Tarehe 21 Novemba ni Siku ya Uvuvi Ulimwenguni Tarehe 21 Novemba ni Siku ya Uvuvi Ulimwenguni 

Ujumbe wa Kard.Turkson:Siku ya Wavuvi duniani na sala!

Ujumbe kwa maadhimisho ya Siku ya Uvuvi ulimwenguni uliotolewa na Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Huduma na Maendeleo fungamani ya binadamu, akijaribu kufafanua kwa kina na mapana nini maana ya siku hiyo na baaadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo wavuvi duniani

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Siku ya Uvuvi ulimwenguni ilianzishwa na Jumuiya  ya wavuvi huko New Delhi India kunako tarehe 21 Novemba 1997 wakati wawakilishi wa wavuvi na utamaduni, pamoja na wafanyakazi wa sekta ya baharnii kutoka nchi 32 duniani waliungana pamoja kama njia mojawapo ya kusheherekea kazi hiyo inayowapatia kipato watu wengi duniani na kuunda  shirika la Kimataifa kwa kujiwekea malengo ya kusaidiana  kwa matendo ya dhati katika uvuvi wa kudumu kwa ngazi ya ulimwengu na haki ya kijamii.

Hii ni sehemu ya ujumbe wa maadhimisho ya Siku ya Uvuvi ulimwenguni wa Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo fungamani ya Binadamu, anayefafanua kwa kina na mapana nini maana ya siku hiyo na baaadhi ya changamoto wanazokabiliana wavuvi duniani. Ni ujumbe ulisomwa katika kilele cha Siku hiyo, katika Mkutano kwenye  Ofisi za FAO mjini Roma, ujumbe wake umeambatana na sala!

Siku ya uvuvi duniani kuangazia utumwa kwenye sekta hiyo

Katika kuadhimisha siku ya uvuvi ulimwenguni tarehe 21 novemba,  Kardinali Peter Turkson, anaendelea katika ujumbe huo: Kuwa na utambuzi wa umuhumu wa kuadhimisha siku hii ya uvuvi ulimwenguni, inatoa fursa na mwamko wa kufikiria hata takwimu za  FAO kwa mwaka 2016 ambazo zinawalenga wanafanya kazi wa aina zote, (muda, kudumu na kidogo) katika uvuvi, watu milioni  59,6  ambao ni karibia asilimia 14% walikuwa ni wanawake. Sehemu kubwa ya watu wanaojikita katuka sekta hii walikuwa ni watu wa bara la Asia kwa asilimia  85%, wakifuatia Afrika, Amerika ya Kusini na visiwa vya Carribien, kwa kuunda karibia milioni 171 ya tani ya samaki katika masoko ya dunia na kuonesha thamani ya kwanza ya kuuza  na uzalishaji wa mabilioni ya dola za kimarekani 320. Msululu katika ulimwengu wa thamani ya uvuvi , unajumishwa na uzalishai, kufanya kazi na kugawana pamoja na masoko ya bidhaa zinazotolewa kwa njia ya usaidizi karibia wa watu milioni 820.

Pamoja na hatua hizo bado kuna changamoto nyingi

Licha ya takwimu hizo zenye msingi, zinazoonesha umuhumu na mchango katika uvuvi wa usalama na wa vyakula, ukuaji wa uchumi na kupunguka kwa umaskini,  Kardinali Turkson anathibitisha kuwa, bado kuna idadi kubwa ya uwepo wa matatizo. Katika nafasi ya kwanza  ambayo unaweza kufikiria juu ya nguvu dhidi ya watu, unyonyaji dhidi ya wimbi la wavuvu ambayo inazidi kungezea idadi kubwa ya kesi za kazi sza suluba, biashara ya binadamu na kupotea kwa watu baharini, Pia kutokana na matatizo hayo unaweza kuunganisha moja kwa moja na uhalifu mwingine wa uvuvu haramu, kutojiandikisha  hata bila kuwa na kibali kutoka katika chombo husika IUU, uhalifu  ndani ya bahari. Hizo ni badhi lakini bado kuna changamoto nyingine zinazohusu na uchafuzi wa bahari na matatizo ya mazingira.

