Papa aridhia kutangazwa kwa wenyeheri wapya wa Kanisa
Sr. Angela Rwezaula - Vatican
Tarehe 8 Novemba 2018, Baba Mtakatifu Francisko, amekutana na na Kardinali Angelo Becciu Rais wa Braza la Kipapa la Kuwatangaza watakatifu, na kuridhia kuwatangaza baadhi kuwa wenye heri na kuwatambua wengine fadhila za kishujaa kuwa watumishi wa Mungu kumi.
Utambuzi wa wafiadini 11 watakaotangazwa kuwa wenyeheri
Wafia dini watatangwaza wenye heri 11 ambao ni Angelo Cuartas Cristóbal na na wenzake 8, waseminali wa Oviedo, waliouwawa kwa ajili ya kutetea imani yao huko Oviedo nchini Uhispania kati ya 1934 na 1937; Mariano Mullerat i Soldevila, Meli na baba wa familia alizaliwa Mtakatifu Coloma de Queralt (Uhispania) tarehe 24 Machi 1897 na kuwawaHuko El Pla, karibu na Arbeca (Uhispania) tarehe 13 Agosti 1936; Giacomo Alfredo Miller, Ndugu wa Shirika la Shule ya Wakristo aliyezaliwa Stevens Point (Marekani tarehe 21 Septemba 1944 aliuwawa kwa sababu ya kutetea imani yake huko Huehuetenango (Guatemala) tarehe 13 Februari 1982.
Baba Mtakatifu amerithia pia fadhila za kishujaa kwa watumishi wa Mungu 10
Hawa ni Giovanni Jacomo, Askofu Mkuu wa Mocisso,aliyekuwa pia askofu wa Caltanissetta; alizaliwa Ragusa (Italia) tarehe 14 Machi 1873 na kifo chake tarehe 25 Machi 1957; Alfredo Maria Obviar, Askofu wa Kwanza wa Lucena na Mwanzilishi wa Shrikia la Wamisionari wa Makatekisti wa Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu. Alizaliwa huko Lipa (Ufilippini) itarehe 29 Agosti 1889 na kifo chake huko Lucena (iilippini) il 1° ottobre 1978; - Giovanni Ciresola, Padre wa Jimbo, Mwanziloshi wa Shirika la Maskini wa Dada wa Damu Azizi . Karamu ya Upendo; alizaliwa huko Quaderni ya Villafranca (Italia) tarehe 30 Mei 1902 na kifo chake huko Quinto ya Valpantena (Italia) tarehe 13 Aprili 1987; Luigi Bosio, SPadre wa Jimbo; alizaliwa huko Avesa (Italia) tarehe 10 Aprile 1909 na kifo chake huko Verona (Italia) tarehe 27 Januari 1994.
Luigi Maria Raineri, mwanashirika wa Shirika la Mtakatifu Paulo (Wabarnabiti); alizaliwa huko Torino Italiwa tarehe 19 Novemba 1895 na kifo chake huko Crespano( Italia) tarehe 24 Novemba 1918; -Raffaella wa Mateso jina ubatizo Raffaella Veintemilla Villacís), Mwanzilishi wa Shirika lwa Wagostiniani Wana wa Mwokozi Mtakatifu; alizaliwa tarehe 22 Machi 1836 na kifo chake huko Lima (Peru) tarehe 25 novemba 1918; Maria Antonia wa Gesù (jina la ubatizo: Maria Antonia Pereira y Andrade), Mtawa wa Shirika la wakarmeli. Alizaliwa huko El Penedo (Uhipania) tarehe 5 Oktoba 1700 na kifo chake huko Santiago ya Compostela (Uhipania) tarehe 10 Machi 1760.
Arcangela Badosa Cuatrecasas, Mwanashirika la Watawa wa Bikira Maria wa Mlima Karmeli; alizaliwa huko Sant Joan les Fonts (Uhipania) tarehe 16 Juni 1878 na kifo chake huko Elda (Uhispania) tarehe 27 Novemba 1918; Maria Addolorata wa Moyo uliochomwa , (jina la ubatizo Maria Luciani), Mtawa wa Shirikwa la watawa wa Mateso ya Yesu Kristo; alizaliwa huko Montegranaro (Italia) tarehe 2 Mei 1920 na kifo chake huko Teramo (Italia) tarehe 23 Julai 1954; na Lodovico Coccapani, mlei wa Shirika la Wafrasiskani wasekulari , alizaliwa , huko Calcinaia (Italia) tarehe 23 Juni 1849 na kifo chake tarehe 14 Novemba 1931.