha Mungu aliye hai

Kwa kuzungumza nafasi ya Kristo mbele ya watu amabo hawaamini na kuishi nje ya Kanisa. Na ndiyo maana mwisho wa maisha yake duniania Yesu alisema: Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni (Yh16, 12-15).

Nafasi ya Yesu Kristo anaye mwonesha Mungu aliye hai, inaihitimisha zaidia katika utangulizi wa Injili ya Yohane. Si katika tafakari ya sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana bali katiuka utenzo wake ambao unatoka katika mioyo yetu kutoa utukofu wa Utatu Mtakatifu. Katika Kanisa, watangaza kuwa Yesu Kristo mwana wa Mungu, na mwana wa ulimwengu wenye thamani ya wokovu. Ndiyo umani yetu ambayo Kristo alianzisha Kanisa leo na kuahidi  hata milango ya kuzimu haitafunguka.

21 December 2018, 15:23