Mkutano wa kwaya Kimataifa kuanzia tarehe 22-25 Novemba 2018 mjini Vatican Mkutano wa kwaya Kimataifa kuanzia tarehe 22-25 Novemba 2018 mjini Vatican 

Mkutano wa III kimataifa wa kwaya mjini Vatican

Kuanzia tarehe 23-25 Novemba 2018, unafanyika mkutano wa III wa kimataifa wa kwaya kutoka pande zote za dunia, kwa ajili ya maadhimisho ya Sikukuu ya Mtakatifu Cecialia. Mkutano huo unafanyika mjini vatican kwa kuwaunganisha washiriki zaidi 8,000 kati yao ni waimbaji na wanamuziki kutoka mabara yote duniani

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Makanisa madogo ya muziki, kwaya za majimbo na maparokia, wanamuziki kutoka duniani kote wanarudi kukutana, kuanzia tarehe 23-25 Novemba 2018 katika Ukumbi wa Paulo VI , kwa ajili ya toleo la III la Mkutano wa Kimataifa wa kwaya Katika Sikukuu ya Mtakatifu Cecilia. Tukio hili limeandaliwa na Baraza la Kipapa la kuhamasisha uinjilishaji mpya kwa ushirikiano wa Chama cha Nova Opera, ambapo wanatazamia kuwaona mjini Vatican, washiriki zaidi 8,000 kati yao ni waimbaji na wanamuziki kutoka mabara yote duniani.

Tarehe 23 Novemba mada kuhusu muziki katika liturujia na katekesi

Mkutano wa kimataifa utafunguliwa Ijumaa 23 Novemba 2018 na mada kuhusu Muziki katika liturujia na Katekesi kwa ajili ya uinjilishaji mpya ambayo itatolewa na Monsinyo Marko Grisona, mbele ya wataalam mkuu wa muziki mtakatifu na liturujia,  Monsinyo  Guido Marini, mwalimu na mwadhimishaji wa Liturujia ya Baba Mtakatifu. Jean Paul Lécot, mtunzi na mpiga kinanda; monsinyo Vincenzo De Gregorio, Mkuu Taasisi ya Muziki Mtakatifu; padre Jordi Agustí Piqué, Mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Liturujia;Padre Óscar Valado Domínguez, mhusika wa muziki katika Baraza la Maaskofu wa Uhispania; padre Konstantin Reymaier, Mkuu wa Kitengo cha Muziki Mtakatifu katika Jimbo Kuu Vienna, na kijana mtunzi wa nyimbo padre  Fabio Massimillo, Mkurugenzi wa Kwaya ya Jimbo la Taranto.

Watakao shuhudia ni pamoja na waimbaji kutoka dunia nzima

Hata hivyo wageni waalikwa na watakaotoa ushuhuda ni waimbaji, wanafunzi na wanamuziki kutoka dunia nzima kama vile Marekani, Brazil, Afrika ya Kati, Lebanon, Iraq, Mexico, China, Vietnam na Uturuki. Jumamosi asubuhi tarehe 24 Novemba 2018, mkutano utaendelea na hotuba ya Kardinali Rino Fischella Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji mpya.

Saaa 11.30 asubuhi majiara ya Ulaya , wajumbe wote watashikiri mkutano na Baba Mtakatifu Francisko katika Ukumbi wa Papa Paulo VI. Na mchana katika ukumbu huo huo saa 12. Jioni, kutakuwa na Tamasha la wanakwaya itakayotolewa kwa heshima ya Mtakatifu Cecilia. Waimbaji wote wataweza kuima kwa sauti nne wakiongozwa na Monsinyo Marko Frisina. Zaidi ya wanakwaya 600 na bendi 70 wataimba kwa pamoja na zaidi ya watu 8,000 kwa kutengeneza sauti moja ya kwaya!

Tukio  litahitimishwa siku ya Jumapili 25 , misa na sala ya Malaika wa Bwana

Tukio hilo litahitimishwa siku ya Jumapili 25 Novemba 2018, saa 4 asubuhi katika maadhimisho ya Misa Takatifu katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro ikiongozwa na Kardinali Rino Fischella, Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji mpya. Na baada ya misa hiyo washiriki wote watakuwa tayari katika uwanja wa Mtakatifu Petro kushiriki na Baba Mtakatifu Francisko,tafakari na sala ya Malaika wa Bwana.

22 November 2018, 14:45