Kardinali Peter Turkson anasema, katika hali halisi hii ya uchungu, wafanyakazi wa uvuvi wanaomba msaada na sisi kama Kanisa hatuwezi kuziba masikio na kukaa kimya. Katika fursa ya maadhimisho ya miaka 70 mwaka 2018  ya Mkataba wa Dunia juu ya  haki za binadamu (D.U.D.U) tunatamani kuthibitisha juu ya Ibara ya 4 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa. Katika kipengele hicho kinaeleza kinagaubaga kuwa hakuna mtu anayestahili kugeuzwa mtumwa na wala kuwa mtwana wa mtu yeyote. Ingawa kwa miaka mingi nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimeridhia pia kutunga sheria za kuunga mkono ibara hii,lakini mabadiliko ya namna ya utumwa na utwana unavyotafsiriwa yameacha nyuma sheria nyingi.

Kardinali anaorodhesha baadhi ya vingele vya Ibara ya 23:kila mtu anayo haki ya kufanya kazi, kuchagua shughuli anayotaka,yenye hadhi ya kazi na ulinzi dhidi ya ukosefu wa ajira; kila mtu hasibaguliwe, anayo haki sawa na malipo sawa ya kazi; kila mtu anayo haki ya kupata mahali ya usalama na wakati huo huo hata katika familia yake kuwa na hadhi kwa mujibu wa maisha ya binadamu ya kushirikisha na ulazima wa kupata ulinzi katika jamii; kila mtu anayo haki ya kuwa na mwakili wa kuweza kutetea maslahi yake. Haki hizi za kazi ni msingi na haki za binadamu, ambazo zinapaswa kuwa hata kwa ajili ya wavuvi. Amethibitisha.Kwa utambuzi wa matatizo mengi yaliyopo dunia ya wavuvi, nchi wanachama na mashirika maalum ya Umoja wa Mataifa waliweza kukubaliana na zana tofauti za kimataifa ambazo kwa mswada uliowekwa katuka matendo kwa nchi zote, ambao unatakiwa utekeleze kubadili kwa dhati maisha ya wafanyakazi wa wavuvi na familia zao pamoja na mazingira hasa yale ya rasilimali ya maji.

Kukumbusha wosia wa Papa Francisko wa kuweka mtu kuwa kitovu na siyo fedha

Kama Kanisa tunataka kuukumbusha wosia wa Papa Francisko wa kuweka  mtu kwanza kama kitovu cha kila kitu. Na nyuma ya kila shughuli ikumbukwe kuwa kuna mtu. Kwa sasa kitovu cha shughuli za kifedha kulingana na kile cha uchumi wa kweli siyo kwa bahati mbaya; nyuma yake kuna aina  ya uchaguzi wa mtu ambao unafikiri unakosea  kwa maana ya kusema kuwa fedha zinafanywa na fedha. Na kumbe fedha za kweli ni zile zinafanywa kwa kufanya kazi. Ni kazi ambayo inampatia mtu hadhi na siyo fedha na kwa maana hiyo kazi halali inampatia mtu heshima anayohistahili mbele ya jamii.

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya uvuvi, Kardinali anawatakia matashi mema ya kuhamasisha daima juu ya hali halisi ya wavuvi na kuunda mazingira msingi katika maisha yao, na kuwataka mashirika yote ya kimataifa kuunganisha juhudi zao na kuacha pembeni zile tofauti, ukimbelembele na ili mwishowe waendelea kwa pamoja mchakato wa  kuelekea ul uenezaji wa mwema wa mkataba na wa zana za kimataifa. Ushirikiano unapaswa kufuatwa kwa ngazi ya ulimwengu, kikanda, kitaifa na mahalia ili kuhakikisha wanafuata vema maisha ya kijamii, viwanda na wanunuzi, hasa mashirika  yasiyo ya kiserikali , wadau wakala na Kanisa. Kufanya kazi kwa pamoja kunaweza kutusaidia kusitisha biashara ya binadamu, kazi za suluba baharini na kutoa ubora wa hali ya kazi na usalama, kupambana na uvuvi haramu na wahusika au wavuvi waweze kujidikisha katika chombo cha (IUU) na kuwa na matumaini ya kuuunda sekta ya uvuvi endelevu katika maono ya kijamii, mazingira na kibiashara!

21 November 2018, 14:30