Papa Francisko amemteua Askofu Abel Gabuza kuwa Askofu mkuu mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Durban, Afrika ya Kusini. Papa Francisko amemteua Askofu Abel Gabuza kuwa Askofu mkuu mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Durban, Afrika ya Kusini. 

Askofu mkuu mteule Gabuza, Jimbo kuu la Durban, Afrika ya Kusini

Askofu Abel Gabuza ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Askofu mkuu mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Durban, Afrika ya Kusini. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mwandamizi mteule Gabuza alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Kimberley, Afrika ya Kusini. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mwandamizi mteule Gabuza alizaliwa kunako tarehe 23 Machi 1955.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Abel Gabuza kuwa Askofu mkuu mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Durban, Afrika ya Kusini. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mwandamizi mteule Gabuza alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Kimberley, Afrika ya Kusini. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mwandamizi mteule Gabuza alizaliwa kunako tarehe 23 Machi 1955 huko Alexandra.

Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, kunako tarehe 15 Desemba 1984 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 23 Desemba 2010 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Kimberley na hatimaye, kuwekwa wakfu tarehe 19 Machi 2011. Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 9 Desemba 2018 akamteuwa kuwa Askofu mkuu mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Durban, Afrika ya Kusini!

Askofu mkuu Gebuza
10 December 2018, 08:49