Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko ameteua Askofu Santusi Lino Wanok,  kuwa katika jimbo la Nebbi Uganda Baba Mtakatifu Francisko ameteua Askofu Santusi Lino Wanok, kuwa katika jimbo la Nebbi Uganda  

Uganda:Jimbo la Lira kupewa Askofu Santusi Lino Wanok !

Askofu Santusi Lino Wanok, aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Nebbi ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa katika Jimbo la Lira nchini Uganda

Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, amekubali maombi ya kung’atuka katika shughuli za kuchungaji iliyowakilishwa na Askofu Giuseppe Franzelli, M.C.C.J, wa jimbo Katoliki ya Lira Uganda, wakati huo huo akamtea Askofu Santusi Lino Wanok, aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Nebbi kushika nafasi ya jimbo hilo.

Askofu Santusi Lino alizaliwa tarehe 7 Aprili 1957 katika kijiji cha Atyak-Yamo parokia ya Warr, Jimbo la Arua. Na majiundo yake ya kifalsafa katika seminari kuu ya kitaifa ya Alokolum, Gulu na Taalimungu katika Seminari Kuu ya Taifa ya Mtakatifu Maria huko Ggaba.  Alipata shahada ya uzamivu wa Taalimungu ya Kibiblia katika Chuo Kikuu cha Kipapa Urubaniano Roma.

Tarehe 27 Septemba 1986 akapata daraja Takatifu la upadre huko Arua na kupewa shughuli ya kichungaji katika sehemu hiyo.  Tarehe 23 Februari 1996 akaanza utume wa jimbo la Nebbi, Uganda. Kunako tarehe 8 Februari 2011 akateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Nebbi na kusimikwa rasimi tarehe 30 Aprili 2011 katika jimbo hilo la Nebbi.

 

 

23 November 2018, 16:47