Cerca

Vatican News
Misa Takatifu ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican tarehe 17 Desemba 2018 Misa Takatifu ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican tarehe 17 Desemba 2018  (@L'Osservatore Romano)

Baraza la Kipapa la Mawasiliano:Misa ya Noeli na matashi mema kwa Papa

Tarehe 17 Desemba 2018, Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Prero imeadhimishwa misa kwa wafanyakazi wote wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican. Misa imeongozwa na Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, Katibu Msaidizi wa Vatican

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Matashi mema ya Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana kwa wote, kwa namna ya pekee wazo ni kwamo  Baba Mtakatifu Francisko, ambapo tarehe 17 Desemba anakumbuka Siku ya kuzaliwa kwake na  maadhimisho ya Ekaristi hii  iwe hata sala kwa ajili ya nia zake na shukrani kwa zawadi ambayo Bwana ametutendea na anatutendea kila siku kwa uwepo wake kati yetu.

Ndiyo maneno ya Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, Katibu Msaidizi wa Vatican aliyotoa wakati wa maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu asubuhi tarehe 17 Desemba 2018 katika Altare ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, ushiriki wa wafanyakazi wote wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Katibu wa Baraza hilo Monsinyo Lucio Adrian Ruiz, Monsinyo Edoardo Viganò ambaye ni mshauri, pia mapadre wote waandishi wa habari katika Baraza la Mawasiliano Vatican.

Mwisho wa mwaka ni fursa maalu kuongozwa ndani ya roho

Askofu Mkuu Edgar Peña Parra katika mahubiri yake amewakumbusha wafanyakazi wote kwamba, “mwisho wa mwaka ni furaha maalum kwa ajili ya kuongozwa kwa kina ili kutafakari juu ya mantiki chanya na zile ambazo  ziweze ziboreshwa. Hiyo ina maana ya kufanya tafakari ya kina kwa ajili ya kutambua hasa kwamba muda ni zawadi ya Mungu”. Mantiki ya pili ambayo lazima kuitafakari kwa  mwaka unaokaribia kumalizika Askofu Mkuu Parra anasema ni ile ambayo ni ya kumshukuru Mungu  kwa yote tuliyopokea kutoka kwa Bwana. Kuanza mwaka na shukrani kwa Bwana ndiyo suala muhimu na chanya kwa ajili yetu.

Mungu yupo karibu nasi pia anayo historia na familia kaka sisi sote

Na mwisho Askofu Mkuu Papa  amewaalika  wafanyakazi wote ili waweze kuweka mipango yao yote, mateso na matumaini hasa ambayo yamo ndani ya mioyo kwenye   mikono ya Mungu, ambaye kama alivyokumbusha katika Injili ya Siku iliyokuwa inasimulia juu ya Kizazi cha Yesu na kwamba, Mungu yuko karibu nasi, yeye anayo historia na familia kama jinsi  sisi sote tulivyo na familia.

 

17 December 2018, 15:12