Cerca

Vatican News
Maandalizi ya mshikamano mjini Vatican kwa ajili ya nchi ya Iraq na utume wa wamisionari wa Don Bosco kwa watoto wakimbizi  nchini Uganda Maandalizi ya mshikamano mjini Vatican kwa ajili ya nchi ya Iraq na utume wa wamisionari wa Don Bosco kwa watoto wakimbizi nchini Uganda  

Vatican:Muziki wa mshikimano kwa ajili ya kusaidia Iraq na Uganda!

Kuna mshikamano kwa njia ya Tamasha la Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana mjini Vatican, iliyozinduliwa kwa njia ya kutumia ujumbe wa simu (SMS) katika namba 45530 ili kuwezesha kusaidia huko Erbil nchini Iraq na Palabek nchini Uganda

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tone dogo ni suluhisho kwa ajili ya matatizo. Ndivyo alivyowakilisha tukio la Tamasha la muziki, Monsinyo Angelo Zan, Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki akifafanua juu ya juhudi ya Baraza hilo katika  kuhamasisha na kuanzishwa kwa Scholas Occurente na Utume wa Don Bosco  kwa ajili ya kusaidia nchi mbili zenye matatizo yaani Iraq na Uganda.

Kutokana na hilo,wameandaa kufanya Tamasha la muziki la XXVI la Kuzaliwa kwa Bwana mjini Vatican, linalotarajiwa kufanyika tarehe 15 Desemba 2018 saa 12.30 za jioni masaa ya Ulaya katika ukumbi wa Paulo VI. Tamasha hilo litaongozwa na kauli mbiu: tutengeneza mtandao na elimu.  Ni  kauli mbiu yenye lengo la kukuza na kuendeleza hali halisi mbili zinazoendelea kukua huko Erbil nchini Iraq na Palabek nchini Uganda.

Scholas Occurentes inajitahidi kusaidia watoto wa Iraq, kwa njia ya mtandao uliopo  kati ya mashirika na kuhamasisha ushiriki  wa mashule na vyuo vikuu vya Italia. Wamisionari wa Mtakatifu Don Bosko wako wanajikita kusaidia wakimbizi 40,000 kutoka nchi ya Sudan ya Kusini kwa kuwafundisha baadhi ya vijana wote walioko katika kambi ya Palabek ambao walikimbia na mama zao kutokana na migogoro nchini mwao. Ili kuweza kuchangia na kusaidia mipango ya shughuli hiyo, tayari ilizunduliwa kwa mpango wa kutuma fedha kwa njia ya ujumbe (sms)  wa mshikamano kwa namba 45530!

Kati ya washiriki wa tamasha la muziki la XXVI, kuna waimbaji maarufu kama vile: Dee Dee Bridgewater, Anastacia, Raphael Gualazzi, Edoardo Bennato, Alessandra Amoroso, Elisa, Ermal Meta,  Miguel Angel Zotto na Daiana Guspero. Mwalimu atakayeongoza bendi hiyo ya nyimbo ya ulimwengu ni Renato Serio, kwa ushirikiano na mwalimu Stefano Zavattoni. Kutakuwa na kwaya ya kiinjili ya “New Direction Tennessee State Gospel Choir” kutoka Marekani,  waimbaji watakaosindikizwa ni wale wa’Art Voice Academy, wakati kwaya ya watoto ni ile ya  Le Dolci Note, ikiongozwa na mwalimu Alessandro Bellomaria.

muziki wa mshikamano
27 November 2018, 09:41