Tafuta

Vatican News
Milioni 300 ya waamini wanaoteseka kwa njia ya ubaguzi au mateso mengine mengi yatokanayo na imani zao ni mwili na damu ya ndugu zetu katika imani Milioni 300 ya waamini wanaoteseka kwa njia ya ubaguzi au mateso mengine mengi yatokanayo na imani zao ni mwili na damu ya ndugu zetu katika imani  

Ripoti ya ACS:milioni 300 ya wakristo wanateswa!

Katika nchi 38 duniani wakristo na waamini wa madhehebu mengine wanabaguliwa au kuteswa. Ni taarifa iliyotolewa mjini Vatican mwishoni mwa wiki iliyopita na Ripoti ya XIV ya Chama cha Kipapa kwa ajili ya Kanisa hitaji (ACS)

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika dunia, mkristo mmoja kati ya saba anaishi katika nchi ambazo zina mateso ya hali ya kutoa wasiwasi na kutengeneza jumla ya zaidi ya milioni 300 ya waamini ambao wanateseka kwa njia ya ubaguzi au mateso mengine mengi yatokanayo na imani zao. Hawa ni mwili na damu ya ndugu zetu katika imani kwa idadi kubwa iliyooneshwa katika Ripoti ya XIV ya Chama cha Kipapa cha Kanisa hitaji iliyowakilishwa Roma katika Ubalozi wa Italia mjini Vatican wiki iliyopita.

Wakristo zaidi wanateswa

Katika ripoti ambayo inatoa takwimu za kipindi kuanzia mwezi Juni 2016, hadi Juni 2018, inaoneshwa kwa dhati kwamba, jumuiya za wakristo wenye kuamini ndiyo wanateseka zaidi, mitindo ya kusongwa na kutovumiliwa. Kadhalika kuna ongezeko kubwa la ukiukwaji wa uhuru wa dini kwa idadi kubwa ya madhehebu. Katika Tafiti zilizofanywa zinaonesha ajali na matukio ambayo yametokea na kukusanywa taarifa hizo. Lakini , shukrani kwa kazi nzuru ya mpango wa utafiti huo kupitia ushirikiano wa wengi katika mtandao unaounganisha zaidi ya nchi  150 duniani kote. Kadhalika katiuka ripoti inaonesha kuwa kuna uwepo wa kuta za utofauti na ukimya katika kesi za kulazimisha kubadili dini, ndoa za kulazimisha na za utoto, mashambulizi, uharibifu wa maeneo ya kufanyia mikutano na ibada na uharibifu wa zana za kidini, kukamatwa kwa watu bila hatia wakizingizwa kukufuru, kukamatwa kwa watu mbalimbali wanaojikita katika shughuli za dini, hata kuzuiwa kwa waamini katika kuendesha ibada za utaduni wazi ni sababu za mateso makubwa kwa wakristo na waamini wengine wa madhehubu ya wachache.

Tatifi zinaonesha kuwa ni nchi 38 ambazo zinaonesha  kuwa na hali mbaya ya ukiukwaji wa uhuru wa kidini, na nchi 21 kati yao zimeoneshwa kuwa ni nchi za mateso kama vile: Afghanistan, Saudi Arabia, Bangladesh, Birmania, China, Korea Kaskazini, Eritrea, India, Indonesia, Iraq, Libia, Niger, Nigeria, Pakistan, Palestina, Siria, Somalia, Sudan, Turkmenistan, Uzbekistan na Yemen. Nchi 17 ni maeneo yenye kuwa na ubaguzi kama vile:Algeria, Azerbaigian, Bhutan, Brunei, Misri, Shirikisho la nchi za Urusi, Iran, Kazakistan, Kirghizistan, Laos, Maldive, Mauritania, Qatar, Tagikistan, Uturuki, Ukraine  na Vietnam.

Hali imezidi kuwa mbaya katika mataifa mengi

Katika Ripoti hiyo inaendelea kuonesha kuwa, hali halisi ya nchi imezidi kuwa mbaya wakati wa kipindi cha kufanya tafiti katika nchi 17 kati ya 38 zilizooneshwa. Pamoja na hayo katika chi nyingine zikiwa ni Korea ya Kaskazi, Saudi Arabia, Nigeria, Afghanistan na Eritrea, hali inabaki bado kuwa tenge  kwani kwa mujibu wa chama cha Kipapa cha Kanisa Hitaji kinathibitisha hali halisi inayojitokeza kuwa hairidhishi kufutaia na hupatikanaji wa haki za watu wakati wanapokiri imani yao kwa uhuru.

Hata hivyo ripoti pia inaonesha kwamba licha ya wasiwasi uliopo, lakini pia kuna hata dalili  cheche  za matumaini  , kwa mfano kupungua kidogo  kwa kesi ya unyanyasaji uliokuwa ukifanywa na kikundi cha Kiislam cha al-Shabaab, ikiwa inamaani katika nchi ya Tanzania na Kenya mahlia ambapo hapo hawali zilikuwa zimeitwa kuwa ni nchi za mateso kwa kipindi cha mwaka 2016-2018. Kadhalika hata na ukosefu wa uaminifu kwa namna fulani wa nchi ambazo zilikuwa ninaficha kuenea kwa harakati mbaya katika baadhi ya  kanda za Afrika, nchi za Mashariki  na Asia!

RIPOTI ACS

 

 

 

27 November 2018, 10:04