Tafuta

Vatican News
Katika kipindi cha  AveMaria kwenye Tv2000, Cristina Parodi na padre Marco Pozza Katika kipindi cha AveMaria kwenye Tv2000, Cristina Parodi na padre Marco Pozza 

TV2000:Papa anazungumza juu ya uhusiano wa Maria na Yosefu!

Katika mwendelezo wa vipindi 11 vinavyoendelea katika Luninga ya Baraza la Maaskofu Italia(tv2000), kuhusu AveMaria, tarehe 20 Novemba saa 3.05 za usiku masaa ya Ulaya, kitakuwa ni kipindi cha sita. Papa Francisko anaelezea juu ya uhusiano kati ya Maria na Mchumba wake Yosefu. Mgeni rasmi ni Cristina Parodi mwandishi wa habari

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Yosefu alikuwa mchumba wa Maria na siyo mfanyakazi wa Mungu. Ndiyo uthibitisho wa Papa Francisko katika kipindi cha sita kuhusu Salam Maria, kipindi kinachoendeshwa katika Luninga ya Baraza la Maaskofu Italia (TV200) kwa ushirikiano ana Baraza la Kipapa la Mawasiliano ya  Vatican , ambacho kinaendeshwa saa 3.05 usiku masaa ya Ulaya, kila siku ya Jumanne, kwa kuongozwa na Padre Marko Pozza Mhusika wa Kanisa dogo katika Magereza ya Padova nchini Italia. Ni vipindi 11 vilivyo andaliwa ambapo tarehe 20 Novemba, imefikia kipindi cha sita kati ya vipindi hivyo. Utangulizi wa kipindi hicho, ni ufafanuzi wa Papa Francisko kuhusu mada hiyo ya Salam Maria ( AVE MARIA) na baadaye Padre Pozza anaendelea na mgeni mwingine kuelezea usozefu  wake wa maisha katika mahusiano ya dhati na Mama Maria.

Maria amejaa neema na Yosefu ni mwenye haki mwanaume wa kutunza Neno la Mungu

Maria alikuwa chini ya mchumba wake kwa mujibu wa utamaduni wa wakati ule. Mama Maria alikuwa akitayarisha chakula, akizungumza naye, kuzungumza na mtoto wake  na ambao walishikirikishana uchungu  alipokuwa na miaka 12 na akawa amebaki katika hekalu huko Yerusalem. Baba Mtakatifu Francisko anaelezea kuwa uchungu wa mme kwa ajili ya mke wake, ni kama uchungu wa kila wazazi. Hii inajihusisha katika hali halisi ya Bikira Maria, kwani katika maamuzi makubwa ambayo alikuwa anafanya Yosefu ilikuwa ni ya kawaida katika nyakati zile. Katika ndoto za Mama Maria mara nyingi alikuwa akipokea ujumbe wa Mungu. Yeye amejaa neema na  Yosefu ni mwenye haki, mwanaume anayejua kutunza Neno la Mungu na hivyo ni sura ya familia nzuri!

Upendo kwa ajili ya mwanae

Ili kuweza kufafanua vema juu ya uhusiano wa mtoto wake, Papa Francisko anakumbusha juu ya uzoefu wake alipokuwa nchini Argentina. Mara nyingi anathibithsa alikuwa akpitia mbele ya gereza la Villa Devoti ya Buenos Aires akiwa ndani ya Buas. Pale kulikuwapo na msululu wa mama wengi na walikuwa wanaonekana kwa na watu wengi. Wote walikuwa wanaona msululu wa wanawake wengi wakiwa katika sululu ili waweze kuingia ndani ya gereza ili kuwaona watoto wao. Na ili mwanamke aweze kuingia ndani ya gereza hilo, mara nyingi walinyenyekezwa sana kwa kukaguliwa. Lakini mama hao hawakujali,Baba Mtakatifu anathibitisha na kwamba, ni kwa sababu walikuwa wanafanya hivyo kwa ajili ya watoto wao. Kwa maana hiyo hata Maria alikuwa akimjali mwanae. Yeye hakujali ni kitu gani wengine wanasema. Lakini pale msalabani aliacha mtoto, si tu kwa sababu ya kuacha maisha, , Bali Mwanae anatupatia mama yake na ndipo anazaliwa katika msalaba.  

Mama wa Mungu na mama wetu sote

Katika kipindi cha sita kati ya kumi na mmoja, mgeni wa siku ya tarehe 20 Novemba 2018 ni mwandishi wa habari Cristina Parodi na Picha ya  Mama Maria wa Napoli, iliyochorwa na Gennaro Troia, ambapo Papa anabainisha kuwa, Maria ni Mama wa Mungu lakini Mungu ambaye anajipunguza na ndiyo maana tunaweza kutambua nini maana ya kile ambacho Mtakatifu Paulo katika Barua yake kwa Wafilipi alielezea kuhusu Mwana wa Mungu ya kwamba; Mungu alijinyenyekeza akawa mtii, naam, mauti ya msalaba na akabeba dhambi zetu zote. Paulo alikuwa akifikiri kuwa, Mungu alijifanya mwenye dhambi. Lakini yeye hakuwa na dhambi bali alijifanya mwenye dhambi kwa ajili yetu na kwa maana hiyo hata Mama ni kwa ajili ya wadhambi na kwa ajili yetu sisi sote.

20 November 2018, 11:33