Tafuta

Upendo na mshikamano wa Papa Francisko kwa ajili ya nchi ya Ukraine Upendo na mshikamano wa Papa Francisko kwa ajili ya nchi ya Ukraine 

Papa kwa ajili ya Ukraine:utume wa Vatican wa kibinadamu ni muhimu!

Upendo wa Papa Francisko, umefika nchini Ukraine na kwa njia ya wajumbe wa Vatican wakiongozwa na Kardinali Turkson siku zilizopita walifanya utume muhimu katika nchi ya Ukraine kuona na kuanzisha baadhi ya mipango ya kibinadamu kwa watu waliopatwa na migogoro hasa ya kivita

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kuanzia tarehe 14-18 Novemba,  Kardinali Peter Turkson, Rais wa Braza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu  na Monsinyo  Tejado Muñoz, katibu wake  walifanya ziara katika nchi za Mashariki ya Ulaya, kwa lengo la kuhakikisha hali halisi kwa baadhi ya mipango ya kibinadamu iliyo anzishwa kwa utashi wa Baba Mtakatifu katika mantiki ya mipango iliyopewa jina la “Papa kwa ajili Ukraine”. Pamoja nao waliambatana na Balozi wa Vatican nchini Ucraine Askofu Mkuu Claudio Gugerotti na maaskofu wengine.

Maisha ya watu

Hatua ya kwanza ya utume kitume ilikuwa katuka Mkoa Donetsk na  Kharkiv ambao walitesekana sana wakati wa upereshini ya wanajeshi iliyo anza kunako mwaka 2014 na migogoro mingine iliyofuata. Hapo wawakilishi wa Vatican waliktana na baadhi ya familia ambazo zimepewa msada wa vifaa vya kupasha nyumba zao joto. Kadhalika walitembelea Hospitali ya Kramatorsk, kituo cha afya kwa ajili ya viuongo vya mwili kwa ajili ya watoto, ambapo walitoa msaada wa mashine za kupima moyo; kituo cha kijamii kwa ajili ya maskini wasio kuwa na nyumba katika Parokia ya Maria Mpalizwa mbinguni huko Kharkiv;na mwisho katika nyumba ya mama na watoto waliotelekezwa  katika eneo la Korotych.

Mshikamano wa Papa

Mpango wa Papa kwa ajili ya Ukraina ulianishwa mwezi Juni 2016 mahali ambapo Baba Mtakatifu alipendekea kuonesha ukatibu na mshikamano kwa watu wa Ukraine na kwa namna ya pekee wale wanaoteka kwa ajili ya hali halisi iliyosabishwa na vita , bila kuwa na ubaguzi wa dini, imani au kabila. Shughuli na usimamizi huo umepewa Baraza la Kipapapa la maendeleo fungamani ya wato na ambao kwa ushirikiani wa Ubalozi wa kitume huko Ukraine na tume ya mafundi wa huko Zhaporizhia kwa mwaka wa kwanza na Sekretarieti ya mafundi huko Kiev, kwa mwaka wa pili ambao kwa kipindi chote hiki wameweza kuunda tamasha mbalimbali za upendo kwa ajili ya Kanisa na kuandaa matukio mbalimbali kwa ngazi ya kimataifa kwa ajili ya shughuli hiyo.

Matokeo mema ya mshikamano

Kwa kipindi cha miaka miwili, mpango huo umewezesha kukusanya euro milioni 16, ambayo ni matunda mema yaliyokusanywa katika majimbo yote katoliki barani Ulaya na fedha nyingine kutolewa na Baba Mtakatifu Francisko na kufika hata msaada kutoka kwa wafadhili karibia 900 .

22 November 2018, 14:35