Muungano wa familia, unapoishi kwa namna ya kibinadamu na utakatifu kwa njia ya sakramenti ni njia ya kukua katika maisha ya neema Muungano wa familia, unapoishi kwa namna ya kibinadamu na utakatifu kwa njia ya sakramenti ni njia ya kukua katika maisha ya neema 

Kard.Farrell:kila mantiki ya familia ianzie na uzoefu!

Kardinali Farrel, Rais wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha katika ujumbe wake wa Mkutano wa Kitaifa wa uchungaji kifamilia wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Guatemala amehimiza juu ya kuanza na uzoefu kwa kila mantiki ya kinyumbani, kwa kuongozwa na Wosia wa Amoris laetitia

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

“Hasidharauliwe mtu, kwa maana anawakilisha udhati wake halisi na wakipekee ambao tunapaswa kuutambua, hivyo inahitaji kujikita kuweka nguvu zetu zote za kichungaji, si katika misingi ya mawazo ya kutaalimungu yasiyowezekana, bali katika uzoefu wa wahusika wa kila familia na kwa kila mantiki ya kinyumbani”. Hayo yamethibitiswa na Kardinali Kevin Joseph Farrell, Rais wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha katika ujumbe wake alioutuma katika fursa ya Mkutano wa XXII wa kitaifa wa uchungaji wa familia. Ni mkutano ulioandaliwa na Baraza la Maaskofu katoliki nchini Guatemala ambao umemalizika tarehe 11 Novemba 2018.

Matashi mema ya mkutano uweza kuwa kisima cha utajiri wa uzoefu wa dhati

Katika ujumbe wake, Kardinali Farrell anawatia moyo wajitajirishe katika sekta mbalimbali kwa kina ya utendaji wa kuchungaji, uliopendekezwa na Wosia wa Kitume Wa Papa Francisko wa Amoris laetitia. Zaidi, anatawakia matashi mema ya kwamba mkutano huo unaweza kuwa kisima cha utajiri wa uzoefu wa dhati na hali halisi ya waamini walei katika maisha yao ya familia na vyama, ili waweza kufikia makanisa mahalia katika uwelewa zaidi na wenye utajiri. Kardinali Farrell anasisitiza kuwa mchango wa Walei katika fadhila zao za wito wa ubatizo ni muhimu. Na hili kuthibitisha hiyo, amepitia katika vipengele mbali mbali vya Wosia wa Baba Mtakatifu Francisko wa Amoris laetita (AL).

Akiendelea na Wosia wa Amoris laetitia: Wema wa familia ni kwa ajili ya wakati endelevu katika dunia na katika Kanisa.  Mababa wa Sinodi wamekuwa na mtazamo juu ya hali halisi ya familia ya dunia nzima na kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anaona kuwa ni muhimu kutoa mchango wa kichungaji na kuwa na mtazamo wa hali halisi inayowahusu.  (AL 31). Wakati huo huo ni lazima kuwa wanyenyekevu na halisi kwa sababu ya utambuzi kuwa mwingine namna yetu ya kujiwakilisha ili wakristo waweze kuamini na kuvutia, lakini leo hii imeweza kuleta matatizo, kwa maana hiyo ni lazima kuwa makini na jinsi gani ya kuweza kuwajibika.

Njia ya kukua katika maisha ya neema

Muungano wa familia, unapoishi kwa namna ya kibinadamu na utakatifu kwa njia ya sakramenti kwa mara nyingine kwa wanandoa, ni njia ya kukua katika maisha ya neema. Na ndiyo fumbo la ndoa. Thamani ya muungano wa miili yao ni kieleleza cha maeneo kinachorohusiwa na mahali ambapo wanandoa wanakaribisha na wanashirikiana maisha yao yote. Kwa maana hiyo wao hawatakuwa peke yao na kwa nguvu zao wakati wa kukabiliana na changamoto za kibinadamu, bali watakuwa na Mungu. Wao wanaalikwa kujibu zawadi ya Mungu na wajibu wao wa kutunza familia na mapambano ya kila siku. Na wanaweza kila siku kuomba nguvu ya Roho Mtakatifu (AL 74)

Kuwasaidia wazee chini ya mantiki ya kiroho na kifamilia

Akiendelea na ujumbe wake kwa njia ya wosia wa Papa Francisko wa amoris Laetitia kwamba, sehemu kubwa ya familia inaheshimu wazee, kwa kuwazunguka kwa upendo na kuwafikiria kama baraka. Kutokana na hilo, ni pongezi maalum kwa mashirika na muungano wa vyama mbalimbali vya kifamilia ambavyo vinajikita kutoa mchango kuwasaidia wazee chini ya mantiki ya kiroho na kifamilia. Familia nyingi zinatufundisha uwezekano wa kukabiliana na hatua za mwisho za maisha kwa kukuza maana ya kweli ya kushirikisha na maisha ya fumbo la pasaka. Kanisa likiwa linapinga vizingiti Euthanaisa kwa njia ya matendo ya dhati, inahisi uwajibikaji wa kusaidia familia ambayo inajitoa kusaidia wazee wake na wagonjwa (AL 48).

Na hatimaye Kardinali Farrell anamalizia ujumbe wake akitazama kipengele cha huduma hasa kwa umanifu wa Kristo, ambapo  Papa Francisko katika Wosia wake wa Amoris laetitia anakumbusha kwamba, kuna kipindi cha hali ya juu katika nafasi na ambayo si katika  mazungumzo ya mafundisho kimaadili au kichungaji, badala yake ni  lazima yaweze kupata suluhisho katika  magesterio. Kwa asili Kanisa ni lazima kuunganika na mafundisho na hatua  zake, lakini hiyo pamoja nayo haizuii mitindo ya kutafsiri katika baadhi ya mantiki ya mafundisho au mahali yanapotekea.

Kwa maana hiyo  yatatokea hadi Roho Mtakatifu atakapotufikisha katika ukweli wote. Ikiwa na maana ya kwamba atakapojieleza kwa ukamilifu wa mafunzo ya Kristo, tutaweza kuona kila kitu na mtazamo wake. Na zaidi kila nchi au dini inaweza kutafuta suluhisho zaidi katika utamadunisho makini na kiutamaduni katika changamoto zake mahalia. Na kwa hakika tamaduni ni za aina nyingi kati yao na kila mmoja anatoa msingi wake ambao unahitaji kupanuliwa, kutamadunishwa na utendaji wake kwa dhati.

 

 

 

13 November 2018, 14:00